Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanawake wanavyorekodiwa kwa siri kwa ajili ya maudhui kuchapishwa TikTok
Diara alikuwa akipata chakula cha mchana wakati ya mapumziko mafupi ya adhuhuri kazini Jijini London ambapo anafanya kazi. Akiwa anaendelea kula, mwanamume mrefu alimkaribia na kumueleza kwamba ; 'Ninakuapia kwamba nywele za rangi nyekundu ni ishara kwamba umevunjwa moyo na mpenzi.'
Mwanamume huyo aliendeleza mazungumzo na Diara kwa muda kwa kuwa wawili hao waliingia kwenye gari moja la huduma ya teksi. Ni hapo ambapo mwanamume huyo alimuomba binti huyo namba yake ya simu.
Jambo ambalo Diara hakuwa amelifahamu ni kwamba mwanamume huyo alikuea an amrekodi kisiri kwa kutumia kamera zilizokuwa kwa miwani aliyovalia. Bila ya kuzikagua kwa kina, huewzi kufahamu kwamba miwano hizo zina kamera na uwezo wa kurekodi picha za video.
Picha hizo za video zilichapishwa kwa mtandao wa TikTok, ambapo zilitazamwa takriban mara milioni 1.3. 'Nilitamani kulia,'Diara aliiambia BBC.
Mwanamume aliyemrekodi, imebainika kwamba, amekuwa akichapisha makumi ya picha za video kama hiyo kwenye mtandao wa TikTok, na kuwapa wanaume wenzake mbinu za kumtongoza mwanamke.
Diara pia aligundua kwamba namba yake ya simu ilikuwa imeweka hadharani katika video hiyo. Na ni hapo ambapo alianza kupokea jumbe nyingi na hata kupigiwa simu.
Mwanamke mwingine, Kim , alirekodiwa katika msimu w ajoto kali mwaka jana, akiwa kwenye ufuo wa bahari mjini West Sussex. Mwanamume mwingine ambaye pia alikuwa amevalia miwani yenye kamera alimrekodi walipokuwa wakizungumza na hata mwanamume huyo akampongeza kwa vazi la aina ya 'bikini ' ambalo alikuwa amevalia.
Alitaka kujuwa anakoishi binti huyo na hata kujaribu kuwasiliana yane kwenye mtandao wa kijami wa Instagram. Kim mwenye umri wa miaka 56, hakuw ana ufahamu kwamba alikuw aan arekodiwa na walipoendelea na mazungumzo yao, walibadilishana taarifa muhimu kuhusu familia yake na anakofanya kazi.
Baadaye, mwanamume huyo alichapisha video mbili mitandaoni, akidai kwmaba anawapa wanaume mbinu za kuwatongoza wanawake na mahusiano ya kimapenzi, Video hizi zilikuwa na mvuto mkubw amitandaoni ambapo watu zaidi ya milioni 6.9 walizitazama kwenye mtandao wa TikTok huku pia video hizo zikiwa na 'Likes' zaidi ya laki moja kwenye mtandao wa kijami wa Instagram.
BBC imetazama mamia ya video fupi kama hizo zilizochapishwa katika mtandao wa TikTok na Instagram ambazo zimechapishwa na makumi ya wanaume ambao ni waandaji maudhui mitandaoni.
'Mainfluensa' hao wanadai kuwapa wanaume wenzao mawaidha ya jinsi ya mutongoza mwanamke, kuanzisha mahusiano na katika visa kadhaa video hizo zimeonekana kurekodia pasi na mwanamke husika kujuwa anarekodiwa au kutoa idhini yake. Wengi wanasemekana kutumia miwani aina ya SMART META GLASSES.
Waandaji wa aina hii wa maudhui mitandaoni, akiwemo mwanamume aliyechapisha video za Kim, wanapata kipato chao kw akutoa mawaidha kwa wateja wao.
