Vita vya Ukraine: Mashujaa wa kivita wajiandaa kwa vita huko Luhansk

Chanzo cha picha, Reuters
Mashambulizi ya kijeshi ya Urusi huko mashariki mwa Ukraine tayari yanazidi.
Unaweza kuiona kwenye foleni ndefu za magari inayoendesha kuelekea magharibi kuelekea sehemu usalama ; unaweza kuhisi katika mitaa isiyo na watu unapoendesha gari kupitia miji na mitaa ya Donbas; na unaweza kuisikia kwa sauti inayoongezeka ya silaha za Kirusi.
Urusi inatuma tena vikosi vyake zaidi kutoka kaskazini hadi mashariki mwa Ukraine.
Kusudi likiwa ni kuzidisha vita katika eneo la Luhansk na Donetsk - sehemu ambazo tayari zilikuwa zimedhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga na kuunga mkono Urusi.
Urusi itachukua fursa ya njia fupi za usambazaji bidhaa - jambo ambalo limeonekana kuwa tatizo katika mashambulizi yake yaliyoshindwa dhidi ya mji mkuu wa Kiev.
Urusi na washirika wake sasa wanadhibiti karibu 90% ya Luhansk na zaidi ya nusu ya Donetsk - maeneo ya zamani ya viwanda ya Ukraine. Kuna moshi unaopanda katika eneo ambalo tayari limeharibiwa na uchimbaji madini na viwanda.
Vikosi vya Ukraine vimekuwa vikipigana vita hapa kwa muda wa miaka minane iliyopita.
Vitengo vyao ni pamoja na baadhi ya wanajeshi walio na vita kali zaidi nchini.
Maafisa wa Magharibi wanasema vikosi vya Ukraine vilivyoko Donbas ni vitengo vilivyo na mafunzo bora na vyenye vifaa.
Mashambulizi ya Urusi yanapoendelea kutoka kaskazini, mashariki na kusini kuna hatari ya kweli kwamba hivi karibuni wanaweza kuzingirwa.
Ukraine tayari imepoteza eneo hilo kwa Urusi. Lakini wanachimba kwa ajili ya mapambano. Tuliposafiri mashariki kuelekea mstari wa mbele tuliona nafasi mpya za ulinzi na mahandaki yakichimbwa.

Chanzo cha picha, Reuters
Sauti za silaha za kivita za Urusi ziliongezeka zaidi tulipokuwa tukielekea kwenye mstari wa mbele wa Ukraine huko Luhansk.
Mlio wa makombora uliingiliana na mlipuko wa mara kwa mara wa risasi ndogo za silaha. Tulikuwa ndani ya mita 500 kutoka kwa nafasi za Urusi.
Huu unaweza kuwa mzozo katika karne ya 21 lakini, wakati mwingine, huhisi kama kitu kutoka kwa Vita vya Kwanza vya dunia.
Wanajeshi wa Ukraine walitupeleka kwenye mitaro. Anatoly, askari mwenye umri wa miaka 52, alichungulia kupitia darubini kutoka kwenye maficho yake ili kutazama eneo ambalo wanajesho wa Urusi walipo. Aliniambia "Nawaona Warusi, wanafanana na mimi".
Lakini alikuwa tayari kupambana. Alisema "wakijaribu kuchukua nafasi yetu, nitawaua. Nisipowaua wataniua. Ni kanuni za vita."
Wanaume wengi tuliozungumza nao waliamini kwamba wamejiandaa vyema na ulinzi wao uliotayarishwa vizuri na utawapa nguvu dhidi ya wavamizi.
Andrej, mwanajeshi mwenye umri wa miaka 27, aliwekwa pamoja na mbwa wake kipenzi Lusifa. Aliniambia "tuna silaha nzuri na ngome nzuri na Urusi ikitushambulia hapa watapoteza".
Wanajeshi hao wanasema wamepewa silaha za magharibi kama vile makombora ya kuzuia vifaru. Walishukuru, lakini walitarajia zaidi.

Chanzo cha picha, Reuters
Andrej alisema kuwa Rais Putin ni "kama mwenda wazimu" lakini akaongeza kuwa wanajeshi wake wa Urusi waliokufa watakuwa mbolea nzuri ya udongo wao.
Wanajeshi walionekana kuchoka kutokana na mapigano, lakini wote walisema ari ilikuwa juu ya kupambana.
Roman, naibu kamanda, alikuwa ametumia miaka minne akisoma saikolojia katika Chuo Kikuu cha Lviv. Pamoja na kupigana aliweza kutoa msaada wa afya ya akili.
Lakini alisema "kawaida watu hawahitaji msaada wangu. Wana motisha nzuri ya kupigania familia zao, marafiki na nyumba zao, tofauti na Warusi", ambao aliwataja kama "zombies".

Wanajeshi wa Ukraine wote wanafahamu vyema kwamba Urusi inatuma tena vikosi zaidi maeneo ya mashariki. Wanajua kuwa hali itakuwa mbaya zaidi.
Lakini Roman anaamini kwamba vikosi vya Ukraine vina busara zaidi. Alisema kwamba mafundisho ya kijeshi ya Urusi hayajaendelea tangu Vita vya Pili vya Dunia, kwa kutegemea mizinga.
Mizinga hiyo ya Kirusi ingawa tayari inalazimisha makumi ya maelfu ya watu kuondoka makwao.

Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Majeshi ya Urusi yaondolewa kabisa kutoka Kyiv-Pentagon
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine













