Israel yashambulia 'ikijiandaa kwa uwezekano wa kuingia' Lebanon - Mkuu wa jeshi
Mashambulizi ya hivi punde zaidi ya Israel dhidi ya Lebanon ni maandalizi ya uwezekano wa kuingia kwa wanajeshi, mkuu wa jeshi anasema.
Muhtasari
Takribani watu 51 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel - Wizara ya afya ya Lebanon
Hezbollah ina uwezekano wa kuwa na silaha nyingi
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hezbollah: Tunachojua kufikia sasa
Marekani yazitaka Israel, Lebanon kuepuka vita
Kiongozi mkuu wa Iran asema 'Hezbollah ni washindi'
Shambulio la Tel Aviv laonesha Hezbollah bado ni tishio
Watu 10 wauawa kwa shambulio la Israel nchini Lebanon
Sudan imerekodi vifo vingi zaidi vya akina mama duniani- MSF
Israel yazuia kombora la Kwanza la Hezbollah lililorushwa Tel Aviv
China yalifanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa
Kesi ya 11 dhidi ya Sean 'Diddy' Combs yawasilishwa akiwa bado gerezani
Trump aonywa na huduma za usalama Marekani juu ya vitisho vya mauaji ya Iran - kambi yake ya kampeni
Starmer awaambia Waingereza waondoke Lebanon mara moja
UN yasema wafanyakazi wao ni miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel
Ryan Routh ashtakiwa kwa jaribio la kumuua Trump
Aina mpya ya ‘Papa zimwi’ yagunduliwa katika maji ya New Zealand
Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yanasababisha 'mauaji ya watu wengi' waziri wa afya asema
Moja kwa moja
Na Asha Juma
Israel yashambulia 'ikijiandaa kwa uwezekano wa kuingia' Lebanon - Mkuu wa jeshi
Chanzo cha picha, Reuters
Mashambulizi ya hivi punde zaidi ya Israel dhidi ya Lebanon ni maandalizi ya uwezekano wa kuingia kwa wanajeshi, mkuu wa jeshi anasema.
"Unasikia ndege zikiruka juu; tumekuwa tukishambulia siku nzima. Hii ni kuandaa mazingira ya kuingia kwako na kuendelea kuiadhibu Hezbollah," Herzi Halevi aliwaambia wanajeshi.
"Leo, Hezbollah ilipanua safu yake ya mashambulizi, na baadaye leo, watapata jibu kali sana. Jiandaeni. "Leo, tutaendelea, hatuachi; tunaendelea kuwagonga na kuwapiga kila mahali.
Lengo liko wazi sana, kuwarudisha salama wakazi wa kaskazini."
Anaongeza kuwa ili "kufanikisha hilo", jeshi "linatayarisha mchakato wa ujanja, ambayo ina maana kwamba buti zako za kijeshi, buti zako za uendeshaji, zitaingia kwenye eneo la adui, kuingia katika vijiji ambavyo Hezbollah imetayarisha kama vituo vikubwa vya kijeshi".
Takribani watu 51 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel - Wizara ya afya ya Lebanon
Chanzo cha picha, AFP
Takriban watu 51 waliuawa na zaidi ya 220 walijeruhiwa katika mashambulizi ya Israel huko Lebanon siku ya Jumatano, waziri wa afya wa Lebanon anasema.
Nalo jeshi la Israel linasema kuwa shabaha 280 za Hezbollah zilishambuliwa.
Katika taarifa yake ya hivi punde, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa ndege zake za kivita zimeshambulia takribani maeneo 280 ya Hezbollah nchini Lebanon siku ya Jumatano.
Inasema shabaha hizo ni pamoja na majukwaa ya uzinduzi ambapo mashambulizi yalifanyika kaskazini mwa Israel asubuhi, pamoja na maghala ya silaha na miundombinu mingine ya kijeshi.
Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa Jumatano ni shabaha 60 zinazotumiwa na Hezbollah, IDF ilisema katika ripoti ya awali.
Hezbollah ina uwezekano wa kuwa na silaha nyingi,
Chanzo cha picha, Reuters
Kombora lililorushwa na Hezbollah kuelekea Tel Aviv
liliripotiwa kuwa ni aina ya Qadr-1 iliyotengenezwa na Iran, kombora la masafa
ya kati ambalo linaweza kubeba kichwa cha vita cha kati ya kilo 700 na kilo
1,000.
Lingeweza kuharibu mengi ya majengo, kama yasingezuiwa katikati ya Israeli na moja ya mifumo mingi ya ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo, na katika
tukio hili ni mfumo kuitwa "David's
Sling" [uliotumika].
Hezbollah ina silaha kati ya 100,000 na 150,000,
ndege zisizo na rubani na makombora.
Hadi 10,000 kati ya silaha hizo zinaaminika kuwa ni makombora ya masafa ya kati, yanayoongozwa kwa usahihi, kama vile Fateh-110, ambayo
yanaweza kufika Tel Aviv na maeneo mengine yenye idadi kubwa ya watu nchini Israel. (Jerusalem
inachukuliwa kuwa shabaha inayolengwa kwa kiwango cha chini kwa sababu ya idadi
kubwa ya Wapalestina.)
Mwezi uliopita, Hezbollah ilitoa video ikijigamba kwa silaha zake kubwa za chini ya ardhi za
makombora hayo, na kutishia kuzitumia kuishambulia Israel iwapo vita vitazuka.
"Operesheni ya Kaskazini ya Israel",
iliyozinduliwa wiki hii, inalenga kuharibu silaha nyingi iwezekanavyo, ikiwa ni
pamoja na maeneo ambayo Israeli inasema
makombora yamefichwa katika nyumba za kibinafsi na karakana.
Lakini mtandao wa Hezbollah wa mahandaki na
mapango, uliojengwa katika mwamba mgumu wa kusini mwa Lebanon, ni mkubwa.
Licha
ya mashambulizi yote ya anga, kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na uwezo wa
kufyatua makombora mengi katika miji ya Israel, lakini uongozi wake pia
unafahamu kuwa kulipiza kisasi itakuwa ni jambo baya kwa Lebanon.
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hezbollah: Tunachojua kufikia sasa
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ndege za Israel zikishambulia maeneo ya Hezbollah
Takriban
watu 15 waliuawa katika wimbi la mashambulizi makubwa ya anga ya Israel katika
maeneo ya kusini na katikati mwa Lebanon.
Ikiwa
unajiunga nasi tu, haya ndiyo mambo mengine unayohitaji kujua:
Makumi
ya watu walijeruhiwa, kulingana na wizara ya afya ya Lebanon, ambayo inasema mashambulizi
hayo yalipiga miji ya katikati mwa Lebanon, mbali na mpaka wake na Israeli.
Hapo
awali, Israel ilisema kuwa ilinasa kombora la balistiki lililorushwa na
Hezbollah kuelekea Tel Aviv - roketi ya kwanza kama hiyo kulenga mji mkubwa wa
nchi hiyo.
Kundi
la Shia lenye ushawishi mkubwa linasema kuwa limerusha "dazeni ya
makombora" kaskazini mwa Israel.
Wazima
moto katika eneo hilo walisambaza picha zinazoonyesha ukubwa wa uharibifu wa
majengo katika eneo la Safed, ambapo maafisa wanasema hakuna majeruhi
walioripotiwa.
Maelfu
ya watu nchini Lebanon wanaendelea na safari, wakielekea kaskazini kuepuka
mashambulizi ya Israel kusini.
Jeshi la Israel linasema kuwa limeanzisha mashambulizi dhidi ya maeneo 60 ya Hezbollah kote Lebanon.
Marekani yazitaka Israel, Lebanon kuepuka vita
Chanzo cha picha, EPA
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amejitokeza hivi karibuni kwenye Kituo cha Habari cha CBS kuzungumzia kuhusu kuongezeka kwa mvutano nchini Lebanon kufuatia mashambulizi ya Israel.
Alisema njia bora ya watu kurejea makwao kusini mwa Lebanon na kaskazini mwa Israel sio vita bali kupitia "diplomasia". "Tunalenga hivi sasa katika kuhakikisha kuwa tunaweza kuepuka vita kamili," Blinken alisema.
Blinken pia aliulizwa kuhusu mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel na kusema kuwa wakati kuna makubaliano, Hamas haijashiriki mazungumzo katika wiki za hivi karibuni.
"Bado inahitaji maamuzi magumu kwa upande wa Israel, lakini ni njia bora ya kukomesha kile kinachotokea Gaza, kuwatoa mateka," alisema.
