Walinda amani wa UN wajeruhiwa baada ya Israel kushambulia mnara wa ulinzi Lebanon

Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa baada ya kifaru cha Israel kufyatua risasi kuelekea mnara wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon, Umoja wa Mataifa unasema.

Muhtasari

  • Tunachokijua kufikia sasa kuhusu mashambulizi ya Israel na Hezbollah
  • Walinda amani wa UN wajeruhiwa baada ya Israel kushambulia mnara wa ulinzi Lebanon
  • Waziri wa New Zealand akosoa kuhusishwa kwa ajali ya meli na jinsia ya nahodha
  • Watu saba wauawa kwa shambulio la Urusi kwenye bandari ya Ukraine
  • Zelensky akutana na Starmer anapotafuta msaada zaidi kivita
  • Wafanyakazi watano waliuawa na mashambulio ya anga ya Israel - Lebanon
  • Baadhi ya watu maeneo ya Florida hawana maji ya kunywa
  • Kenya yachaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Haki za Binadamu la UN
  • Taylor Swift asifiwa kwa kutoa msaada kwa waathirika wa kimbunga
  • Tajiri wa India Ratan Tata afariki dunia
  • Syria inasema shambulizi la Israel huko Damascus liliua raia
  • Kimbunga Milton chapungua nguvu huku kukitolewa onyo la mafuriko makubwa Florida
  • Hospitali inahamisha wagonjwa huku vifaru vya Israel vikizunguka kambi ya Jabalia
  • Biden na Netanyahu wajadili jibu la Israel dhidi ya Iran

Moja kwa moja

Na Asha Juma, Lizzy Masinga & Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mabashara kwa leo, asante kwa kuwa nasi, tunakuacha na video hii ya kimbunga Milton:

  2. Tazama: Kamera za wavuti za Florida zinaonyesha Kimbunga Milton kikitua

    Maelezo ya video, Tazama: Kamera za wavuti za Florida zinaonyesha Kimbunga Milton kikitua

    Kamera za Fort Myers, Tampa na Sarasota zimepiga picha Kimbunga Milton kilipotua maeneo hayo.

    Kimbunga Milton kina pepo za kasi ya kilomita 120 kwa saa (205km/h), kulingana na kituo cha taifa cha vimbunga cha Marekani, na kinasonga kaskazini-mashariki kwa takriban mita 15 kwa saa kikivuka Florida na kuelekea Atlantiki katika saa zijazo.

  3. Urusi imeshambulia bandari za Ukraine mara 60 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita - Ukraine

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Ghala la nafaka liliharibiwa vibaya katika shambulio la Urusi Orikhiv katika mkoa wa Zaporizhzhia.

    Naibu Waziri Mkuu wa serikali ya Ukraine Oleksiy Kuleba amesema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wanajeshi wa Urusi wameshambulia miundombinu ya bandari za Ukraine zilizoko kusini mwa nchi hiyo mara 60.

    Kwa mujibu wa Kuleba, mashambulizi haya hufanywa kwa makusudi na yanalenga kupunguza uwezekano wa Ukraine kuuza nje ya nchi bidhaa zake.

    "Tunazungumza juu ya uchochezi wa makusudi wa mgogoro wa chakula katika sehemu hizo za ulimwengu ambazo zinategemea moja kwa moja usambazaji wa nafaka za Ukraine," Kuleba aliandika kwenye kituo chake cha Telegram.

    Kutokana na makombora hayo, karibu vituo 300 vya miundombinu ya bandari, magari 177 na vyombo vya kiraia 22 viliharibiwa au kuharibiwa, Naibu Waziri Mkuu aliandika.

    Aliongeza kuwa wafanyakazi 79 wa bandari, kampuni za vifaa na wafanyakazi wa meli walijeruhiwa katika mashambulizi hayo

    Shambulio la hivi karibuni la Urusi dhidi ya miundombinu ya bandari ya Ukraine lilifanyika Alhamisi usiku: moja ya bandari katika mkoa wa Odessa ilishambuliwa kwa roketi, watu wanane waliuawa na karibu kumi walijeruhiwa.

    Jeshi la Urusi halikutoa tamko lolote kuhusu shambulio hilo.

