Msanii:'Je, Kariakoo ya miaka ishirini ijayo itakuaje?'

Kariakoo

Chanzo cha picha, Ngaira

    • Author, Esther Namuhisa
    • Nafasi, BBC Swahili
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Si majira ya asubuhi, mchana wala usiku, Kariakoo ni eneo ambalo mara zote linakuwa na pilika pilika nyingi za watu wakinunua na kuuza vitu, jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

"Ninakumbuka nikiwa mdogo, nilikuwa ninaenda na shangazi yangu kununua nguo na vyakula katika soko la Kariakoo" ni simulizi ambayo mchoraji wa picha hii , Ngaira Mandara alipata wazo la kusimulia hadithi za eneo hili marufu jjini Dar es salaam.

Ngaira anasema kwamba , rafiki yake ambaye alikuwa nje alimsimulia jinsi anavyoikumbuka Kariakoo hivyo alifunga safari na kwenda kuitembelea Kariakoo kwa dhumuni la kupata mchoro ambao utaweza kueleza historia ya eneo hilo.

"Kariakoo ni sehemu ambayo tunazunguka kila siku na kuwaona watu wakiwa na shughuli zao kila siku, lakini naamini kuwa kila mtu ana stori yake. Yule 'machinga' (Mchuuzi) kariakoo, kizazi kijacho kitafurahi kusikia kile alichokifanya .

Inawezekana Kariakoo tunayoiona sasa isifanane na Kariakoo ya miaka 20 ijayo lakini picha inaweza kutunza kumbukumbu", Ngaira ameeleza.

muonekano

Chanzo cha picha, Ngaira

Maelezo ya picha, Soko la Kariakoo katika muonekano wa nje

"Ninapenda kuchora watu na majengo ili kupata historia yake.

Ni majengo ambayo tunayaona kila siku, inawezekana labda kizazi cha sasa hawajui kuwa soko hili liko kama shimo ndani , au inawezekana kuna kipindi muonekano wa Kariakoo ukababadilika miaka ijayo.

Vivyo hivyo kwa upande wa watu, mfano nilichora picha ya mama anapika chapati na kuweka mtandaoni , watu wengi wakikuja kuandika namna wanavyokumbuka eneo wanalonunua chapati na vitu gani wanavifurahia.

Napenda kupata simulizi za watu wengine kupitia picha, nataka watu kukumbuka historia za maisha waliopitia, mitaa walioishi na kukumbuka wapi walitoka na wapi walipo sasa" Ngaira alieleza.

mchoraji

Chanzo cha picha, Ngaira

Maelezo ya picha, Ngaira Mandara, Mchoraji
Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Simulizi ambazo tutasema kwa watoto na wajukuu au kizazi kijacho, picha inasimulia vizuri zaidi.

Kariakoo ni makazi pia ya watu, je maisha ya watu wanaokaa katika eneo hilo yakoje?

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Upande wa ndani wa soko la Kariakoo

Chanzo cha picha, Ngaira

Maelezo ya picha, Upande wa ndani wa soko la Kariakoo

Kariakoo ni soko ambalo watu kutoka maeneo mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi ufika hapo kwa ajili ya kufanya biashara au kufanya manunuzi.

Umaarufu wa soko hilo ni historia inayotokana na gharama kuwa nafuu na upatikanaji wa bidhaa kwa urahisi.

Hata kuna wanaokumbuka mtaa mfani ndio lazima ukutane na vibaka mfano 'mtaa wa kongo' ulipata umaarufu kwa kuwa na vibaka hivyo watu wanapaswa kuwa makini.

Mavazi pia ni jambo ambalo linazingatiwa katika mtaa huo.

hatua ya awali

Chanzo cha picha, Ngaira

Ngaira Mandara ni mchoraji mwenye umri wa miaka 28, anasema kuwa alianza kupenda kuchora tangu alipokuwa shule ya msingi.

Na mwaka 2016 ndio alipoamua kufanya sanaa kuwa kazi yake rasmi.

Ngaira anachora kwenye makaratasi au ubao , anafanya sanaa ya uchoraji wa kidigitali ambao kila kifaa cha kuchora anakipata kwenye komputa na vilevile anachora michoro inayosogea maarufu kama 'animation'.

Michoro hii huwa anaiweka katika bidhaa kama nguo, chupa za maji,vikombe, mabegi na picha za ukutani.