Picha za wiki barani Afrika 6 - 13 Desemba 2019

Swahili fashion

Tamasha la mitindo na mavazi maarufu kama Swahili Fashion Week limefanyika wiki hii nchini Tanzania, Jukwaa hili la maonyesho ya mavazi Afrika Mashariki na kati linalotoa fursa kwa wabunifu wa mavazi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili na kwingineko Afrika kuonesha vipaji vyao na kupanua wigo wao wa masoko.

Maonesho haya ya 12 yamekutanisha wabunifu 34 wa Afrika Mashariki na kwingineko ulimwenguni.

Wabunifu wa mavazi walioshiriki kuonesha mitindo yao kutoka Afrika mashariki, Kati na ulimwenguni kwa mwaka huu , ni pamoja na Afrikawala, Mary Angel na Marta Zampolini kutoka Italia.

Mwanzilishi wa Tamasha hili Mustapha Hasanali anasema kuwa Watanzania na Waafrika wanapaswa sasa kutumia bidhaa za nyumbani.

Mwanzilishi wa Tamasha hili Mustapha Hasanali
Maelezo ya picha, Mwanzilishi wa Tamasha hili Mustapha Hasanali

"Tunahamasisha umma wa Watanzania kupenda kuvaa mavazi yaliyobuniwa na wabunifu wa hapa Tanzania (Made in Tanzania). Kwa kufanya hivyo tunakuza vipaji vyao na kuwafanya siku moja kutambulika kama wabunifu wakubwa Ulimwenguni. Upendo unaanzia nyumbani na ndiyo dhumuni la kufanya haya, ni kukuza tasnia hii ya ubunifu" anasema Hassanali.

Mavazi ya aina mbalimbali yameoneshwa katika jukwaa hili, mavazi ya rasmi, ya kawaida na ya sherehe mbalimbali kama Harusi.

mavazi ya Afrika
Mavazi ya Afrika-swahili fashion week

Mavazi aina ya kitenge yalionekana kutawala kwa kutumia na wabunifu wengi wa mavazi.

Raia wa Afrika Kusini ,Zozibini Tunzi kutununikiwa taji la Miss Universe mjini Atlanta, US.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raia wa Afrika Kusini ,Zozibini Tunzi kutununikiwa taji la Miss Universe mjini Atlanta, US.
Mwanafunzi wa kucheza mziki mjini Nairobi (ballet dancer)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwanafunzi wa kucheza mziki mjini Nairobi (ballet dancer)
Ruth Akulu (right) and colleagues cut a cake together.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Sherehe za mahafali ya Chuo kikuu nchini Uganda mjini, Kampala.
A man uses coloured paint and chalk on a dark canvas.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mchoraji wa Eritrea Nebay Abraha akiwa nchini Ethiopia, Addis Ababa.
A woman holding an umbrella walks past a mural as heavy showers continue in Johannesburg, South Africa, 09 December 2019. Heavy rainfalls are predicted for the upcoming days for most of the inner country after a low pressure zone brought heavy rains last week.

Chanzo cha picha, EPA

A lion cub bares its teeth at the camera from behind the bars on its cage.

Chanzo cha picha, Barcroft Media

Picha za Getty Images, EPA, Barcroft Media, AFP, Reuters na BBC.