    Vita vya Ukraine: Soma zaidi

  4. Tunachokijua kufikia sasa kuhusu mashambulizi ya Israel na Hezbollah

    Moshi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    • Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wajeruhiwa: Katika saa moja iliyopita, Umoja wa Mataifa unasema nafasi zake kusini mwa Lebanon zimeshutumiwa na vikosi vya Israel.
    • Walinda amani wawili walijeruhiwa baada ya mnara kushambuliwa, na moto kutoka kwa wanajeshi wa Israeli pia kugonga ngome ya UN, inasema.
    • Shambulizi kwenye shule za Gaza: Shambulio la anga la Israel limepiga shule inayohifadhi watu waliokimbia makazi yao huko Deir al-Balah.
    • Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas inasema takribani watu 28 waliuawa.
    • Mapigano yamekuwa yakiendelea Jabalia. IDF inasema "imeondoa magaidi 50" katika eneo hilo katika siku iliyopita.
    • Roketi za Hezbollah: Kundi linaloungwa mkono na Iran linasema kuwa limekuwa likirusha makombora zaidi kutoka Lebanon hadi kaskazini mwa Israel, hivi karibuni katika mji wa Karmiel.
    • Mashambulizi zaidi jana usiku: Jana usiku, wahudumu wa afya watano waliuawa katika shambulio la anga katika kijiji cha Derdghaiya kusini mwa Lebanon.
    • Huduma ya matibabu ya dharura ya Lebanon inasema inahofia misheni yake ya uokoaji kuathiriwa.
    • Kando na hilo, jeshi la Israel linasema kuwa limewaua makamanda wawili wa Hezbollah waliokuwa wamepanga mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Israel.
    • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo mchana kwa mazungumzo kuhusu Lebanon.
  5. Walinda amani wa UN wajeruhiwa baada ya Israel kushambulia mnara wa ulinzi Lebanon

    Askari

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa baada ya kifaru cha Israel kufyatua risasi kuelekea mnara wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon, Umoja wa Mataifa unasema.

    Kulingana na taarifa ya Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL), mnara wa uangalizi katika makao yake makuu huko Naqoura ulipigwa moja kwa moja, na kusababisha walinda amani hao kuanguka.

    "Imekuwa bahati nzuri kwa majeruhi, wakati huu, sio mbaya, lakini wamesalia hospitalini," UN inasema. Inaongeza kuwa wanajeshi wa Israel pia walifyatua risasi kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa huko Ras Naqoura, "na kugonga lango ambako walinzi wa amani walikuwa wakilinda, na kuharibu magari na mfumo wa mawasiliano".

    Unaweza kusoma;

  6. Waziri wa New Zealand akosoa kuhusishwa kwa ajali ya meli na jinsia ya nahodha

    Meli ikiwa imepinduka

    Chanzo cha picha, Samoan Government

    Waziri wa ulinzi wa New Zealand amewakosoa "maamiri jeshi" kwa kusema kwamba ilaumiwe jinsia ya kike ya nahodha kwa kusababisha kuzama kwa meli moja ya wanamaji ya taifa hilo.

    HMNZS Manawanui iligonga ardhi maili moja kutoka kisiwa cha Samoa cha Upolu Jumamosi usiku ilipokuwa ikichunguza mwamba. Baadaye ilishika moto na kupinduka.

    Watu wote 75 waliokuwa ndani ya meli hiyo walihamishwa kwenye boti za kuokoa maisha na kuokolewa mapema Jumapili, Jeshi la Ulinzi la New Zealand lilisema katika taarifa.

    Maafisa sasa wanachunguza chanzo cha tukio hilo na kutathmini uwezekano wa uharibifu wa mazingira kutokana na ajali hiyo.

    "Uchunguzi unafanyika kubaini kilichosababisha tukio hili baya," alisema Judith Collins, waziri wa ulinzi mwanamke wa kwanza wa New Zealand.

    "Jambo moja ambalo tayari tunajua halikusababisha ni jinsia ya nahodha wa meli."

    Collins alisema kuwa wanawake waliovalia sare wamenyanyaswa mitaani katika siku za hivi karibuni. "Hii ni tabia ya kuchukiza.

  7. Watu saba wauawa kwa shambulio la Urusi kwenye bandari ya Ukraine

    Makombora ya Urusi yamelenga eneo la Odesa la Ukraine wiki nzima

    Chanzo cha picha, Reuters

    Makombora ya Urusi yameigonga meli ya kontena za kiraia katika bandari, mkoa wa Odesa nchini Ukraine, na kuua watu saba, kulingana na maafisa wa eneo hilo.

    "Hili ni shambulio la tatu kwenye meli ya kiraia katika siku nne zilizopita," gavana wa eneo hilo, Oleh Kiper alisema.

    Alisema Urusi ililenga miundombinu ya bandari na waathirika wote ni Waukreni.

    Wengine kadhaa walijeruhiwa, na mfanyakazi wa bandari alifariki hospitalini kutokana na majeraha siku ya Alhamisi, Kiper aliongeza.

