Hezbollah ni nini?

Chanzo cha picha, EPA
Hezbollah ni chama cha kisiasa cha Washia na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Lebanon, ambacho kimeongozwa na Hassan Nasrallah tangu 1992. Jina lenyewe linamaanisha Chama cha Mungu.
Hezbollah iliibuka na usaidizi wa kifedha na kijeshi kutoka Iran wakati wa utawala wa Israel wa Lebanon katika miaka ya mwanzoni mwa 1980, na kama kikosi cha kuwatetea Shia wa Lebanon waliokuwa bila sauti upande wa kusini, ingawa mizizi yake ya kiitikadi inaanzia kwenye uamsho wa Uislamu wa Shia nchini Lebanon katika miaka ya 1960 na miaka ya 1970.
Baada ya Israel kujiondoa mwaka 2000, Hezbollah ilipinga shinikizo la kupokonywa silaha na kuendelea kuimarisha tawi lake la kijeshi, Islamic Resistance.
Kundi hilo pia polepole likawa wakala mkuu wa mamlaka katika mfumo wa kisiasa wa Lebanon - kupitia chama chake cha Loyalty to the Resistance Bloc - na kimepata nguvu ya kura ya turufu katika baraza la mawaziri.
Hezbollah imekuwa ikishutumiwa kwa miaka mingi kwa kutekeleza mfululizo wa mashambulizi ya mabomu na njama, hasa dhidi ya malengo ya Israel na Marekani. Imetajwa kuwa shirika la "kigaidi" na mataifa ya Magharibi, Israel, nchi za Ghuba za Kiarabu na Jumuiya ya Kiarabu (AL).
Mshirika mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad, Hezbollah ilituma maelfu ya wapiganaji kumpigania Bw Assad wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria vilivyoanza mwaka 2011 huku mzozo huo ukizidi, na hivyo kudhihirisha wazi kusaidia vikosi vinavyoiunga mkono serikali kurejesha maeneo waliyopoteza kwa waasi waasi hasa kwenye mpaka wa milima ya Lebanoni.
Israel mara nyingi hushambulia maeneo yanayolengwa nchini Syria yanayohusishwa na Iran na wanamgambo wa Hezbollah, lakini mara chache haikubali.
Kujihusisha kwa Hezbollah nchini Syria, kumezidisha mivutano ya kimadhehebu nchini Lebanon.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Uungaji mkono wake kwa rais wa Syria wa Shia Alawite na uhusiano mkubwa na Iran pia ulishuhudia kuongezeka kwa uhasama kutoka mataifa ya Ghuba ya Kiarabu, yakiongozwa na mpinzani mkuu wa Iran katika eneo hilo, Saudi Arabia.
Kufuatia shambulio la kushtukiza la kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba 2023, ambalo liliua takriban watu 1,400, Hezbollah na Israel zimerushiana risasi katika mpaka. Huku Israel ikianzisha mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi huko Gaza na kuua maelfu ya watu, kundi hilo lilisema liko tayari kabisa kuchangia katika mapigano dhidi ya Israel.
Jeshi la Hezbollah, usalama, na nguvu ya kisiasa pamoja na huduma za kijamii inazotoa zimeanzisha sifa yake kama dola ndani ya serikali, na kuonekana kushindana na taasisi za serikali na kupata ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapinzani wake. Kwa namna fulani, uwezo wake sasa unazidi ule wa jeshi la Lebanon, na nguvu yake kubwa ya kijeshi ilitumika dhidi ya Israeli katika vita vya 2006.
Baadhi ya Walebanon wanaichukulia Hezbollah kuwa tishio kwa uthabiti wa nchi hiyo, lakini ni maarufu sana ndani ya jumuiya ya Shia.
Pingamizi dhidi ya Israel
Asili sahihi ya Hezbollah ni vigumu kubainisha, lakini vitangulizi vyake viliibuka kufuatia uvamizi wa Israel kusini mwa Lebanon kujibu mashambulizi ya wanamgambo wa Kipalestina mwaka 1982, wakati viongozi wa Shia wanaopendelea jibu la wanamgambo walijitenga na vuguvugu kuu la Amal.
Shirika jipya, la Islamic Amal, lilipata usaidizi mkubwa wa kijeshi na wa kimantiki kutoka kwa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran ,Revolutionary Guards wenye makao yake katika Bonde la Bekaa, na likaibuka kuwa mashuhuri na madhubuti zaidi kati ya wanamgambo wa Shia ambao baadaye waliunda Hezbollah.