Nilianza kufuatilia suala hili wakati nilipogundua kwamba kuna video yangu nikiwa katika mazungumzo na mwanamume na mabayo ilirekodiwa kisiri yenye anwani ,' Kumtongoza binti mwenye nywele za njano katika enel la Leicester Square ["Picking up Cute Blonde in Leicester Square"} Nilipozidi kuendeleza uchunguzi, niligundua kwamba sikuwa peke yangu.
Diana na Kim ni miongoni mwa wanawake saba kutoka Uingereza, Marekani na Australia ambao wameiambia BBC kwamba walirekodiwa bila kujuwa.. Wote walisema kwamba walihisi kudhulumiwa na kuwachwa katika hali ya kuwa na msongo wa mawazo baada ya kupata taarifa kwamba video zao zilikuwa zimechapiswhwa mitandaoni.
Nchini Uingereza, hakuna sheria kwa sasa ambayo inaharamisha mtu kurekodiwa hadharani bila ya ayeye kutoa idhini yake, amesema wakili wa masuala ya kibinafsi Jamie Hurrworth – lakini 'kuwa katika Eneo la hadharani' hakumaanishi kwamba 'ni sawa kutenda utakavyo' au kurekodiwa na kisha video hizo zichapishwe mitandaoni.'
Baada ya kuripoti video hizi kwa mara ya kwanza kwa usimamizi wa TikTok, Dilara aliambiw ana kampuni hiyo kwamba hakuna makosa yoyote yaliyofanyikabaada ya uchunguzi kufanyika. Hata hivyo, baada ya BBC kuwasiliana nao, wasimamizi wa TikTok walisema kwamba video hizo ziliondolewa mitandaoni na kampuni hiyo baadaye na katiak taarifa walielezea zaidi kwamba ,' Tutaondoa video ambazo zinekiuka kanuni za kijami na zinazohusu dhuluma na watu kuteswa.'
Kim alimuuliza mwanamume ambaye alirekodi vídeo yake , kuondoa taarifa kuhusu familia na kazi anayoifanya, ila hakufanya hivyo.
Kampuni zinazotengeneza miwani yenye kamera zimesemekana kuangazia 'faida juu ya usalama wa wanawake, hali yao ya maisha na haja ya kuweka hatua za kuwalinda ,' alisema Rebecca Hitchen kutoka shirikal la End Violence Against Women Coalition.
Hata hivyo, mashirika ya kutoa misaada na wataalamu wanaonya kwamba video za aina hiyo huenda zikakosa kuorodheshwa katika viwango vinavyotambulika kisheria kama makosa ya jinai katika sheria ya Uingereza ya usalama mitandaoni.
Dilara aliitazama video yake siku ya pili, wakati ambapo rafiki yake alimtumia : 'Moyo wako unashtuka sana na wala huwezi kufanya lolote.'
Kim na Dirala wanasema kwamba kurekodiwa katika hali hii kulihisi kama uvunjaji wa haki zao za kibinafsi na wanaamini kwamba hatua ni sharti ichukuliwe.
'Hakuna anayehaki ya kumrekodi mwengine na kumdhulumu kiasia hiki na kumfanya kuwa kama chombo cha ngono kwa ajili ya kutengeneza hela bila ya anayerekodiwa kutoa idhini,' alisema Kim.
BBC ilijaribu kuwasiliana na wanaume hao wawili waliowarekodi Kim na Dirala, lakini hatukupata majibu.WAwili hao walitumia miwani aina ya RAY-BAN iliyoundwa kwa akili unde inayomilikiw ana kampuni ya META. Mwanamume aliyemtongoza Dirala alivalia miwani yenye vioo ambavyo unaweza kuyaona macho yake naye mwanamue aliyemzungumzia Kim alikuwa amevalia miwani iliyokuwa na rangi ya kuzuia miale ya jua kubana macho almaarufu SUN GLASSES.
Aina hii ya miwani ina pata mvuto mkubw ana umaarufu. Kati ya Oktoba 2023 na Februari 2025, takriban miwani milioni 2 ziliuzwa kwa wateja kwa mujibu wa kampuni ya kutengeneza miwani ya ESSILOR LUXOTTICA.
