Ufahamu ujumbe wa michoro iliyochongwa katika mawe ya Nyero wilayani Kumi nchini Uganda

Maeneo matatu yenye mawe makubwa wilayani Kumi mashariki mwa Uganda yana michoro ya kale yenye umri wa karne kadhaa za nyuma. Je michoro hiyo ina maana gani?

Nyero rocks
Maelezo ya picha, Michoro ya mviringo yanaonekana kuchongwa katika mawe makubwa wilayani Kumi nchini Uganda.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Hili ni eneo la ukumbusho la 'Nyero Rock Paintings' mjini Kumi.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Inasemekana kuwa, zaidi ya miaka 3000 iliyopita, jamii ya mbilikimo ya Batwa iliishi hapa.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Jamii hiyo ilichonga michoro iliyoashiria au kuangazia hali yao ya maisha.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Baadhi ya michoro hiyo ni mviringo, ama mduara, ikiwakilisha jua ambalo waliabudu kama “Mungu” wao.
Nyero rocks

Chanzo cha picha, 6

Maelezo ya picha, Pia kuna mchoro wa Mamba, ambaye anasemekana alikuwa katika ziwa la karibu na eneo hilo, aliyewaua wengi wa wakaazi wao.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Kadhalika kuna mchoro wa “ngazi” kwa sababu jamii hiyo walikuwa wafupi, walihitaji ngazi ili kufikia maeneo ya juu.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Michoro hii imejaa ndani ya mapango ambayo jamii hiyo ya Batwa walikuwa wakiishi.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Mapango hayo yako chini sana, huenda sababu ni kutokana na kuwa wao walikuwa watu wafupi.
Nyero Rocks
Maelezo ya picha, Kwa sasa eneo hilo ni kivutio kikuu cha utalii nchini na bado lina umuhimu mkubwa wa kishirikina kwa jamii ya watu wanaoishi mashariki mwa Uganda.
Nyero rocks
Maelezo ya picha, Wengi huenda katika enoe hilo ili kutoa dua zao wakiwa na imani kwamba watafanikiwa. Wanawake walio na matatizo ya kupata watoto pia huenda kuomba ndani ya mapango hayo wakiamini watafanikiwa kushika mimba na kujifungua watoto.