Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumamosi: Hakuna mpango wa Alexander-Arnold kuondoka Real Madrid
Beki wa kulia wa England, Trent Alexander-Arnold, hajaambiwa aondoke Real Madrid, licha ya ripoti kutoka Hispania kudai kuwa kocha mpya Alvaro Arbeloa amemtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atafute klabu mpya majira haya ya kiangazi. (Mail)
Arsenal wanachunguza uwezekano wa kufanya usajili wa kiangazi kwa mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina, Julian Alvarez, mwenye umri wa miaka 25. (ESPN)
Bayern Munich watakabiliwa na ushindani kutoka Liverpool katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast, Yan Diomande, 19, kutoka RB Leipzig. (Bild)
Beki wa England wa Liverpool, Joe Gomez, 28, anahitajika na AC Milan. (Calciomercato)
West Ham wamekataa ofa ya pauni milioni 32.9 pamoja na pauni milioni 3 kama nyongeza kutoka Flamengo kwa kiungo wa Brazil mwenye umri wa miaka 28, Lucas Paqueta. (The Athletic)
Kiungo wa Crystal Palace na England, Adam Wharton, 21, pamoja na kiungo wa Brighton na Cameroon, Carlos Baleba, 22, wameibuka kuwa malengo halisi zaidi kwa Manchester United kuliko kiungo wa Nottingham Forest na England, Elliot Anderson, 23, ambaye wanaamini atajiunga na Manchester City. (The I)
Liverpool wanatazamia kumrudisha beki wa kushoto wa Ugiriki, Kostas Tsimikas, 29, kutoka kwa mkopo wake Roma. (Talksport)
Chelsea wamefanya mawasiliano ya awali na Juventus kujadili dili la mkopo kwa kiungo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, Douglas Luiz, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Nottingham Forest. (Fabrizio Romano)
Rennes watamlenga beki wa kati wa England wa Toulouse, Charlie Cresswell, 23, iwapo beki wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 20, Jeremy Jacquet, ataondoka kwenda Chelsea. (Florian Plettenberg)
Brighton wamemweka wazi kuwa winga wa England mwenye umri wa miaka 19, Tommy Watson, anapatikana kwa mkopo, huku klabu kadhaa za Championship na moja ya Premier League zikionyesha nia. (Sky Sports)