Kwa nini Marekani ilitumia silaha ya 'sauti' huko Venezuela?

Muda wa kusoma: Dakika 3

Madai ya kwamba "silaha ya kuzalisha sauti" isiyojulikana ilitumiwa nchini Venezuela yamezua uvumi kuhusu teknolojia ya kijeshi ya Marekani na madhara yake katika mwili wa binadamu.

Akaunti ya mashuhuda wa walinzi wa Venezuela, iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, ilisema kuwa silaha hizo ziliwalaziomu wanajeshi wa Venezuela na Cuba kupiga goti huku 'wakitokwa na damu' puani .

Ingawa utawala wa Trump haujathibitisha ikiwa silaha hiyo inaweza kutumika, wataalam wa ulinzi wanaashiria kifaa kinachojulikana cha sonic ambacho kimetumika kwa miaka mingi.

Silaha hiyo, inayojulikana kwa jina LRAD, imefafanuliwa kama "sauti ya aina tofauti," kulingana na Mark Cancian, Luteni Kanali mstaafu wa Wanamaji na mshauri mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa.

Huenda maafisa wa Marekani walizitumia walipotua Caracas, Venezuela, kuwachanganya wanajeshi wa Venezuela na kuwaonya kuweka chini silaha zao.

Rais Trump alijigamba Jumanne jioni kwamba 'hakuna mtu mwingine' aliye na silaha hizi, akijivunia uwezo wa jeshi la Marekani.

Maswali yanabaki juu ya aina ya silaha na jinsi ilivyotumiwa. Trump alisita kutoa maelezo zaidi alipohojiwa na Katie Pavlich wa NewsNation.

"Ni silaha ambayo hatuitaki...hakuna mtu mwingine aliye nayo," alisema. "Lakini tuna silaha ambayo hakuna mtu mwingine anayeijua," aliongeza.

"Ninasema ni bora kutozungumza juu yake, lakini tuna silaha za kushangaza," alisema na kuongeza, "ilikuwa shambulio la kushangaza."

Habari hizo zilijiri baada ya X kuripoti kuwa silaha ya ulemavu wa kusikia ilitumiwa nchini Venezuela ambayo iliwalazimu wanajeshi kutapika.

Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House Caroline Leavitt alishiriki ushahidi na X mapema mwezi huu.

Katika tovuti yake ya X, alishiriki mahojiano na mwanajeshi ambaye jina lake halikutajwa ambaye alisema alikuwa kazini usiku wa shambulizi dhidi ya Venezuela ambalo lilimkamata Maduro.

"Acha unachofanya na usome hii," aliandika, akitumia emoji inayoonyesha bendera ya Marekani.

Mahojiano hayo yalimwona mlinzi huyo akifichua nguvu ya kushangaza ya silaha mpya ya ajabu ya jeshi la Marekani, ambayo aliitaja kama 'wimbi la sauti kali sana' ambalo lililemaza vikosi vya Venezuela.

'Ghafla nilihisi kama kichwa changu kilikuwa kinalipuka ndani,' askari alisema. 'Sote tulikuwa na damu puani. Baadhi walitapika damu. Tulianguka chini, bila fahamu. Hatukuweza hata kusimama baada ya silaha kutumika.'

Ikulu ya Urusi Kremlin imeitaka Marekani kutoa taarifa zaidi kuhusu silaha hiyo ya ulemavu wa kusikia.

Msemaji wa Putin Dmitry Peskov alisema serikali yake itaanzisha uchunguzi na kukusanya taarifa za ziada kuhusiana na matamshi ya Trump.

Kupoteza kusikia kunahusishwa na hali inayojulikana kama Havana Syndrome, hali ya kutatanisha lakini bado haijaeleweka kikamilifu.

Dalili za kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kushindwa kufikiri vizuri, kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi, na usingizi.

Iwapo aina ya silaha, LRAD, ndiyo inayozungumziwa na inadhaniwa kuwa ilitumika, imekuwa ikitumiwa hapo awali na nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Israel.