Picha za wiki barani Afrika 6 - 13 Desemba 2019

Tamasha la mitindo na mavazi maarufu kama Swahili Fashion Week limefanyika wiki hii nchini Tanzania, Jukwaa hili la maonyesho ya mavazi Afrika Mashariki na kati linalotoa fursa kwa wabunifu wa mavazi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili na kwingineko Afrika kuonesha vipaji vyao na kupanua wigo wao wa masoko.

Maonesho haya ya 12 yamekutanisha wabunifu 34 wa Afrika Mashariki na kwingineko ulimwenguni.

Wabunifu wa mavazi walioshiriki kuonesha mitindo yao kutoka Afrika mashariki, Kati na ulimwenguni kwa mwaka huu , ni pamoja na Afrikawala, Mary Angel na Marta Zampolini kutoka Italia.

Mwanzilishi wa Tamasha hili Mustapha Hasanali anasema kuwa Watanzania na Waafrika wanapaswa sasa kutumia bidhaa za nyumbani.

"Tunahamasisha umma wa Watanzania kupenda kuvaa mavazi yaliyobuniwa na wabunifu wa hapa Tanzania (Made in Tanzania). Kwa kufanya hivyo tunakuza vipaji vyao na kuwafanya siku moja kutambulika kama wabunifu wakubwa Ulimwenguni. Upendo unaanzia nyumbani na ndiyo dhumuni la kufanya haya, ni kukuza tasnia hii ya ubunifu" anasema Hassanali.

Mavazi ya aina mbalimbali yameoneshwa katika jukwaa hili, mavazi ya rasmi, ya kawaida na ya sherehe mbalimbali kama Harusi.

Mavazi aina ya kitenge yalionekana kutawala kwa kutumia na wabunifu wengi wa mavazi.

Picha za Getty Images, EPA, Barcroft Media, AFP, Reuters na BBC.