Chanzo cha picha, Reuters
Makundi hayo yalianzisha mashambulizi dhidi ya jeshi la Israel na mshirika wake, Jeshi la Lebanon Kusini (SLA), pamoja na mataifa ya kigeni nchini Lebanon. Wanaaminika kuwa walihusika na mashambulizi ya ubalozi wa Marekani na kambi ya Wanamaji ya Marekani mwaka 1983, ambayo kwa pamoja yalisababisha vifo vya Wamarekani 258 na wanajeshi 58 wa Ufaransa, na kusababisha vikosi vya kulinda amani vya Magharibi kuondoka.
Mnamo 1985, Hezbollah ilitangaza rasmi kuanzishwa kwake kwa kuchapisha "barua ya wazi" ambayo ilibainisha Marekani na Umoja wa Kisovieti kama maadui wakuu wa Uislamu na kutaka "kuangamizwa" kwa Israel, ambayo ilisema ilikuwa inazikalia kwa mabavu ardhi za Waislamu.
Pia ilitoa wito wa "kupitishwa kwa mfumo wa Kiislamu kwa msingi wa uteuzi huru na wa moja kwa moja wa watu, na sio msingi wa kulazimisha kwa nguvu".
Makubaliano ya Taif ya mwaka 1989 ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Lebanon na kutoa wito wa kupokonywa silaha wanamgambo uliifanya Hezbollah kubadili jina la tawi lake la kijeshi kama kikosi cha "Islamic Resistance" kilichojitolea kukomesha ukaliaji wa Israel, na kuiruhusu kutunza silaha zake.
Baada ya jeshi la Syria kuweka amani Lebanon mwaka 1990, Hezbollah iliendelea na vita vyake vya msituni kusini mwa Lebanon, lakini pia ilianza kutekeleza jukumu kubwa katika siasa za Lebanon. Mnamo 1992, ilishiriki kwa mafanikio katika uchaguzi wa kitaifa kwa mara ya kwanza.
Wakati majeshi ya Israeli hatimaye yalipoondoka mwaka 2000, Hezbollah ilipewa sifa ya kuwasukuma nje. Kundi hilo lilipinga shinikizo la kupokonywa silaha na lilidumisha uwepo wake wa kijeshi upande wa kusini, likidai kama halali wa kuendelea kuwepo kwa Israel katika Mashamba ya Shebaa na maeneo mengine yenye mzozo.
Mnamo 2006, wanamgambo wa Hezbollah walianzisha shambulio la kuvuka mpaka ambapo wanajeshi wanane wa Israeli waliuawa na wengine wawili kutekwa nyara, na kusababisha jibu kubwa la Israeli.
Ndege za kivita za Israel zilishambulia ngome za Hezbollah Kusini na katika vitongoji vya kusini mwa Beirut, huku Hezbollah ikirusha takriban roketi 4,000 dhidi ya Israel. Zaidi ya Walebanon 1,125, wengi wao wakiwa raia, walikufa wakati wa mzozo huo wa siku 34, pamoja na wanajeshi 119 wa Israeli na raia 45.
Hezbollah ilinusurika vita na ikaibuka kuwa na ujasiri. Ingawa tangu wakati huo imepandisha hadhi na kupanua safu yake ya silaha na kuajiri wapiganaji wapya wengi, kumekuwa hakuna milipuko mikubwa kwenye eneo la mpaka, ambalo sasa linasimamiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa na jeshi la Lebanon.

Chanzo cha picha, Reuters
Ushawishi mkubwa
Mwaka 2008, wakati serikali ya Lebanon inayoungwa mkono na nchi za Magharibi ilipoamua kuzima mtandao wa mawasiliano wa kibinafsi wa Hezbollah na kumuondoa mkuu wa usalama wa uwanja wa ndege wa Beirut juu ya uhusiano na kundi hilo, Hezbollah ilijibu kwa kutwaa sehemu kubwa ya mji mkuu na kupambana na makundi hasimu ya Sunni.
Ili kumaliza mapigano ya kimadhehebu yaliyosababisha vifo vya watu 81 na kuifikisha Lebanon kwenye ukingo wa vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe, serikali ilirudi nyuma na makubaliano ya kugawana madaraka yaliipa Hezbollah na washirika wake uwezo wa kupinga uamuzi wowote wa baraza la mawaziri.
Katika uchaguzi wa 2009, ilishinda viti 10 bungeni na kubakia katika serikali ya umoja.

Chanzo cha picha, Reuters
Baadaye mwaka huo huo, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Hassan Nasrallah alitoa ilani mpya ya kisiasa ambayo ilitaka kuangazia "maono ya kisiasa" ya kundi hilo.
Ilitupilia mbali marejeleo ya jamhuri ya Kiislamu iliyopatikana katika ilani ya 1985, lakini ikadumisha msimamo mkali dhidi ya Israel na Marekani na kusema Hezbollah ilihitaji kusalia na silaha zake.
Mnamo mwaka wa 2011, kundi hilo na washirika wake walilazimisha kusambaratika kwa serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Saad Hariri, Msunni anayeungwa mkono na Saudi Arabia, huku Hizbullah ikionya kwamba haitasimama kwa vile wanachama wake wanne walituhumiwa kuhusika na mauaji ya 2005 ya Baba yake ,Hariri Rafik.
Mnamo Desemba 2020, mwanachama wa Hezbollah Salim Ayyash alihukumiwa kifungo cha maisha bila kuwepo mahakamani na Mahakama Maalum ya Lebanon inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kwa kuhusika na mauaji hayo.
Hezbollah na washirika wake wameendelea kuwa sehemu ya serikali zinazofuata, ambapo wana ushawishi mkubwa.












