Vitu vya nadra vilivyopatikana katika Titanic vinavyotunzwa katika ghala la siri

Muda wa kusoma: Dakika 7

Rebecca Morelle, mhariri wa sayansi , na Alison Francis

BBC News

g

Mkoba uliotengenezwa kwa ngozi ya mamba na chupa ndogo za manukato ambayo bado yanatoa harufu kali ni baadhi tu ya mabaki ya thamani yaliyopatikana kutoka kwa meli maarufu zaidi duniani iliyozama - Titanic.

Mahali halisi pa ghala ambako vitu hivi vimehifadhiwa ni siri inayolindwa kwa karibu, kutokana na thamani ya vitu vilivyomo Tunachoweza kusema ni kwamba ni mahali fulani huko Atlanta, Georgia, Marekani.

Maelfu ya vitu vimejaa: kuanzia kwenye kidimbwi cha bafu kilichogeuzwa liyogeuzwa hadi glasi iliyochongwa na vitufe vidogo.

BBC ilipewa fursa adimu ya kuangalia karibu na kituo cha kuhifadhia vitu hivyo na hivyo kugundua hadithi zilizo nyuma ya baadhi ya vitu hivi.

Unaweza pia kusoma:
g
Maelezo ya picha, RMS Titanic ikiondoka Belfast kwa majaribio ya safari ya baharini, 1912

Mkoba wa mamba unaoficha hadithi ya kusikitisha

"Ni mkoba mzuri sana, wa mtindo wa kuvutia," anasema Tomasina Ray, mkurugenzi wa RMS Titanic Inc, kampuni ambayo imepata mabaki haya.

Kampuni hiyo ya Marekani ina haki za kukusanya mabaki ya meli hiyo na kwa miaka mingi imekusanya vitu 5,500 kutoka kwenye eneo la kifusi cha meli , ambavyo baadhi yake huchaguliwa na kuwekwa kwenye maeneo ya maonyesho katika maeneo mbali kote ulimwenguni.

Mkoba huo umetengenezwa kwa ngozi ya mamba , ambayo imenusurika miongo kadhaa katika kina cha Atlantiki ya Kaskazini.

Vitu hivyo nyeti ndani vimehifadhiwa pia, vikifichua maelezo ya maisha ya mmiliki wake - abiria wa daraja la tatu aitwaye Marian Meanwell.

"Alikuwa na umri wa miaka 63," anasema Tomasina. "Na alikuwa akisafiri kwenda Marekani kuwa na binti yake ambaye alikuwa mjane karibuni."

Miongoni mwa vitu vilivyokuwemo ndani yake ilikuwa picha iliyofifia, inayodhaniwa kuwa ya mama wa Marian Meanwell.

f

Pia kulikuwa na makaratasi ambayo angehitaji kwa maisha yake mapya nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na barua ya kumbukumbu iliyoandikwa kwa mkono kutoka kwa mwenye nyumba wake wa zamani huko London. Inasema: "Tumekuwa tukimuona Bi Meanwell kuwa mpangaji mzuri, mwenye kulipa haraka malipo."

Kadi yake ya matibabu ilikuwa ndani pia, kwani abiria wote wa daraja la tatu walihitaji kuthibitisha kuwa hawakuleta ugonjwa nchini Marekani.

Marian Meanwell alikuwa amewekwa kwenye meli ya Majestic - meli nyingine ya White Star Line. Lakini haikusafiri, kwa hivyo kwenye kadi, Majestic ilivuka na mzigo wake ikinaonyesha kuwa alihamishiwa kwenye Titanic na akawa mmoja wa watu 1,500 waliopoteza maisha yao.

"Kuwa na uwezo wa kuelezea hadithi yake na kuwa na vitu hivi ni muhimu sana," anasema Tomasina.

"Kwa upande mwingine, yeye ni jina linguine lililowekwa kwenye orodha."

f

Manukato ambayo bado yamefungwa

Vitu ambavyo viliwea kunusurika pia vimeokolewa kutoka chini ya bahari.