    Shambulio la hivi karibuni zaidi kwenye bandari moja ya Ukraine kwenye ufuo wa Bahari Nyeusi uliambatana na ziara ya Ulaya ya Rais Volodymyr Zelensky, ambaye anazuru viongozi wa London, Paris na Roma.

  8. Zelensky akutana na Starmer anapotafuta msaada zaidi kivita

    Sir Keir Starmer na Zelensky

    Chanzo cha picha, EPA

    Waziri Mkuu Sir Keir Starmer anakutana na Volodymyr Zelensky katika Mtaa wa Downing, wakati rais wa Ukraine akijaribu kupata uungwaji mkono wa Ulaya kwenye vita vya nchi yake.

    Zelensky alisema atatoa maelezo ya "mpango wake wa ushindi" wakati wa mkutano huo, wakati Sir Keir ameahidi "kuendelea kujitolea na kuunga mkono" Ukraine.

    Mazungumzo hayo yanakuja wakati mzozo kati yake na Urusi ukielekea katika msimu wake wa baridi wa tatu na huku kukiwa na matarajio ya Donald Trump, ambaye anaonekana kutoiunga mkono Ukraine, kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani mwezi Novemba.

    Mark Rutte, mkuu mpya wa muungano wa kijeshi wa Nato, pia amewasili Downing Street kushiriki katika mazungumzo na Zelensky.

    Unaweza kusoma;

  9. Wafanyakazi watano wa afya waliuawa na mashambulio ya anga ya Israel - Lebanon

    .

    Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha za matokeo ya shambulizi lililoua wahudumu wa afya

    Lebanon inasema wahudumu wa afya watano waliuawa katika shambulio la anga la Israel katika mji wa Derdghaiya, kusini mwa nchi hiyo jana usiku.

    Shirika la habari la AFP limetuma picha kutoka eneo la tukio, huku waokoaji wakiendelea kutafuta chini ya vifusi.

    .

    Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

  10. Baadhi ya watu maeneo ya Florida hawana maji ya kunywa

    Palm trees in wind

    Chanzo cha picha, EPA

    Watu katika mji wa Florida wa St Petersburg hawana maji ya kunywa, baada ya maafisa kulazimika kufunga mfumo wa maji kutokana na uharibifu wa vimbunga.

    Maafisa wanasema kufungwa kwa mfumo huo kunatarajiwa kudumu "mpaka ukarabati unaohitajika ukamilike" na hii inaweza tu kufanywa wakati ni salama kwa wafanyikazi kuwa nje, taarifa hiyo inasema.

    Wakazi wote wameshauriwa kuchemsha maji yoyote yanayotumika kwa kunywa, kupikia na kupiga mswaki.

    Zaidi ya nyumba milioni 2.6 na biashara zakosa umeme

    Wakati huo huo, zaidi ya nyumba na biashara milioni 2.6 hazina umeme kote Florida, kulingana na data ya hivi punde.

    Pia maeneo mengine yameathirika - takriban wateja 70,000 hawana umeme huko North Carolina na 37,000 huko Georgia.

  11. Kenya yachaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Haki za Binadamu la UN

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kenya ni miongoni mwa nchi zilizochaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa mjumbe wa Baraza la Haki za Binadamu.

    Umoja wa Mataifa imesema mataifa hayo yatahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari mosi, 2025.

    Nchi zilizochaguliwa kutoka Afrika ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC), Ethiopia, Gambia na Benin kutoka Afrika.

    Hata hivyo kabla ya kuchaguliwa, makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Kenya yalikuwa yamepinga Kenya kupewa fursa hiyo kwa madai kwamba serikali iliyopo madarakani “imehusika na ukiukaji wa haki za kibinadamu”.

    Mashirika hayo yalinukuu ukiukwaji wa haki za binadamu kama vile mauaji ya kiholela, utekaji nyara na kutoweka kwa raia wakiwa mikononi mwa polisi.

  12. Taylor Swift atoa msaada wa $5m kwa waathirika wa kimbunga

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwigizaji wa pop wa Marekani Taylor Swift amesifiwa kwa kutoa $5m kama msaada kwa waathirika wa kimbunga Helene na Milton.

    Akielezea mchango wake kama "ukarimu", Claire Babineaux-Fontenot, ambaye anaongoza shirika lisilo la kifaida la Feeding America, alisema "utasaidia jamii kujenga upya, kupata chakula muhimu, maji safi na kujikwamua kutokana na dhoruba hizi mbaya" .

    "Pamoja, tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli katika kusaidia familia wanapokabiliana na changamoto zilizopo.

