Majumba marefu ya New York yanasababisha mji huo kuzama ni nini kifanyike kuukomboa mji huo

Chanzo cha picha, Getty Images
Ardhi ya chini ya Jiji la New York inazama kwa kiasi fulani kutokana na wingi wa majengo yake yote na sio jiji pekee la pwani kukumbwa na tatizo hilo. Viwango vya maji ya bahari pia vinapanda na kufikia usawa wa misitu ,je hali hii inaweza kutatuliwa vipi.
Mnamo mwezi Septemba 27, mwka 1889, wafanyakazi walimaliza ujenzi wa Jengo la Mnara. Lilikuwa ni jengo la orofa 11 ambalo, kutokana na muundo wake wa chuma , lilikua jengo imara.linafikiriwa kuwa jengo refu la kwanza la jiji la New York.
Ni jengo lililojengwa kwa muda mrefu na mnara wake uliezekwa mwaka 1914 lakini kusimamishwa kwake kuliashiria mwanzo wa ujenzi ambao bado mpaka sasa haujawahi kutokea katika miji ya pwani.
kulingana na utafiti uliofanywa na wanajiolojia wa Marekani, inakadiriwa kwamba kilomita 777 ya mji wa new york imejengwa kwa tani milioni 762 za saruji, kioo na chuma, ingawa takwimu hiyo inahusisha baadhi maeneo ya mji huo na kuna tani kadhaa ambazo bado hazijajumuishwa kwenye ujenzi wa mji huo.
Uzito huo wote una athari ya ajabu kwa ardhi ambayo ipo katika eneo hilo la pwani. Kulingana na utafiti uliochapishwa mwezi Mei, ardhi inazama kwa milimita 1 mpaka 2 kwa mwaka kutokana na shinikizo linalotokana na uzito wa majengo yalio juu yake. jambo ambalo kwa miaka michache ijayo inaweza kusababisha shida kubwa katika eneo hilo la pwani.
Jiji la New York tayari limekuwa likipitia tatizo hilo tangu msimu wa baridi uliopita na harakati ya kuondolewa kwa uzito wa barafu katika baadhi ya maeneo yaliopo kwenye ukingo wa bahari , husababisha ardhi kutanuka na maeneo mengine ya pwani ikiwa ni pamoja na sehemu ambayo Jiji la New York huwa linabaki na muonekano wa kawaida.
''Lakini kutokana na uzito mkubwa wa majengo ya kwenye jiji la New york huwa kunatokea tatizo hilo la ardhi kudidimia', Parsons anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na hili ni janga la kimataifa, " New York inaweza kuonekana kama wakala wa miji mingine ya pwani nchini Marekani jambo linawafanya watu kuongezeka katika mji huo kila siku kwa lengo la kutafuta maisha , ajira na wengine kufanya tu ziara ya kujionea maajabu ya jiji hilo’’, anasema Parsons,
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kuna sababu nyingi zinazosababisha miji ya pwani kuzama, sababu moja wapo ni wingi wa miundombinu iliowekwa na bindamu katika maeneo hayo.
Kiwango cha miundombinu hii ni kikubwa: mnamo 2020 wingi wa vitu vilivyotengenezwa na wanadamu ulizidi ule wa biomasi yote hai.
Je, kuna hatua zozote zinaweza kuchukuliwa ili kuokoa miji hii ambayo ina mamilioni ya watu kudidimia na kuzama baharini?
Baadhi ya miji duniani kama vile Jakarta, mji mkuu wa Indonesia inazama kwa kasi kikubwa kuliko mingine. "Katika baadhi ya miji, mingine hali hiyo ya kudidimia inapungua kwa sentimita chache kwa mwaka," anasema Steven D'Hondt, profesa wa uchunguzi wa bahari katika Chuo Kikuu cha Rhode Island huko Narragansett.
Kwa kasi hii, jiji linazama kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko viwango vya maji ya bahari vinavyoongezeka na ili kuepukana na tatizo hili basi inabidi kasi iongezeke katika kuyeyusha barafu inayopatikana katika miji ya pwani.