Kampuni ya META imeiambia BBC kwamba miwani yake inamwanga wa LED ambao huwaka wakati ambapo mtu anarekodi video au picha.
Aidha kampuni hiyo ya Teknolojia imeweka wazi kwamba imehakikisha kuwa kuna uwazi na kuwa mwanga huo ni ishara tosha kwa wote kwamba miwani inarekodi, na zipo na teknolojia ya kumzuia mtu kuondoa uwezo wa miwano hayo kuwaka wakati wa kurekodi .
Lakini BBC imeona video kadhaa zilizochapishwa mitandaoni zinazoonyesha jinsi ya kuzima mwanga huo au kuondolewa kabisa.
Kim na Dirala au wanaweake wengine wote waliozungumza na BBC wanasema hawakuona mwanga wowote kwenye miwani ambayo waliowarekodi walikuwa wamevalia.
'Ikiwa video zilirekodiwa kwa kutumia miwani yenye kutumia teknolojia ya akili unde ya META , basi kwa kawaida ilitakiwa mwanga huo kuwaaka kama ishara kwamba miwani zilikuw azinarekodi,' alisema wakili wa masuala ya kibinafsi Jamie Hurworth, 'Hili linazua maswali kuhusu ikiwa kuna haja ya kuweka vizingiti vikali kudhibiti teknolojia hiyo.'
Waziri anayesimamia masuala ya Ulinzi wana usalama wa wanawake na wasihana dhidi ya dhuluma – Jess Phillips amesema katika taarifa ya kwamba : 'Kuwarekodi wanawake na wasichana kisiri ni uchafu na hatutakubali mtu yeyote kunufaika na hilo.'
Wanawake kusumbuliwa na simu nyingi
Kwa sababu nambari yake ya simu ilikuwa imechapishwa hadharani kwenye mitandao ya kijami katika video yake, Dirala anasema kwamba alisumbuliwa kwa kupigiwa simu nyingi kwa muda mrefu wa wiki kadhaa, wakati mwingi simu yake ikiwa haiachi kuita, nazo jumbe fupi za SMS zikiingia kwenye simu yake kila dakika na wakati mwingine usiku wa manane.
Wakati mmoja, anasema alipokea simu na mwanamume aliyekuwa upande wa pili wa laini akamueleza: 'Unafahamu jinsi ulivyo mpumbavu?Je unalijutia hili? Unafahamu jinsi ulionekana kama mtu ambaye ni mwepesi kushawishiwa kimapenzi?'
Wanaume wamefika kazini kwake kwa kutumia video iliyochapishwa mitandaoni au wanawasiliana naye kwenye ujumbe za ndani Yaani DM wakitaka kujua taarifa zaidi kumhusu , anasema.
Mbali na kuchapisha video hizo kwenye mitandao ya TikTok kisiri, mwanamume aliyemrekodi anaakaunti katika mtandao wa DISCORD yenye ufuasi mkubwa – ambayo ni APP ya kuwasiliana na kutumiana ujumbe yenye umaarufu miongoni mwa wanaocheza michezo ya mitandaoni almaarufu GAMERS. NI hapo ambapo amechapisha au KUPOSTI maudhui yake ya mawaidha kwa wateja na pia kuweka video nyinginezo.
Baada ya TikTok kuondoa video ya Dirala, iliambia BBC kwamba ; 'Tumeondoa video hiyo kw akukiuka kanuni zetu za kijami kuhusiana dhuluma za mitandaoni na tumehakikisha hazitaonekana kwa kuzifanya kuwa haziwezekani kuonekana .'
Kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii imeiambia BBC kwamba haikubali maudhui ya mitandaoni kujumuisha taarifa za kibinafsi ambazo huenda zikavuja na kusababisha wahusika kuwa katika hatari ya kufuatwa na watu wenye mipango ya kuwaumiza , kuwalghai au kuwaumiza wahusika ,' wakisema kwamba kuna Eneo katika tovuti yao ambapo masuala ya ukiukaji wa haki za kibinfsi zinaweza kuripotiwa.
