Tunachojua kuhusu kijiji cha Syria kinachoweza 'kuchochea vita kati ya Israel na Hezbollah'

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Wakati Hizbollah ikikanusha kuhusika na shambulio la kijiji cha Majdal Shams katika eneo la Milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu, Israel inaendelea kulishutumu kundi la waasi la Lebanon kwa kuua watu 12 na kujeruhi makumi, na kuapa kulipiza kisasi, na kuzusha hofu ya "vita kamili" kati ya nchi hiyo. pande hizo mbili, kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na tovuti ya Axios, zikiwanukuu maafisa wa Marekani.

Maafisa wanahofia kwamba shambulio hilo linaweza kuongeza uwezekano wa kutokea vita kati ya Israel na Hezbollah, na kuzidisha mzozo wa kikanda na kuivuta Marekani katika mzozo huo, wakibainisha kuwa "Marekani imekuwa ikijaribu kuepusha hilo kwa muda wa miezi 10."

Mzozo kati ya Israel na Hezbollah umekuwa ukiftokota tangu shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7, huku mvutano ukiendelea kwenye mpaka wa pamoja wa kilomita 120.

Majdal Shams, maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema makabiliano kwenye mpaka wa Lebanon na Israel yanaweza kulitumbukiza eneo hilo kwenye "janga," na kutoa wito wa "utulivu" katika eneo hilo, kulingana na Reuters.

Jeshi la Israel limetangaza kuwa watu 12 wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa baada ya kombora kulipuka katika uwanja wa mpira wa miguu katika kijiji cha Druze kinachofahamika kama Majdal Shams katika milima ya Golan inayokaliwa kimabavu.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari aliilaumu Hezbollah kwa kuekeleza shambulio hilo, na kulielezea kama "shambulio mbaya zaidi" dhidi ya raia wa Israel tangu Oktoba, lakini Hezbollah ilikanusha vikali kuhusika na shambulio hili hatua.

Soma pia:
xx

Chanzo cha picha, Reuters

Majdal Shams ni wapi?

Majdal Shams iko katika eneo la Golan Heights, uwanda wa miamba kusini magharibi mwa Syria wenye umuhimu mkubwa wa kimkakati, ambao ulikaliwa na Israel wakati wa vita vya 1967 na kusalia chini ya udhibiti wake tangu wakati huo, ingawa jumuiya ya kimataifa inaitambua Milima ya Golan, kama sehemu ya Syria.

Hapo awali Majdal Shams ilisimamiwa chini ya ugavana wa kijeshi wa Israel, na mnamo 1981 Knesset ilipitisha Sheria ya Milima ya Golan, ambayo ilijumuisha eneo hilo katika mfumo wa baraza la mitaa la Israel na hatimaye kuunganishwa.

Hatua hii ilitambuliwa rasmi tna Marekani pekee, wakati wa utawala wa Donald Trump mnamo Machi 2019.

Jamii nne zilizosalia za Druze za Syria katika maeneo yanayokaliwa na Israel, Majdal Shams ndiyo kubwa zaidi, ikifuatiwa na Ein Qiniya, Masada, na Buqa'atha.

kwa mujibu wa Ofisi Kuu ya Takwimu ya Israel, Majdal Shams ilikuwa na wakazi 11,458 mwaka 2022, wengi wao wakiwa Druze.

Druze ni kina nani?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Druze ni kundi la kidini linaloishi kwenye maeneo ya kaskazini mwa Israel, Lebanon, Jordan na Syria. Nchini Israel wana haki ya uraia na wanakadiriwa kuwa1.5% ya raia wote wa nchi hiyo.

Wale wanaoishi katika eneo la Golan walipewa uraia wa Israel, pale eneo hilo lilipojitenga na Syria mwaka 1981, lakini sio kila mtu alikubali uraia huo.

Kundi la Druze linaloishi ndani ya Golan bado wanaweza kusoma na kufanya kazi, licha ya kuwa wale wenye uraia rasmi ndio wanaoweza kupiga kura.

Wanaume katika jamii ya Druze wanatakiwa kujiunga na jeshi. Hili ndio kundi kubwa zaidi ambalo lina asili ya uyahudi kwenye vikosi vya kijeshi vya Israel, IDF.

Nchi nyingi bado hazitambui umiliki wa Israel wa eneo la milima ya Golan.

Jamii ya Druze inayoishi katika milima ya Golan iliendelea kudumisha uhusiano wa karibu na Syria hata baada ya Israel kuliteka eneo hilo mwaka 1967 na kulichukuwa mwaka 1981, gazeti la Times of Israel linasema.

Gazeti hilo linasema kati ya Druze 21,000 wanaoishi katika miji minne katika Milima ya Golan ya Israel, takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani zinaonyesha kuwa takriban 4,300 kati yao ni raia wa Israel.

Golan ya Syria haihitaji ''utambulisho"

Mnamo mwaka wa 2018, mawakili wa Druze waliwasilisha malalamiko katika Mahakama Kuu ya Israel wakidai haki ya Druze kuchagua wawakilishi wao katika mabaraza ya manispaa kupitia uchaguzi, badala ya mfumo wa awali wa uteuzi.

Mahakama ilikubali malalamiko hayo, na Israel iliamua kujumuisha Druze katika Milima ya Golan katika uchaguzi wa manispaa kwa mara ya kwanza tangu ilipokaliwa kimabavu 1967.

Uamuzi huo ulizua mabishano miongoni mwa Wadruze, huku wengi wakieleza hofu kwamba Israel inafanya njama ya kuhalalisha udhibiti wake kwenye eneo hilo kwa kuwajumuisha katika mchakato wa uchaguzi.

Miongoni mwa waliokerwa na uamuzi huo ni pamoja na wakazi wa kijiji cha Majdal Shams, ambapo baadhi yao wakiwa na bendera za Syria, walikusanyika nje ya lango la vituo vya kupigia kura kwa lengo la kuwazuia wakazi wa mji huo kushiriki uchaguzi wa manispaa katika eneo hilo.

Maelezo zaidi:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi