Uchambuzi wa Titanic ulivyogundua kuhusu saa za mwisho za meli kabla ya kuzama

Chanzo cha picha, Atlantic Productions/Magellan
Uchambuzi wa kina wa uchunguzi kwa kidijitali wa Titanic umefichua mapya kuhusu saa za mwisho za meli iliyokuwa hatarini.
Mfano halisi wa 3D unaonesha vurumai za jinsi meli hiyo ilivyopasuka vipande viwili ilipozama baada ya kugonga jiwe la barafu mnamo 1912, watu 1,500 walipoteza maisha katika janga hilo.
Uchambuzi unatoa mwonekano mpya wa chumba cha boiler (kifaa cha kuzalisha mvuke), kuthibitisha madai ya mashuhuda ambao wahandisi walifanya kazi hadi mwisho ili kuwasha taa za meli.
Na uchunguzi wa kompyuta pia unaonesha kwamba matundu ya ukubwa wa vipande vya karatasi za A4 katika meli yenye yalichangia kuzama kwa meli hiyo.

Chanzo cha picha, Atlantic Productions/Magellan
"Titanic ndiye shahidi wa mwisho wa maafa, na bado ina hadithi za kusimulia," alisema Parks Stephenson, mchambuzi wa Titanic.
Uchambuzi huo umechunguzwa kwa filamu mpya ya National Geographic and Atlantic Productions iitwayo Titanic: The Digital Resurrection.
Ajali hiyo, ambayo iko mita 3,800 chini katika maji ya barafu ya Atlantiki, ilichorwa kwa kutumia roboti za chini ya maji.
Zaidi ya picha 700,000, zilizochukuliwa kutoka kila pembe, zilitumiwa kuunda "pacha wa kidijitali", ambaye alifichuliwa kwa ulimwengu pekee na BBC News mnamo 2023.
Kwa sababu ajali hiyo ni kubwa sana na iko katika utusitusi wa kina kirefu, kuichunguza kwa kutumia vitu vya chini vya maji huonesha tu vijipicha vya kustaajabisha. Uchambuzi, hata hivyo, unatoa mwonekano kamili wa kwanza wa Titanic.
Gubeti (bow) iko wima juu ya sakafu ya bahari, kana kwamba meli inaendelea na safari yake.
Lakini ukiwa umbali wa mita 600, sehemu ya nyuma ni chuma kilichochongwa. Uharibifu huo ulitokana na kugonga sakafu ya bahari baada ya meli hiyo kukatika katikati.

Chanzo cha picha, Atlantic Productions/Magellan
Teknolojia mpya ya uchoraji ramani inatoa njia tofauti ya kuisoma meli.
"Ni kama eneo la uhalifu: unahitaji kuona ushahidi ni nini, katika muktadha wa mahali ulipo," Parks Stephenson alisema.
"Na kuwa na mtazamo wa kina wa eneo zima la ajali ni muhimu kuelewa kilichotokea hapa."
Uchunguzi unaonesha maelezo mapya ya karibu, ikiwa ni pamoja na uwazi ambao kuna uwezekano mkubwa ulitokana na kuvunjwa na mwamba wa barafu.
Inalingana na ripoti za mashuhuda walionusurika kwamba barafu iliingia kwenye vyumba vya watu wengine wakati wa mgongano huo.

Chanzo cha picha, Atlantic Productions/Magellan
Wataalamu wamekuwa wakichunguza moja ya vyumba vikubwa vya boiler vya Titanic, ni rahisi kuonekana kwenye skana kwa sababu iko nyuma ya sehemu ya meli iliyovunjika vipande viwili.
Abiria walisema kuwa taa zilikuwa bado zimewashwa huku meli ikizama chini ya mawimbi.
Rudufu ya kidijitali inaonesha kwamba baadhi ya boiler zina umbo la kutumbukia (concave), ambayo inaonesha kwamba zilikuwa bado zinafanya kazi wakati zilipozama majini.
Wote walikufa katika janga hilo lakini vitendo vyao vya kishujaa viliokoa maisha ya watu wengi, alisema Parks Stephenson.
"Waliweka taa na nguvu kazi hadi mwisho, ili kuwapa wafanyakazi muda wa kuwasha boti za kuokoa maisha kwa usalama na mwanga badala ya giza totoro," aliiambia BBC.

Chanzo cha picha, Atlantic Productions/Magellan
Rudufu mpya pia imetoa maarifa zaidi kuhusu kuzama kwa chombo hicho.
Inachukua mfano wa kina wa muundo wa meli, iliyoundwa kutoka kwenye michoro ya Titanic, na pia habari kuhusu kasi yake, mwelekeo na kusimama, kutabiri uharibifu uliosababisha ilipogonga barafu.
"Tulitumia seti ya kanuni za hesabu za hali ya juu, uundaji wa kielelezo wa kikokotozi na uwezo wa kutumia kompyuta kubwa zaidi kuunda upya kuzama kwa Titanic," Prof Jeom-Kee Paik, kutoka Chuo Kikuu cha London, aliyeongoza utafiti huo alisema.
Rudufu hiyo inaonesha kwamba meli ilipopiga tu kishindo dhidi kwenye kilima cha barafuilikumbwa na msururu wa milipuko kwenye sehemu ya chombo hicho.

Chanzo cha picha, Jeom Kee-Paik/ University College London
Titanic ilipaswa kuwa isiyoweza kuzama, iliyobuniwa kusalia ikielea hata ikiwa vyumba vyake vinne visivyopitisha maji vimefurika.
Lakini Rudufu inatathimini uharibifu wa barafu ulioenea katika sehemu sita.
"Tofauti kati ya kuzama kwa Titanic na kutozama iko chini ya ukingo mzuri wa mashimo ya ukubwa wa kipande cha karatasi," alisema Simon Benson, mhadhiri mshiriki katika usanifu wa majini katika Chuo Kikuu cha Newcastle.
"Lakini shida ni kwamba mashimo hayo madogo yamesambaa juu ya sehemu kubwa ya urefu wa jumla wa meli, kwa hivyo maji ya mafuriko huja polepole lakini kwa hakika kwenye mashimo hayo yote, na hatimaye vyumba vinafurika juu na Titanic inazama."
Kwa bahati mbaya uharibifu hauwezi kuonekana kwenye kwenye picha za skena kwani sehemu ya chini imefichwa chini ya mchanga.

Chanzo cha picha, Atlantic Productions/Magellan
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga












