Tetesi za soka Ulaya Jumanne 30.01.2024

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wanafikiria kuwasilisha ombi la dakika za mwisho mwisho kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Conor Gallagher(Times - Usajili unahitajika)

Mkataba wa Brentford kumsajili winga wa Norway Antonio Nusa mwenye umri wa miaka 18 kutoka Club Bruges unasuasua. (Sky Sports)

Miguel Almiron anatazamiwa kusalia Newcastle baada ya Al-Shabab ya Saudi Pro League kushindwa kufikia thamani ya pauni milioni 30 ya Magpies kwa winga huyo wa Paraguay mwenye umri wa miaka 29(Guardian)

Granada wamefufua uhamisho wao wa mkopo kwa winga wa Manchester United wa Uruguay Facundo Pellistri, 22. (Manchester Evening News)

Aston Villa wanafikiria kumuuza mhitimu wa chuo cha mafunzo ya soka Jacob Ramsey ili kutafuta fedha ili kutii kanuni za faida na uendelevu, huku Newcastle, Tottenham na Bayern Munich zikiwa na nia ya kumnunua kiungo huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 22 aliyekadiriwa kuwa na thamani ya £50m. (Athletic -Usajili unahitajika)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Al-Ittihad wako kwenye mazungumzo na klabu ya Saudi Pro League ambayo haijatajwa katika mji mkuu Riyadh kuhusu mpango wa kumuuza mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Karim Benzema, 36. (L'Equipe)

West Ham wako kwenye mazungumzo na Al-Ittihad kuhusu mpango wa kumnunua winga wa Ureno Jota mwenye umri wa miaka 24 baada ya mazungumzo na FC Nordsjaelland kuhusu kumnunua mshambuliaji wa Ghana Ibrahim Osman, 19, kukwama.(Standard)

Everton na Luton wana nia ya kumsajili mshambuliaji Muingereza Chuba Akpom mwenye umri wa miaka 28 kwa mkopo kutoka Ajax .(Teamtalk)

Mshambulizi wa Marekani Timothy Weah, 23, amekataa uhamisho wa mkopo kutoka Juventus kwenda Everton (Guardian)

Everton hawana shinikizo la kuwauza wachezaji kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho licha ya kutokuwa na uhakika kuhusu hli ya kifedha ya klabu hiyo (The i)

Lyon wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Nottingham Forest na Ubelgiji Orel Mangala, 25. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Southampton wanakaribia kuinasa saini ya winga wa Bournemouth na Wales David Brooks, 26, kwa mkopo. (HITC)

Leeds wametoa ofa ya mkopo kwa mlinzi wa Everton mwenye umri wa miaka 26 Ben Godfrey (Sun)

Sunderland wamekubali ada ya pauni milioni 2 na Leeds kwa beki wa pembeni wa Norway wa U-21 Leo Fuhr Hjelde. (Fabrizio Romano)

Burnley na Hull City wamewasilisha ofa rasmi kwa Millwall kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Romain Esse, 18. (Football Insider)

Chelsea itasikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Albania Armando Broja mwenye umri wa miaka 22 mwezi huu wakati wanajiandaa kuajiri mshambuliaji mpya mwenye jina kubwa msimu huu wa joto.. (90min)

Winga wa Brentford Muingereza Michael Olakigbe, 19, yuko kwenye majadiliano ya kina ili kujiunga na Peterborough United kwa mkopo kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho Alhamisi (Teamtalk)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah