Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2025: Tume ya Uchaguzi INEC yaendelea kutoa matokeo

.

Chanzo cha picha, NEC

Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa Uchaguzi Tanzania
Muda wa kusoma: Dakika 1

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imetangaza matokeo kutoka takribani mikoa 80 kati ya mikoa 100 nchini, kituo cha utangazaji cha serikali TBC kinaonyesha.

Haya yanajiri licha ya maandamano kushuhudiwa nchini humo kwa siku ya tatu mfululizo,licha ya Mkuu wa Majeshi la kuwaamuri kukomesha vitendo vya vurugu.

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushinda uchaguzi huo kwa tiketi ya Chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimetawala nchi tangu uhuru mwaka 1961.

Matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Tanzania Bara yanatarajiwa kutangazwa Jumamosi.

Visiwani Zanzibar - ambako wananchi humchagua rais wao - Hussein Mwinyi wa chama tawala cha CCM, ambaye alikuwa anagombea muhula wa pili, ameshinda uchaguzi huo kwa aslimia 80 ya kura.

Hata hivyo upinzani huko Zanzibar unadai uchaguzi huo umekumbwa na "udanganyifu mkubwa", shirika la habari la AP liliripoti.

Kwa Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2025 Bonyeza hapa: