Ramadhan 2023: Baadhi ya matukio muhimu katika historia ya Uislamu katika mwezi wa Ramadhan

Yakin Badr

Chanzo cha picha, Haramain Sharifain

Maelezo ya picha, Maswahaba 14 wa Mtume waliuawa katika vita vya Badr

Kwa Waislamu kote duniani, Ramadhani ni mwezi mtukufu na hatua muhimu katika historia ya Uislamu.

Ramadhani ni mwezi mtukufu ambao Waislamu hutumia mwezi wa Ibada wakiwa wamefunga, moja ya nguzo za Uislamu.

Mbali na kuwa mwezi wa Ibada, matukio mengi ya kihistoria yalitokea wakati wa Ramadhani, ambao ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu.

Sheikh Muhammad Mashhud mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu aliambia BBC baadhi ya matukio muhimu zaidi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ingawa kuna matukio mengi ya kihistoria yaliyotokea wakati wa mwezi huu mtukufu.

Kuteremshwa kwa Quran

Tukio muhimu zaidi lililotokea katika mwezi wa Ramadhani.

Tukio hilo ambalo ni muhimu zaidi kwa Waislamu katika mwezi huo, lilikuwa ni kuteremshwa kwa Quran Tukufu kwa Mtume Mohammad (SAS).

Mwenyezi Mungu aliteremsha ufunuo wa Quraan kupitia Malaika wake Jibril.

Uteremsho wa Quran ulifanyikakatika moja ya usiku unaoaminiwa kuwa mtukufu katika mwezi wa Ramadhani.

Usiku huo katika mwezi wa Ramadhani una thamani ya zaidi ya miezi elfu moja.

Vita vya Badr

Vita vya Badr vilitokea tarehe 17 Ramadhani, miaka miwili baada ya Mtume kuhama kutoka Makka kwenda Madina.

Waislamu walishinda vita, ingawa maadui walikuwa wengi zaidi yao..

Maswahaba kumi na wanne wa Mtume waliuawa kishahidi siku hiyo.

Ni wakati wa vita hivi ambapo Abu Jahl, mmoja wa maadui wakubwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliuawa.

Kutekwa kwa Makkah

Miaka minane baada ya Hijra (kuhama kwa Mtume kutoka Makka kwenda Madina) ya tarehe 18 Ramadhani Mtume aliingia Makkah pamoja na jeshi lake kuuteka mji wa Makka ambao nao ulipatikana kwa amani, ingawa hakuna mapigano yaliyofanyika.

Kutekwa kwa mji huo kulikomesha ibada ya masanamu huko Makka, mojawapo ya vipindi muhimu sana katika historia ya Uislamu.

Watu wengi walisilimu baada ya ushindi huo.

Kifo cha Nana Khadija RA

Hili ni kaburi la Nana Khadija RA, mke wa kwanza wa Mtume Mohammad (SAS), kando ya kaburi la mtoto wake mkubwa Kasim RA.

Chanzo cha picha, Haramain Sharifain

Maelezo ya picha, Hili ni kaburi la Nana Khadija RA, mke wa kwanza wa Mtume Mohammad (SAS), kando ya kaburi la mtoto wake mkubwa Kasim RA.

Nana Khadija RAalifariki tarehe 10 mwezi wa Ramadani.

Alikuwa mke wa kwanza wa Mtume Mohammad, na wa kwanza kukubali Uislamu.

Bi Khadija alikuwa mfuasi mkubwa wa msingi wa Uislamu..

Kifo cha Nana Aisha RA

Mnamo mwaka 58 AH, Nana Aisha RA, mke wa Mtume alifarik dunia.

Bi Aisha alifariki tarehe 17 mwezi wa Ramadan.

Alikuwa kiungo muhimu katika Uislamu. Baadhi ya wanazuoni wanasema robo ya mafundisho ya Uislamu yamesimuliwa na Nana 'Aisha RA.

Kifo cha Hazrat Ali

Mnamo tarehe 19 mwezi wa Ramadhani, Ali ibn Abi Talib (RA) aliuawa kwa kuchomwa kisu.

Alifariki tarehe 21 Ramadhani miaka 40 baada ya Hijrah kutokana na majeraha aliyoyapata katika shambulio hilo.

Ali Radiyallahu Anhu alikuwa wa nne wa Makhalifa wa Khulafur Rashidun wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Vita vya Tabuk

Vita vya Tabuk ni moja ya matukio muhimu katika historia ya Uislam wakti wa mwezi wa Ramadhani.

Mtume Mohammad alimtuma Yemen, Ali Radiyallahu Anhu kama kiongozi wa jeshi.

Watu wengi walijiunga na dini ya Kiislamu na kuongeza idadi ya Waislamu.