Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 08.08.2021: Kane, Messi, Silva, Lukaku, Coutinho, Camavinga, Mbappe, Martial
Tottenham wanatafakari uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, ikiwa Manchester City watalipa pauni milioni 120 na zaidi na marupurupu ya ziada ya pauni milioni 20. (Star Sunday)
City wanategemea uwezo wa Kane kumshawishi mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy kumruhusu kujiunga na mabingwa hao ligi ya Primia. (Sunday Mirror)
Lionel Messi na Paris St-Germain wamekubaliana mkataba wa miaka miwili, huku mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 34 akitarajiwa kumaliza rasmi uhusiano wake wa miaka 21 na Barcelona kwa "heshima"leo Jumapili katika mazungumzo na waandishi wa habari katika uwanja wa Nou Camp. (Le Parisien - in French)
Ikiwa Messi atahamia mji mkuu wa Ufaransa, atapokea mshahara wa euro milioni 40 kwa mwaka (karibu pauni milioni 34). (L'Equipe - in French)
Uwezekano wa Messi kuhamia uwanja wa Parc des Princes utaimarisha matumaini ya Manchester United kumsajili kiungo wa kati wa Rennes Mfaransa Eduardo Camavinga, 18, ambaye amehusishwa pakubwa na uhamisho wa kwenda PSG. (Star Sunday)
Sergio Aguero, 33, atasalia Barcelona, licha ya tetesi kwamba anataka kuondoka baada ya taarifa kuibuka kwamba rafiki yake na mchezaji mwenza wa Argentina Leonel Messi anaondoka klabu hiyo. (Marca - in Spanish)
Arsenal wanatafakari uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Portugal Bernardo Silva, ambaye awali aliwaambia mabingwa hao wa Ligi ya Primia kwamba anataka kuondoka klabu hiyo. Gunners wanamchukulia Silva kama mbadala wa kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison, 24. (Sunday Mirror)
Silva anajiandaa kufanya mazungumzo na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola na anatarajiwa kushinikiza uhamisho wake kwenda Barcelona. (Sunday Sun)
City wako tayari kumpatia Silva ofa yoyote kwa ajili ya Harry Kane lakini piawako tayari kumkosa kabisha nahodha huyo wa England bada ya kufikia bei ya Tottenham ya paundi milioni 150 . (Mail on Sunday)
Mabingwa wa Italia Inter Milan wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku kwenda Chelsea na wanataka wachezaji wawili zaidi kabla ya kufanya hivyo. Wachezaji hao npamoja wa mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, mshambuliaji wa Atalanta na Colombia Duvan Zapata, 30, na mshambuliaji wa Roma na Bosnian Edin Dzeko 35. (Sky Sport Italia - kwa Kitaliano)
Arsenal na West Ham pia wanamtaka Abraham lakini Atalanta watawasilisha dau la kumnunua mshambuliaji huyo wa Chelsea ikiwa Inter Milan itamuulizia Zapata kuchukua nafasi ya Lukaku. (Fabrizio Romano)
Lukaku atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu Jumapili nchini Ubelgiji kabla ya kukamilisha uhamisho wake na anatarajiwa kuwasili Londan siku ya Jumatatu. (Athletic - subscription required)
Tottenham wamehusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, lakini uhamisho huo utategemea uamuzi wa Spurs kumuuza mshambuliaji wa England Harry Kane. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barca tayari wammtoa Coutinho kwa Everton, lakini klabu hiyo ya Mersey inaweza kukataa nafasi ya kumsajili mchezaji wa zamani wa Liverpool. (Liverpool Echo)
Burnley wanajitahidi kutoa ofa kwa winga wa Uingereza RB Leipzig mwenye umri wa miaka 23, Ademola Lookman, hivyo anaweza kuzingatia kujaribu kumsajili beki wa Ivory Coast Maxwel Cornet, 24, kutoka Lyon
Paris St-Germain mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, nyongeza ya mshahara ili kumshawishi asaini mkataba mpya na kilabu hicho.
Klabu ya Granada ya Uhispania inakaribia kumsajili kipa wa Argentina Sergio Romero, ambaye hana klabu baada ya kuondoka Manchester United mkataba wake ulipomalizika msimu huu wa joto. (Ideal - in Spanish)