'Mama yako amekuwa maarufu mtandaoni'
Kima anasema kwamba alifahamu kuhusu video zake kusambaa mitandaoni kupitia mwana wake wa kiume ambaye alimpigia simu saa kumi na moja asubuhi. Alikuwa amepata ujumbe kutoka kwa marafiki zake kadhaa waliosema kwamba ,'Mama yako amekuwaa maarufu mitandaoni - Yaani video yake imekwenda Viral'
Baada ya kurekodiwa katika ufuko wa bahari huko West Wittering katika msimu wa joto kali mwaka jana , Kim anasema amepokea maeflu ya jumbe za SMS kutoka kwa wanaume. Baadhi ya jumbe hizo zilikuwa zenye maudhui ya kingono: 'Watu wanasema , 'Sema bei yako ili tutazame uchi wako' au 'Una akaunti ya OmlyFansa?'
Miezi sita baadaye, anasema kwamba bado anapokea jumbe za aina hiyo.
Kim hakidhani kwamba kuna haja ya kumuomba mwanamume aliyemrekodi kuondoa video yake kwa sababu ilikuwa 'imetazamwa sana.'
Kim anasema alihisi kuvunjiwa heshima wakati mwanamume huyo alipokataa kuondoa kipande cha video ambapo anazungumzia kuhusu kazi na familia yake.
'Nilikuwa kama kifaa tu kwake, kipande cha nyama.'
Baadhi ya 'Mainfluensa' Yaani watengeneza maudhui mitandanoni ambao wanatengeneza video kama hiyo, hupata hela kutoka kwa wateja wao ambao huwalipa kupata mafunzo kuhusu na mawaidha kuhusu jinsi ya kumtongoza mwanamke.
Ikiwa maudhui yao yana umaarufu makubwa basi 'Mainfluensa' hao hupokea malipo kutoka kwa Mpango wa fidia wa TikTok .{TikTok Creator Reward Program}
Wakili anayeshughulikia masuala ya usalama wa haki z akibinafsi Jamie Hurwoth amesema kwamba wakati wa unampomrekodi video ya watu katika eneo la umma hadharani, hilo sio kinyue na sheria, 'Sheria inalinda haki ya mja ya maisha yake ya binafsi na inaweza kuwalinda watu binafsi waliopo katika maeneo ya umma na vile vike wakiwa katika maeneo ya kibinafsi.'
PICHA: Wakili Jamie Hurworth amesema kwamba hakuna sheria mahususi inayokataza kurekodi mtu katika maeneo ya umma bila ya idhini yake.
Lakini Beatriz Kira, ambaye ni Mhadhiri wa somo la sheria katika chuo kikuu cha Sussex, anasema kwamba ni vigumu kwa mifumo ya kubuni sheria kuwa sambamba na jinsi 'teknolojia bunifu inavyopanuka na matumizi yake yanavyotishia usalama wa wanawake mitandaoni.' Anapendekeza kuwepo kwa njia mbadala ya kuangazia suala la teknolojia zinazobuniwa kila uchao na kuweka udhibiti wake nchini Uingereza.
Rebecca Hitcen, kutoka shirika la {End Violence Against Women Coalition} anasema kwamba kampuni za teknolojia kama vile TikTok, zinatakiwa kuchukuwa hatua za kuzuia uwezekano wa maisha ya wanawake kuhatarishwa.
Maelekezo kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana kutoka kwa msimamizi wa masuala ya habari , OFCOM, ni sharti yachukuliwe kwa uzito wake aliongezea kusema na ' ni sharti yafanywe kuwa muongoz wa lazima na ambaye atayakiuka kupata adhabu kali.'
Wanawake waliozungumza na BBC wamesema kurekodiwa kisiri – na kisha video hizo kuchapishwa mitandaoni, kumewaacha wakijiuliza maswali kujihusu na wanayeweza kumuamini.
'Nilikuwa tu mwema kwa mtu ambaye sikumjuwa,'alisema Kim. 'Kwa hilo, ni masikitiko makubwa kwamba imani hiyo imevunjwa.'