Tomasina anapofungua chombo cha plastiki unahisi harufu nzuri ya kupendeza inajaa hewani . " Ni harufu kali sana ," anakiri.

Ndani kuna chupa ndogo za manukato. Chupa huzi zimefungwa na kufunikwa , lakini harufu yake kali inaweza kutoka na ukaihisi , hata baada ya kuwa ndani ya bahari kwa miongo.

"Kulikuwa na muuzaji wa manukato na alikuwa na zaidi ya chupa hizi ndogo 90 za manukato," Tomasina anaelezea.

Jina lake lilikuwa Adolphe Saalfeld na alikuwa akisafiri kama abiria wa daraja la pili.

Saalfeld alikuwa mmoja wa watu 700 walionusurika. Lakini huku wanawake na watoto wakipewa kipaumbele wakati wa zoezi la kuwaokoa watu, baadhi ya wanaume walioitoa meli hiyo walibaki na wasiwasi.

"Alikuwa amefariki wakati tulipopata chupa hizi ," anasema Tomasina. "Lakini ni ufahamu wangu kwamba aliishi na hatia kidogo - hatia ya manusura."

Maisha ya champagne

f

Pia katika mkusanyiko wa vitu hivi kuna chupa ya champagne - iliyojaa na champagne ndani yenye kifuniko juu.

"Maji kidogo labda yangeingia kupitia kifuniko chake na kisha ikakaa chini ya bahari, "anasema Tomasina.

Wakati Titanic ilizama mnamo 1912, baada ya kugonga barafu, meli iligawanyika na vitu vilivyokuwemo vikamwagika na kusababisha eneo kubwa la uchafu.

"Kuna chupa nyingi kwenye sakafu ya bahari na sufuria nyingi za jikoni pia, kwa sababu Titanic ilivunjika karibu na moja ya eneo la jiko," anasema Tomasina.

Kulikuwa na maelfu ya chupa za champagne kwenye makabati. Mmiliki wa meli hiyo alitaka abiria wake wa daraja la kwanza kupata uzoefu wa mzuri katika meli hiyo, kwa ujumla kwa chakula bora na vinywaji vya kutosha.

f
Maelezo ya picha, Kifusi cha meli ya Titanic iliyopata ajali

"Ilikuwa kama jumba la kifalme linaloelea na Titanic ilipaswa kuwa meli ya kifahari zaidi," anasema Tomasina.

"Kwa hiyo kuwa na champagne, kuwa na mazoezi, kuwa na huduma hizi zote na mambo haya mazuri kwa abiria ingekuwa muhimu sana kwao."

f
Maelezo ya picha, Meli ya Titanic ilikuwa na eneo la mazoezi ya viungo (gym)

Kufungua viunganishi (pini) vya vipuli vya meli

Titanic ilikuwa katika safari yake ya kwanza, ikisafiri kutoka Southampton kwenda Marekani, wakati alipogonga barafu.

Meli hiyo ilikuwa na sifa za hali ya juu za usalama kwa wakati huo na ilisemekana kuwa haiwezi kuzama.

Tomasina anatuonyesha baadhi ya viunganishi vya vyuma vya meli, pini za chuma ambazo zilishikilia sahani zake za chuma pamoja.

Kulikuwa na zaidi ya milioni tatu.

"Wakati Titanic ilipozama, kulikuwa na nadharia kwamba walikuwa wakitumia vifaa vya kiwango cha chini labda, na hiyo ndio iliyosababisha kuzama kwa kasi," Tomasina anaelezea.

f

Baadhi ya viunganishi hivi vimefanyiwa majaribio ili kuona ikiwa vina uchafu wowote.

"Kulikuwa na viwango vya juu vya kutu katika viunganishi hivi, ambayo ni nyenzo kama kioo ambacho ambayo huenda huvifaya kuwa vidogo zaidi katika baridi," anasema.

"Kama pini hizi zilisinyaa na moja ya viunganishi hivi vikatoka kwa urahisi zaidi, basi huenda ilikuwa ni sehemu ambapo barafu ingeweza kupiga na kusababisha ajali ."

Tomasina anasema bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu jinsi meli hiyo ilivyozama.

"Tunaweza kusaidia kuangalia nadharia, kwa hivyo kuweza kuchangia sayansi na hadithi hiyo nyuma yake ni kitu ambacho tunafurahi sana kukifanya."

Mgawanyiko wa madaraja

Maisha ndani ya meli ya Titanic yalitofautiana kulingana na madaraja ya kijamii - hata chini ya vikombe na sahani ambazo wangezitumiwa kunywa na kula.

Vikombe vyeupe vya udongo vya darasa la tatu ni rahisi na imara , na vilikuwa na nembo ya Nyota Nyekundu .

Sahani ya daraja la pili ina mapambo mazuri ya maua ya bluu na inaonekana nzuri kidogo.

Lakini sahani ya chakula cha jioni ya daraja la kwanza imetengenezwa na China maridadi zaidi. Ina nakshi ya dhahabu.

Abiria matajiri wa daraja la kwanza walipewa huduma ya fedha kwa ajili ya chakula chao - lakini katika daraja la tatu, ilikuwa hadithi tofauti.

"Wasafiri wa daraja la tatu walitumia sahani ya China pia - lakini ilikuwa dhahiri kuwa kutokana na kiwango chake kuwa cha chini kuliko za madaraja ya chini mstari wa nakshi yake ulionekana kuchaa ," anaelezea Tomasina.

f

RMS Titanic Inc ni kampuni pekee inayoruhusiwa kisheria kurejesha vitu kutoka kwenye tovuti hiyo - ilipewa haki hii na mahakama ya Marekani mnamo 1994. Lakini inapaswa kufanya hivyo chini ya hali ya masharti makali - vitu lazima vibaki pamoja kila wakati, kwa hivyo haviwezi kuuzwa kando, na vinapaswa kuhifadhiwa vizuri.

Hadi sasa, mabaki yote yamekusanywa kutoka kwenye eneo lenye uchafu baharini.

Lakini hivi karibuni kampuni hiyo imezua utata ikisema kuwa inataka kupata vitu kutoka kwa meli yenyewe - ikiwa ni pamoja na vifaa vya redio Macroni iliyotumiwa kupiga simu za wasafiri waliokuwemo walipokuwa wakitaka usaidizi simu kutoka katika Titanic usiku wakati meli hiyo ilipozama.

f
Maelezo ya picha, Kidimbwi cha kuogelea cha bafuni katika mabaki ya Titanic
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wengine wanaamini kuwa mabaki hayo ni eneo la kaburi na linapaswa kuachwa.

"Titanic ni kitu ambacho tunataka kukiheshimu," Tomasina anasema katika kujibu.

"Tunataka kuhakikisha kwamba tunahifadhi kumbukumbu, kwa sababu sio kila mtu anaweza kwenda chini ya Titanic, na tunataka kuwa na uwezo wa kuleta taarifa zake kwa umma."

Chumba zaidi kinaweza kuhitajika hivi karibuni kwenye kabati za ghala hili la siri.

Safari ya hivi karibuni ya kampuni hiyo kwenye wavuti imehusisha kuchukua mamilioni ya picha za mabaki ili kuunda skani ya kina ya 3D.

Na, pamoja na kuchunguza hali ya sasa ya chumba cha redio cha Marconi, timu pia imekuwa ikitambua vitu katika eneo la uchafu ambao wangependa kupata katika mbizi za baadaye.

Nani anajua watakachopata na ni hadithi gani ambazo hazijulikani kila kitu kinaweza kufunua taarifa nyingi kuhusu ajali mbaya ya Titanic na abiria wake.

Haki miliki ya picha Marian Meanwell: Patricia Chopra /Encyclopedia Titanica; Adolphe Saalfeld: Kumbukumbu ya Astra Burka; Mabaki ya Titanic: RMS Titanic Inc; Sanaa ya Titanic: Kevin Church / BBC; Picha za kihistoria: Getty.

Uundaji wa Lilly Huynh

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi