Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini utawala wa Xabi Alonso Real Madrid umekwisha
Picha zilisambaa haraka. Kylian Mbappe akiwapa ishara wachezaji wenzake kuondoka uwanjani. Xabi Alonso akimtaka abaki. Mbappe akisisitiza. Na Xabi, hatimaye, akageuka na kufanya kama nyota yake ilivyodai. Hakuna gwaride la heshima kwa Barcelona baada ya ushindi wao wa Spanish Super Cup siku ya Jumapili.
Kwa wengi, ilionekana kama ukosefu wa bahati, jambo ambalo halikuhusishwa na Xabi Alonso. Pia ilionesha kitu tofauti kabisa, kwamba ni timu na sio meneja, anayesimamia.
,Na baada ya fainali ambayo ilikuwa ngumu, na goli la bahati mbaya, unaweza kufikiria Xabi akisema: inatosha.
Lakini hii haikuwa kujiuzulu. Na haikupangwa. Xabi Alonso hakutarajia kuondoka kama kocha wa Real Madrid - miezi saba na nusu tu baada ya kuteuliwa. Hapana
Katika taarifa rasmi, Real Madrid ilielezea kuondoka kwake kama "makubaliano ya pande zote" lakini ilikuwa ni kuondoka ambako hakukuepukika.
Baada ya kutofautiana sana na meneja wao kuhusu mbinu za mchezo katika miezi michache iliyopita, mwendo wa saa 4:30 usiku kwa saa za Uhispania siku ya Jumatatu, bodi ilikutana na uamuzi mezani - kuondoka kwa Xabi Alonso.
Maelezo aliyopatiwa na wasaidizi wake yalikuwa, yenye utata.
'Hakuwa na uwezo wa kutekeleza soka ambalo lilimfanya kuwa na mafanikio makubwa akiwa Bayer Leverkusen'. 'Hali ya kimwili ya timu haikuwa nzuri'. 'Wachezaji hawakuwa wameimarika'. 'Hawakuonekana kumchezea'.
Mechi alizopoteza ziliorodheshwa : Paris St-Germain katika nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, Atletico Madrid katika La Liga (5–2), miongoni mwa nyinginezo.
Na bado Real Madrid wako katika nane bora katika awamu ya Ligi ya Mabingwa, kinyang'anyiro ambacho wana hhistoria nacho .
Wametinga raundi inayofuata ya Copa del Rey na wako pointi nne nyuma ya Barcelona bada ya nusu ya mechi za La Liga, baada ya kuwashinda Wakatalunya hao walipokutana Oktoba. Mgogoro?
Zaidi ya shida, ilikuwa uthibitisho kwamba Florentino Perez hakuwahi kumwamini meneja wake.
Xabi Alonso alipendekezwa kwake na akakubali kuwa bosi mpya wa klabu, lakini bila hatia. Katika klabu yake ya awali ya Bayer Leverkusen, sio kila mtu alimpenda Xabi kuanzia siku ya kwanza.
Lakini matokeo yalionekana na kikosi kilimpenda. Huko Madrid, hata kwa matokeo mazuri, hiyo haikufanyika. Tangu mwanzo, Xabi alijisikia kuwa mpweke.
Kuanza kazi ya ukocha katika Real Madrid ni changamoto ngumu zaidi katika soka. Hakuna anayesema hapana kwa Madrid, hata wale ambao wanaelewa jinsi ilivyo vigumu kubadilisha utamaduni uliojengwa juu ya kipaji cha mtu binafsi ambapo kila mtu anashambulia na kila mtu anaweka ulinzi.
Meneja anakuwa na nguvu zaidi anapowasili, lakini Madrid waliounguza mamlaka yake tangu mwanzo.
Alitaka kuanza uongozi wake baada ya Kombe la Dunia la Klabu, sio kabla yake. Michuano hiyo ilichezwa baada ya msimu mrefu, huku wachezaji wakifikiria likizo na wengine wakijua hawatakuwepo mwaka unaofuata. Hakuruhusiwa hata kulijadili.
Usajili wa wachezaji wapya haukusaidia hata kidogo: Franco Mastantuono, aliyeuzwa na sehemu za vyombo vya habari kama mpinzani mkuu wa Yamal , hakuleta matokeo yoyote.
Mgogoro wa Vinicius Junior ulikuwa mwanzo wa mwisho, huku kiwango chake kikishuka na kumlaumu meneja mpya, kisha akapinga waziwazi kubadilishwa kwake kwenye El Clasico, kisha akaomba msamaha kwa kila mtu isipokuwa meneja.
Mazungumzo ya mkataba yalisitishwa ili kuona kilichotokea kwa Xabi.
Majeraha yaliharibu safu ya ulinzi, huku klabu ikipuuza ombi lake la kiungo (aliyemtaka Martin Zubimendi).
Hakukuwa na watu wenye nguvu wa kuunganisha timu kucheza kwa pamoja. Hata Federico Valverde alionekana kujali zaidi alikocheza kuliko timu ya pamoja.
Mbappe alitafuta kuvunja rekodi, sio kila alichohitaji kurekebisha baada ya kupona jeraha lake la hivi punde, akicheza na kufikia mabao 59 ya Cristiano Ronaldo katika mwaka wa kalenda.
Xabi hakuwahi kuwashawishi wachezaji kuwa njia yake ilikuwa njia sahihi. Na bila hiyo, hangeweza kulazimisha mashambulizi, mbinu ambayo iliisaidia timu yake ya Leverkusen.
Upi mustakbali wa Real Madrid?
Ni lazima aamue kama pumziko ndilo litakalofuata kwake. Wale wanaomjua wanafikiri kwamba kuondoka, ingawa hatakiwi, ingekuwa ni ahueni kidogo.
Mipango yake haikufanya kazi.
Lakini ujumbe kutoka kwa klabu kubwa za Ulaya uko wazi, wengi wangefurahi kuwa naye msimu ujao, ikiwa hali itaruhusu.
Real Madrid, kwa mara nyingine tena, inatazamwa na jicho shauku - klabu ambayo inafanya kazi tofauti, inaweka vikwazo kwa meneja wake, na hata kuandaa kimya kimya mazingira ya kutimuliwa kwa miezi kadhaa kabla ya kutokea, kwa kusaidiwa na vyombo vya habari vyenye uaminifu.
Anayefuata ni Alvaro Arbeloa, kocha wa Castilla. Mtu wa klabu. Lakini kama gwiji kama Xabi Alonso hangeweza kubadilisha utamaduni, Arbeloa anakabiliwa na kazi ambayo karibu haiwezekani.
Ikiwa msimu huu utamalizika bila mataji, wasomi wa Uropa watahisi kuthibitishwa katika imani yao. Iwapo, kwa mojawapo ya utata uliozoeleka wa soka, Real Madrid itaishia kunyanyua medali ya fedha, tutafikia hitimisho lile lile tunalofanya kila mara.
Kwamba baadhi ya mameneja wanafaa vilabu fulani. Na vilabu vingine vinakataa kusimamiwa hata kidogo.