D'Hondt ni mmoja wa waandishi watatu wa utafiti wa mwaka 2022 ambao walitumia picha za satelaiti kupima viwango vya kuzama kwa miji ya pwani katika miji 99 ya ulimwengu. "Ikiwa upungufu utaendelea kwa viwango vya hivi karibuni basi miji hii itakabiliwa na matukio makubwa ya mafuriko mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa," aliandika D'Hondt na wenzake Pei-Chin Wu na Matt Wei, ambao wote wako katika Chuo Kikuu cha Rhode Island.

Chanzo cha picha, Getty Images
Asia ya Kusini mashariki iliangaziwa sana katika orodha ya miji inayokabiliwa na upungufu wa haraka zaidi ya kudidimia. Sehemu za Jakarta zinapungua kati kwa 2cmm hadi 5cm (0.8-2in) kwa mwaka. Kando ya Jakarta, ambayo inabadilishwa kuwa mji mkuu wa Indonesia na mji unaojengwa umbali wa maili 1,240 (1996km) kutoka, kulikuwa na Manila (Ufilipino), Chittagong (Bangladesh), Karachi (Pakistani) na Tianjin (china). Miji hii tayari inakabiliwa na uharibifu wa miundombinu na mafuriko ya mara kwa mara.
Wakati huo huo, ingawa haiko kwenye pwani, mji wa Mexico unazama kwa kasi ya 50cm jambo linaloshangaza kwa mwaka kutokana na Wahispania kumwaga vyanzo vyake vya maji vya msingi walipoikalia kama koloni. Utafiti umependekeza kuwa inaweza kuchukua miaka 150 zaidi kabla ya tatizo la mji huo kuzama kutatuliwa.
Lakini miji ya pwani ambayo ni lengo la utafiti wa D'Hondt na wenzake. Sehemu kubwa ya Semarang nchini Indonesia, kwa mfano, inazama kwa cm mbili mpaka tatu (0.8-1.2in) kwa mwaka wakati eneo kubwa kaskazini mwa Tampa Bay, Florida, linapungua kwa 6mm (0.2in) kila mwaka.
Hata hivyo, hali hiyo inachochewa na mwanadamu si tu kwa uzito wa majengo yetu, lakini pia kutokana na uchimbaji wa visima kwa lengo la kupata maji ya kutumia kila siku na uzalishaji wetu wa mafuta na gesi ya kina. madhara yanayotokana na zoezi la uchimbaji ardhi hutofautiana kutoka kwa kulingana na kina kinachochimbwa na mtu mmoja mmoja , jambo linalosababisha hatua ya kuzuia janga la kudidimia kwa ardhi kuwa ngumu'' anasema Wei,
Lakini njia pekee ya kutatua tatizo hili ni ` ni kuangalia namna gani ya kumaliza kazi tunazofanya kwenye ardhi. Kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari husababisha uharibifu mkubwa na hata kupelekea kutoka kwa mafuriko,na mawimbi yanayoweza kuzimsha boti zote.

Chanzo cha picha, Getty Images
Madhara ya kwanza kuongezeka kwa usawa wa bahari, anasema D'Hondt, huanzia chini ya ardhi . hii ni kutokana na kwamba asilimia kubwa ya mkondo wa maji huwa unazikwa kwa chini kutokana na wingi wa majengo , miundombinu iliyozikwa, misingi ya majengo, na kisha, maji ya bahari hufunika maeneo hayo hali Hii inapoendelea, dhoruba huleta maji zaidi katika miji.
Suluhisho la tatizo hili linatofautiana kulinga na ukubwa wa tatazo lenyewe.
Njia moja ya wazi, ingawa ina madhara kwa mji uliondelea, ni kusitisha kuweka majengo mapya. Kama Parsons anavyoelezea, uwekaji wa ardhi chini ya majengo "kwa ujumla hukamilika mwaka mmoja au miwili baada ya ujenzi". Ingawa sehemu kubwa ya Jiji la New York ina msingi wa marumaru na miamba hii ina kiwango ambacho ardhi huongezeka au kupanuka na inapopasuka majengo huzama au kudidimia. Lakini kama eneo hilo lina udongo wenye rutuba nyenzo ambazo zimeenea sana katika eneo la chini basi kwa kiasi kikubwa eneo hilo hwa salama.
Kwa hivyo ili kuhakikishia usalama maeneo ya pwani ,basi majengo makubwa zaidi yajengwe kwenye mwamba thabiti ili kupunguza kasi ya mji kudidimia au kuzama.
suluhu lingine, angalau kwa baadhi ya maeneo, ni kupunguza kasi ya uchimbaji wa visima vya maji na uchimbaji kutoka kwa vyanzo vya chini ya ardhi. Parsons na wenzake wanaonya kwamba kuongezeka kwa idadi ya watu katika miji ya pwani kunapelekea matumizi ya maji kuwa makubwa na njia pekee ya kupata maji yenye uhakika ni kuchimba visima chini ya ardhi na na kuunganishwa na ujenzi zaidi ili kukabiliana na kuongezeka kwa idadi ya watu.
Kutafuta njia endelevu zaidi za kusambaza mahitaji ya maji ya jiji na kudumisha viwango vya maji chini ya ardhi kunaweza kusaidia.
Hata hivyo, mbinu inayojulikana zaidi ni programu isiyo kamilifu ya kujenga na kudumisha ulinzi wa mafuriko kama vile kuta za bahari. Marekebisho ya Tokyo ili kuzuia ardhi ni ya pande mbili. Jiji limejenga miundo mbinu halisi kama vile nguzo za zege, kuta za bahari, na kuweka njia inayoruhu maji kusambaa kwenda baharini. Hizi zimeunganishwa na hatua za kijamii kama vile mazoezi ya uokoaji na mfumo wa kutoa onyo ya kuwepo kwa majanga mapema.
Uchimbaji wa visima vya maji na mafuta huchochea kwa kiasi kikubwa hali hiyo
Wakati mwingine wakazi wenyewe husababisha hali hii. Utafiti wa mwaka 2021 uliandika jinsi wakazi wa Jakarta, Manila na Ho Chi Minh City wamechukua hatua zao binafsi, zisizo rasmi. Hizi ni pamoja na kuinua sakafu, kuhamisha vifaa vya nyumbani na, huko Manila, kujenga madaraja ya muda kati ya nyumba katika maeneo yenye miundo mbinu duni.
Zana nyingine muhimu ni pamoja na mizinga ya kupunguza uzito: mizinga mikubwa ambayo hukaa chini ya ardhi na kutoa maji ya dhoruba kwa kasi inayodhibitiwa, polepole. Martin Lamley, mtaalam wa mifereji ya maji katika kampuni ya utengenezaji wa mabomba ya Wavin, anasema kuwa matangi ya kupunguza maji yanapaswa kuunganishwa na vitu vya asili kama vile madimbwi, njia za kuloweka maji (mashimo yenye uchafu ambayo maji hutoka polepole) . “Changamoto tunazokabiliana nazo leo zinatofautiana sana na wakati mifereji ya maji taka mijini na mifereji ya maji ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza,” anasema.
Tunaweza kuona suluhu za kiubunifu zaidi kadri maji yanavyoongezeka. Mnamo mwaka 2019, umoja wa mataifa ilifanya majadiliano ya pande zote juu ya miji inayoelea, ambayo inaweza kuchukua muundo wa miundo ya pontoon. Hatimaye, kukomesha mabadiliko ya tabia nchi kwa kuondoa utoaji wa hewa ya ukaa kungezuia au kuchelewesha angalau kuyeyuka kwa sehemu za barafu, na hivyo kupunguza kasi ya kupanda kwa kina cha bahari.