    "Asante, Taylor, kwa kusimama nasi katika harakati za kumaliza njaa na kusaidia jamii zenye uhitaji," Babineaux-Fontenot aliongeza.

  13. Tajiri wa India Ratan Tata afariki dunia

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tajiri wa India Ratan Tata amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, imesema Tata Group, muungano wa makampuni alioongoza kwa zaidi ya miongo miwili.

    Tata alikuwa mmoja wa viongozi wa biashara wanaotambulika kimataifa nchini India.

    Kundi la Tata ni mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya India, yenye mapato ya kila mwaka ya zaidi ya $100bn (£76.5bn).

    Katika taarifa ya kutangaza kifo cha Tata, mwenyekiti wa sasa alimtaja kama "kiongozi wa kipekee".

    Natarajan Chandrasekaran aliongeza: "Kwa niaba ya familia nzima ya Tata, ninatuma salamu zetu za rambirambi kwa wapendwa wake.

    "Alichoanzisha kitaendelea kututia moyo tunapojitahidi kuzingatia kanuni alizotetea kwa dhati."

    Waziri wa Biashara wa Uingereza Jonathan Reynolds alisema kwa heshima kwamba Tata alikuwa "nguzo muhimu katika ulimwengu wa biashara" ambaye "alichukua jukumu kubwa katika kuunda tasnia ya biashara Uingereza".

  14. Syria inasema shambulizi la Israel huko Damascus liliua raia

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imelaani shambulizi la anga linaloshukiwa kuwa la Israel katika jengo la ghorofa mjini Damascus na kusema kuwa, liliwauwa raia saba.

    Wizara hiyo ilisema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliofariki kutokana na shambulio la Jumanne jioni kwenye kitongoji cha Mezzeh, ambacho kina makao ya ubalozi wa Iran na vituo vingine vya kidiplomasia.

    Jeshi la Israel halijatoa maoni yoyote.

    Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria limesema idadi ya waliouawa ni 13, wakiwemo raia tisa na wanachama wawili wa kundi la Lebanon la Hezbollah, ambalo ni mshirika mkuu wa Iran na serikali ya Syria.

    Kikundi cha ufuatiliaji chenye makao yake makuu nchini Uingereza kilisema kuwa shambulizi hilo lililenga nyumba moja inayotembelewa na viongozi wa kundi la "Axis of Resistance" la Iran.

    Shirika la habari la serikali ya Syria, Sana, limekinukuu chanzo cha kijeshi kikisema kuwa jengo hilo lilishambuliwa na makombora matatu yaliyorushwa na ndege za Israel kutoka upande wa Milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu.

    Picha kutoka eneo la tukio zilionyesha wafanyakazi wa huduma za dharura wakikagua uharibifu mkubwa wa vyumba kwenye ghorofa ya kwanza, ya pili na ya tatu.

    "Nilikuwa nikielekea nyumbani wakati mlipuko ulipotokea na mawasiliano na umeme ukakatika, hivyo sikuweza tena kuwasiliana na familia yangu," fundi umeme Adel Habib, 61, anayeishi katika jengo hilo, aliliambia shirika la habari la AFP.

    "Hizi zilikuwa dakika tano ndefu zaidi za maisha yangu hadi niliposikia sauti za mke wangu, watoto na wajukuu zangu."

    Shirika la Kuchunguza Haki za Binadamu la Syria limewataja raia waliouawa kuwa ni daktari wa Yemen, mke wake na watoto wao watatu, pamoja na mwanamke na mtoto wake, daktari wa kike na mwanamume.

    Ubalozi wa Iran umesema kuwa hakuna raia wa Iran ambaye ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

    Siku ya Jumatano, afisa wa polisi wa Syria aliuawa katika shambulizi la Israel karibu na mji wa kusini-magharibi wa Quneitra.

    Soma zaidi:

  15. Kimbunga Milton chapungua nguvu huku kukitolewa onyo la mafuriko makubwa Florida

    ,

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kimbunga Milton kilitua katika maeneo ya Florida lakini sasa kimedhoofika na kuorodheshwa katika kitengo cha pili.

    Ingawa hata baada ya hatua hiyo, bado kina nguvu kweli na kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa na upepo mkali katika eneo hilo.

    Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa imetoa onyo la juu kuhusu mafuriko kwa maeneo ya kote Florida.

    Eneo la Tampa Bay, kwenye pwani ya magharibi ya Florida, limekuwa chini ya ushauri kwa saa nyingi, lakini maeneo mengine pia sasa yamejumuishwa.

    Orlando, katikati mwa jimbo, na maeneo ya pwani karibu na jiji la Daytona kwenye pwani ya mashariki pia yako chini ya onyo la mafuriko.

    Kulingana na NWS, onyo la mafuriko ya ghafla linamaanisha mafuriko "yamekaribia au yanatokea" na watu wanapaswa "kuchukua hatua" mara moja kuhamia maeneo ya juu.

    "Mafuriko ya ghafla yanaweza kuchukua muda wa kuanzia dakika hadi saa na kuendelea. Inawezekana hata kupata mafuriko katika maeneo ambayo hayapati mvua mara moja."

    Tazama jinsi Kimbunga Milton kinavyopiga eneo la Florida

    Maelezo ya video, Tazama: Kamera za eneo la Florida zinaonyesha Kimbunga Milton kinavyopiga

    Soma zaidi:

  16. Hospitali inahamisha wagonjwa huku vifaru vya Israel vikizunguka kambi ya Jabalia

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Mapigano yanaendelea huku milio ya risasi na mizinga ya Israel ikishuhudiwa, madaktari wa Palestina wanasema kuwa wameanza kuwahamisha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na wagonjwa wengine kutoka katika Hospitali ya Kamal Adwan katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, huku wanajeshi na vifaru vya Israel vikizunguka kambi ya Jabalia.

    Jeshi la Israel limekuwa likifanya mashambulizi yake ya tatu ya ardhini katika eneo hilo tangu vita vya Gaza kuanza, likisema kuwa linalenga kuwapanga upya wapiganaji wa Hamas wanaolenga kufanya mashambulizi.

    Hospitali zingine mbili za eneo hilo karibu haziwezi kufikiwa na zinakabiliwa na maagizo ya kuhamishwa, maafisa wa afya wa Gaza wanasema.

    Makumi ya watu wanaripotiwa kuuawa na kujeruhiwa upande wa kaskazini katika siku za hivi karibuni.

    Soma zaidi:

  17. Biden na Netanyahu wajadili jibu la Israel dhidi ya Iran

    .

    Chanzo cha picha, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel

    Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamezungumza kwa simu iliyokuwa ikitarajiwa kwa muda wa dakika 30 - ambayo inaaminika kuwa mawasiliano yao ya kwanza tangu Agosti - ambayo ilijumuisha majadiliano juu ya lengo la Israel kulipiza kisasi kwa shambulio la kombora la Iran wiki iliyopita.

    Ikulu ya White House ilielezea mazungumzo hayo kuwa ya "moja kwa moja" na "yenye tija", na kusema Biden na Netanyahu wamekubali "kuwasiliana mara kwa mara" katika siku zijazo. Makamu wa Rais Kamala Harris pia alijiunga na wito huo.

    Akizungumza muda mfupi baadaye, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema mashambulizi yake dhidi ya Iran yatakuwa "mabaya, sahihi na zaidi ya yote ya kushangaza".

    Nguvu mbili zimeungana pamoja. Mojawapo ni kusita sita kwa Joe Biden kushuhudia Marekani ikiburutwa kwenye vita na Iran ambayo inaamini haina ulazima na ni hatari.

    Nyingine ni hisia kali miongoni mwa baadhi ya Israel kwamba wana fursa ya kusababisha pigo kubwa dhidi ya Iran - adui yao mkubwa.

    Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hezbollah yamewapa nguvu Waisrael ambao walikuwa wakitamani sana kujinasua kutoka katika vita hivyo vya ugomvi kwenye mpaka wao na Lebanon.

    Upande wake, Lebanon, ilihisi kama mafanikio na maendeleo, tofauti kabisa na nafasi ya Gaza.

    Licha ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 42,000, wengi wao wakiwa raia, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hajaweza kutimiza malengo yake mawili ya vita - kusambaratishwa kwa Hamas na kuwaokoa mateka.

    Hamas bado inapigana, na bado inashikilia karibu mateka 100, ambao wengi wao wanaweza kuwa wamefariki.

    Uharibifu uliofanywa kwa maadui wa Israel, Hezbollah huko Lebanon na Hamas huko Gaza, umesababisha baadhi ya Waisrael kukubali kwa haraka kwamba hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa na kushambulia Iran moja kwa moja.

    Kwao, shambulio baya la anga dhidi ya Iran ni hatua inayowavutia ambayo hawakufikiria kufika huko.

    Maeneo lengwa katika orodha ya Waisrael wengi ni yenye ngome nyingi, mengine yakiwa ndani kabisa ya milima kuliko na vituo vya nyuklia vya Iran na Israel na wengine wanahofia kuwa vinaweza kutumika kutengeneza bomu.

    Soma zaidi:

  18. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 10/10/2024