Picha mpya zinazoonyesha jinsi Meli ya Titanic inavyooza chini ya bahari

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc
Ilikuwa ni picha iliyofanya kifusi cha meli ya Titanic iliyopata ajali kutambulika mara moja kikionekana kwenye eneo la giza la kina cha bahari ya Atlantiki.
Lakini uvumbuzi huu mpya umefichua athari za kuoza taratibu kwa sehemu kubwa ya mabaki ya meli hiyo iko kwenye sakafu ya bahari.
Mabaki ya meli hiyo yaligunduliwa wakati wa msururu wa upigaji wa roboti za chini ya maji katika msimu huu wa kiangazi.
Picha zilizochukuliwa na roboti hizo zinaonyesha jinsi kifusi hicho cha Titanic kilivyobadilika baada ya zaidi ya miaka 100 chini ya mawimbi ya bahari.
Meli hiyo ilizama Aprili 1912 baada ya kugonga jiwe la barafu, na kusababisha vifo vya watu 1,500.

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc
"Muundo wa upinde wa Titanic ni wa kipekee – na ni wa nyakati zote - na ndivyo unavyofikiria unapofikiria ajali ya meli. Lakini sasa hauonekani hivyo tena,” alisema Tomasina Ray, mkurugenzi wa ukusanyaji wa vifusi katika taasisi ya RMS Titanic Inc, kampuni iliyofanya ugunduzi huo.
"Ni ukumbusho mwingine tu wa kuoza kwa meli unaotokea kila siku. Watu huuliza kila mara: 'Titanic itakuwa huko kwa muda gani?' Hatujui lakini tunaitazama na kuifuatilia kwa wakati halisi."

Chanzo cha picha, Alamy
Timu ya wagunduzi hao inaamini kuwa sehemu ya kifusi cha Titanic, ambayo ina urefu wa mita 4.5 (14.7ft) ilimeguka na kudondoka wakati fulani katika miaka miwili iliyopita.
Picha na uchunguzi wa skani iliyotolewa na wagunduzi 2022 wa kampuni ya ramani ya bahari kuu ya Magellan na waundaji wa filamu Atlantic Productions zinaonyesha kuwa vifusi bado vilikuwa yameambatishwa - ingawa vilikua vimeanza kuoza na kuachana.
"Wakati fulani chuma kilimeguka na kuanguka," Tomasina Ray alisema.

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sio sehemu pekee ya meli, ambayo iko mita 3,800 chini, ambayo inatoweka baharini tu. Muundo wa chuma pia unaliwa na vijidudu, na kutengeneza kutu inayoitwa rusticles.
Safari za awali zimegundua kuwa sehemu za Titanic zinameguka na kudondoka. Upigaji mbizi ulioongozwa na mgunduzi Victor Vescovo mnamo 2019 ulionyesha kuwa sehemu ya meli hiyo iliyokuwa ofisi ya maafisa wake ilikuwa ikiporomoka, na kuharibu vyumba na kuzifanya sehemu kama vile bafu la nahodha lisionekane.
Safari hii ya majira ya kiangazi ya RMS Titanic Inc ilifanyika Julai na Agosti.
Roboti mbili zinazoongozwa (ROVs) zilichukua zaidi ya picha za video milioni ambazo zilichukuliwa kwa muda wa saa 24, na kutoa picha za ufafanuzi wa hali ya juu za mabaki yote mawili, ambayo yalimeguka.
Kampuni sasa inakagua kwa makini video hizo ili kuorodhesha matokeo na hatimaye itaunda uchunguzi wa kina wa 3D wa eneo lote la ajali.
Picha zaidi kutoka kwa roboti hizo zitafichuliwa katika miezi ijayo.

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc
Timu hiyo pia imetangaza ugunduzi mwingine wa picha ambayo walikuwa wakitarajia kupata.
Mnamo 1986 sanamu ya shaba iitwayo Diana wa Versailles ilionekana na kupigwa picha na Robert Ballard, ambaye aligundua mabaki ya Titanic mwaka mmoja kabla.
Lakini eneo lake halikujulikana na takwimu ya kifusi hicho chenye urefu wa 60cm haikuandikwa tena, ingawa sasa, imegunduliwa ikiwa imepinduka kwenye kwenye sakafu ya bahari.
"Ilikuwa kama kupata sindano kwenye tundu la nyasi, na ugunduzi wa mwaka huu ulikuwa muhimu tena," alisema James Penca, mtafiti wa Titanic na mtangazaji wa podcast ya Witness Titanic.
Sanamu hiyo iliwahi kuonyeshwa abiria wa daraja la kwanza wa Titanic.
"Sebule ya daraja la kwanza ilikuwa chumba kizuri zaidi, na cha kina sana kwenye meli. Na kitovu cha chumba hicho kilikuwa ni ukumbi wa Diana wa Versailles," alisema.
"Lakini kwa bahati mbaya, Titanic ilipogawanyika vipande viwili wakati wa kuzama, chumba cha mapumziko kilipasuka. Na katika uharibifu huo, sanamu ya Diana ilivuliwa vazi lake na kutupwa kwenye giza la eneo la taka." la bahari.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni ya RMS Titanic Inc ina haki za kuokoa vifusi vya Titanic, na ndiyo kampuni pekee inayoruhusiwa kisheria kuondoa bidhaa kwenye eneo la ajali.
Kwa miaka mingi, kampuni hiyo imepata maelfu ya vitu kutoka kwa eneo la uchafu, ambavyo baadhi yake vinaonyeshwa katika maeneo mbali mbali kote ulimwenguni.
Wanapanga kurejea mwaka ujao ili kufanya ugunduzi zaidi - na sanamu ya Diana ni mojawapo ya vitu ambavyo wangependa kuviokoa.
Lakini wengine wanaamini kuwa ajali hiyo ni kaburi ambalo linapaswa kuachwa bila kuguswa.
"Ugunduzi huu wa sanamu ya Diana ndio hoja kamili dhidi ya kuachana na Titanic," Bw Penca alisema akijibu.
"Hiki kilikuwa kipande cha sanaa ambacho kilikusudiwa kutazamwa na kuthaminiwa. Na sasa kipande hicho kizuri cha sanaa kiko kwenye sakafu ya bahari... katika giza nene jeusi ambako imekuwa kwa miaka 112.
"Ili kumrudisha Diana ili watu waweze kumuona kwa macho yao wenyewe - thamani yake, kuamsha upendo wa historia, nisingependa kamwe kuiacha sanamu hiyo kwenye sakafu ya bahari."
Taarifa ya ziada na Kevin Church
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












