Vita vya Ukraine: Putin anataka nini ili kumaliza vita?

Chanzo cha picha, EPA
Wajumbe wa Urusi na Ukraine wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana mjini Istanbul kujadili vita kati ya nchi hizo mbili.
Pande hizo mbili zimewahi kutamka hadharani baadhi ya misimamo yao. Ukraine ilisema itazingatia matakwa ya Moscow ya kutoegemea upande wowote, lakini haitaafikiana juu ya eneo lake. Urusi ilitoa wito wa kuwaondoa "wanazi" na "wanajeshi wa kigeni" nje ya Ukraine, bila kufafanua maana halisi ya madai hayo
Wiki tano za mashambulio ya mabomu, maelfu ya vifo katika miji iliyobomolewa na zaidi ya watu milioni 10 wakiwa wametawanyika ndani na nje ya Ukraine, Putin anataka nini ili kumaliza vita?
Ukraine 'kutoegemea upande wowote'
Urusi kwa muda mrefu imetaka Ukraine "kutoegemea upande wowote" juu ya suala la upanuzi wa muungano wa kijeshi wa Magharibi, Nato.
Kwa hakika, baadhi ya wachambuzi wanaamini kuwa hii ndiyo ilikuwa "sababu kuu" ya uvamizi wa Urusi, anasema Pascal Lottaz, mtaalamu wa kutoegemea upande wowote katika Taasisi ya Waseda ya Utafiti wa Juu nchini Japan.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine

Chanzo cha picha, EPA
Urusi pengine itahitaji kwamba Ukraine ijumuishe katika katiba yake ahadi ya kutojiunga na Nato na kutia saini makubaliano ya nchi mbili na Urusi ili kuimarisha msimamo huu, Lottaz anasema.
Rais wa Ukrain, Volodymyr Zelensky, amedokeza kuwa yuko tayari kujadili kutoegemea upande wowote, ingawa haijulikani wazi ni hili linamaanisha nini katika suala la uwezekano wa Ukraine kujiunga na EU katika siku zijazo.
Uanachama wa EU utakuja na uhakikisho wa usalama wa pande zote, na haijulikani wazi jinsi Ukraine na Urusi zinaweza kutazama hali hiyo.
'Kuondoa silaha'
Hii inaweza kuthibitisha hatua nyingine ya kushikamana kama Ukraine isiyo na kijeshi, bila NATO au washirika wa Ulaya, itakuwa katika hatari ya uvamizi mwingine wa Urusi.
Lakini Lottaz anamini cha msingi zaidi kuhusu takwa hili sio kuvunja Ukraine, bali ni kuhakikisha haina mashambulizi au silaha za nyuklia ambazo zinaweza kutishia usalama wa Urusi - hasa silaha za Nato.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfano mmoja unaowezekana uliwekwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, wakati Marekani ilikubali kwamba Japan inapaswa kuunda upya jeshi lake la kujilinda, na jeshi limepigwa marufuku kikatiba kutumia vita kama njia ya kusuluhisha mizozo ya kimataifa.
Kufikia hilo Japan na Marekani zilitia saini mkataba wa pande mbili na Japan ikategeme Marekani kwa usalama wake.
Lottaz anaamini matakwa ya Urusi yatafikia hapo, kulenga kuondoa uwezo wowote wa kutia hofu ambao Ukraine inaweza kuwa nao.
'Kuondoa Wanazi'
Putin ameishutumu serikali ya Ukraine kwa kudhibitiwa na makundi ya Wanazi mamboleo, madai mbayo yanapingwa na waangalizi wa kisiasa.
Lakini kwa kutoa shutuma hizo, Vladimir Putin anaibua kumbukumbu zenye nguvu za shambulio la Hitler dhidi ya Muungano wa Kisovieti, na analinganisha na mashambulizi dhidi ya waasi wa Urusi mashariki mwa Ukraine.
Shutuma dhidi ya Wanazi yanaweza kusababisha kosa la kibinafsi kwa Rais Zelensky, ambaye anatoka katika familia ya Kiyahudi ambayo babu na babu walipigana na Wanazi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lottaz anasema "kuondoa Wanazi" huenda la "Kirusi la kubadili utawala", lakini wazo hilo liko mbali kwani vikosi vya Ukraine vimejibu mashambulizi na kuzuia wanajeshi wa Urusi kusonga mbele.
Ili kujiondolea fedheha, Urusi huenda ikakubali Zelensky kusalia madarakani lakini isisitize kuondolewa kwa kikosi cha Azov, kundi la wapiganaji wa mrengo wa kulia ambalo limekuwa kiungo muhimu katika upinzani, wa walinzi wa kitaifa.
Lottaz anasema hii huenda"ikawa hatua ndogo" lakini "huenda ikaathiri jeshi la ulinzi kwa kiwango fulani".
Donetsk na Luhansk
Baada ya kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine, Urusi ilitangaza mkakati mpya wa kijeshi unaojumuisha "kwa kasi" kupunguza mashambulizi dhidi ya Kyiv.
Badala yake, mwelekeo ungerejea mashariki mwa Ukraine katika maeneo yanayozungumza Kirusi, ambayo yanadhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi.
Moscow inaweza kudai kwamba Ukraine iachane na maeneo yanayotaka kujitenga ndani ya Donetsk na Luhansk, kwenye bonde la mto Donbas, ambalo liko katikati ya mgogoro.

Chanzo cha picha, Getty Images
Crimea
Pia kuna uwezekano wa Urusi kudai kwamba Ukraine ikubali rasmi unyakuzi wake wa Rasi ya Crimea.
Rasi hiyo ilivamiwa na kuchukuliwa na Urusi mnamo 2014 na inatawaliwa na Moscow.
Ikiwa Kyiv itakubaliia na takwa hili, itakuwa hasara kubwa ya kupoteza eneo kwa Ukraine.
Mkataba wa kabla ya Putin wa Urusi na Ukraine mnamo 1997 ulitambua Crimea kama sehemu ya Ukraine.
Lugha ya Kirusi
Kremlin pia inaweza kudai uhakikisho kwamba matumizi ya lugha ya Kirusi yatalindwa nchini Ukraine.
Tangu mzozo na Moscow ulipozidi mwaka 2014, Urusi imekuwa sehemu ya mzozo wa kisiasa nchini Ukraine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 2017 mahakama za Ukraine zilipiga marufuku lugha ya Kirusi kufundishwa shuleni na kutoka wakati huokumekuwa na miswada ya kudhibiti utumizi wa lugha ya Kirusi nchini humo.
Kuanzia Januari,magazeti yote ya kitaifa na majarida nchini Ukraine yaliamuriwa yachapishwe kwa Kiukreni.
Kwa vyovyote vile matakwa ya Putin kuhusu masuala hayo yote, wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema makubaliano ya amani kati ya Ukraine na Urusi yanaweza kuchukua muda mrefu kujadiliwa.
Lakini nchi zote mbili zina sababu za kufikia amani.
Kwa Ukraine, inahusu kuzuia vifo zaidi vya raia, upotezaji wa nyenzo kutokana na uharibifu wa miji yake, na kusimamisha mtiririko wa wakimbizi kwenda nchi jirani.
Kwa Urusi, ni juu ya kupunguza matokeo ya majeruhi makubwa kati ya wanajeshi wake yenyewe na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za Magharibi - ambavyo tayari vinaathiri Warusi wa kawaida.















