Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 07.08.2021:Messi, Lukaku, Romero, Odegaard, De Ligt, Milenkovic, Ward-Prowse

Paris St-Germain wanatarajiwa kutoa ofa ya mkataba wa miaka miwili kwa Lionel Messi katika mkutano uliopangwa kati ya baba wa mchezaji huyo na uongozi wa PSG Jumamosi. (Telegraph)

Baba wa Messi aliwasiliana na PSG kuulizia kama klabu hiyo ya ufaransa ina nafasi ya kumsajili mchezaji huyo mwa miaka 34. (Marca)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ameomba ''mkutano wa dharura'' na wawakilishi wa Messi baada ya kutangazwa kuwa hatasalia Barcelona. (AS in Spanish)

Kocha wa PSG Mauricio Pochettino amethibitisha kuwa mawasiliano yamefanyika kuhusu uhamisho huu muhimu, na kama Messi ataweka wino na timu hiyo ya Ligue 1, moja kwa moja Kylian Mbappe,22, atasaini mkataba mpya hatua ambayo itafanya klabu hiyo kuachana na mbio za kumsajili Paul Pogba, 28, kutoka Machester United. (ESPN)

Messi mwenyewe anaelezwa kuwa chaguo lake la kwanza ni kuona anaungana tena na kocha Pep Guardiola Manchester City. (Mail)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar,29, amempa ofa ya shati yake namba 10 ya PSG likiwa jaribio la kumshawishi kuhamia kwenye klabu hiyo. (RMC Sport)

Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, aliyejiunga na Barcelona mwezi Mei baada ya kuondoka Manchester City, anaelezwa anataka kuondoka kwenye klabu hiyo ya Catalan baada ya kutangazwa kuwa rafiki yake wa karibu hatasalia Nou Camp. (Beteve-in Catalan)

Chelsea wameendelea kuwa na hakika wa kuingia makubaliano na Inter Milan mwishoni mwa juma kwa ajili ya kumsajili tena Romelu Lukaku, huku kocha Thomas Tuchel akitarajia kumaliza mchakato wa uhamisho kabla ya kuanza kwa msimu mpya. (Standard)

Lukaku ameridhia masharti binafsi na Chelsea na anasubiri vilabu kumaliza mchakato wa uhamisho. (football.london)

Barcelona wamekubaliana na kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 23, lakini hawajakubaliana ada na klabu yake ya Lille. (Le10 Sport)

West Ham United wamesalia kwenye mazungumzo na Fiorentina kuhuhu dili la pauni milioni 14 kwa ajili ya mlinzi Nikola Milenkovic,23, lakini watakabiliwa na ushindani kutoka Juventus. (Mail)

Klabu hiyo ya London pia inamtaka mlinzi wa Marseille Duje Caleta-Car,24, baada ya mlinzi wa kati kukataa ofa msimu wa joto uliopita( L'Equipe)

Mshambuliaji wa Kimarekani Josh Sargent,21, yuko karibu kumaliza hatua za uhamisho kuelekea Norwich City akitokea Werder Bremen. (Goal)

Real Madrid wamezuia uhamisho wa kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard,22, kwenda Arsenal baada ya Toni Kroos kupata jeraha. (AS,via Team Talk)

Southampton wamekataa dau la pauni milioni 25 kutoka kwa Aston Villa kwa ajili ya James Ward-Prowse,26, na hawana nia ya kumuuza kiungo huyo wa kati msimu huu.( Football Insider)

Chelsea wanamtaka mlinzi wa Juventus Matthijs de Ligt,21, wanaweza kutoa ofay a pauni milioni 50 na mshambuliaji Timo Werner,25. Hatahivyo Juve wanamtaka zaidi kiungo wa kati Muitaliano Jorginho,29, sambamba na kitita cahfedha. (Calciomercatoweb)

West Ham wametangaza dau la pauni milioni 15 kwa ajili ya mlinzi anayekipiga Rennes Nayef Aguerd,25, klabu hiyo ya Ufaransa ikitarajiwa kukataa ofa hiyo. (Football Insider)