"Lakini pia, kama ulivyosema, itasaidia kaskazini. Itatoa njia kwa Hezbollah kujiondoa na kuruhusu diplomasia kufanya kazi."
Kiongozi mkuu wa Iran asema 'Hezbollah ni washindi'
Chanzo cha picha, Reuters
"Hezbollah ni washindi," kiongozi mkuu wa Iran alichapisha kwenye akaunti yake rasmi ya X asubuhi ya leo, majibu ya kwanza kutoka kwa Ayatollah Ali Khamenei kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na Hezbollah.
Hatua hiyo Inakuja huku kukiwa na uvumi kuhusu hadhi ya Iran katika kuunga mkono Hezbollah, chama chenye ushawishi mkubwa cha Waislamu wa madhehebu ya Shia na kundi lenye silaha ambalo limepata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa Iran, kifedha na kijeshi, kwa miaka mingi, hasa inapoonekana Tehran inajaribu kujitenga na nchi za Magharibi na kufikia makubaliano katika mazungumzo ya nyuklia.
Akizungumza mjini New York siku ya Jumatatu, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alisema kuwa Iran haitafuti vita pana zaidi katika Mashariki ya Kati na kwamba mzozo huo hautakuwa na washindi.
Na katika mahojiano na shirika la habari la Reuters, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uangalizi wa nyuklia, Rafael Grossi alisema kuwa amehisi nia kubwa ya maafisa wa Iran kushirikiana na shirika hilo kwa njia ya maana zaidi baada ya mazungumzo mjini New York, na kwamba anatarajia kusafiri hadi Tehran mwezi Oktoba.
Haya yote yanazua maswali kuhusu msimamo wa Iran, ikiwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Hezbollah yataongezeka na Lebanon kuingia katika vita kamili.
Shambulio la Tel Aviv laonesha Hezbollah bado ni tishio
Chanzo cha picha, Reuters
Shambulio la leo la Hezbollah, mara ya kwanza kundi hilo lililenga Tel Aviv kwa kombora, linaweza kuwa ujumbe kwa Israeli: wanaweza kuwa wamedhoofika lakini wanasalia kuwa tishio.
Kundi hilo limekumbwa na wimbi la mashambulizi ambalo halijawahi kushuhudiwa ambalo liliharibu sana uwezo wake wa kufanya kazi, lakini halijazuia uwezo wake wa kupigana.
Wik iliyopita, shambulio dhidi ya vifaa vya mawasiliano na simu za upepo zilipunguza mawasiliano yao. Kisha, shambulio la anga kwenye ngome yake ya Dahieh, kusini mwa Beirut, ambalo kimsingi lilimaliza safu ya kamandi ya kitengo chake kikuu cha mapigano, Kikosi cha Radwan.
Na siku ya Jumatatu, kampeni kali na iliyoenea ya anga ikilenga maeneo ya kufyatua roketi na maeneo ya kuhifadhi silaha.
Mashambulizi hayo ya anga yamesababisha vifo vya takribani watu 500, wakiwemo raia wengi, waziri wa afya wa Lebanon anasema.
Ilikuwa siku mbaya zaidi nchini Lebanon tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mnamo 1990.
Hezbollah imesalia na msimamo mkali, ikiapa kuendelea na mashambulizi yake, huku kukiwa na uvumi kwamba mkakati wa Israel unaweza kujumuisha uvamizi wa ardhini kusini mwa Lebanon, kuunda eneo la amani, kuharibu miundombinu yake na kuwasukuma wapiganaji mbali na mpaka.
Wakati huo huo, maelfu bado wako kwenye harakati, wakielekea kaskazini kutafuta usalama.
Watu 10 wauawa kwa shambulio la Israel nchini Lebanon
Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu sita wameuawa baada ya mashambulizi ya Israel nchini Lebanon.
Watu wanne waliuawa na wengine saba kujeruhiwa katika mji wa Joun, katikati mwa Lebanon, wizara hiyo inaongeza. Awali wizara hiyo ilisema watu sita wamefariki katika maeneo mengine mawili.
Watu watatu waliuawa na kumi na watatu kujeruhiwa katika mji wa Ain Qana, kusini mwa Lebanon, na wengine watatu waliuawa na wengine tisa kujeruhiwa huko Al-Maaysra huko Keserwan, wizara hiyo inaongeza.
Sudan imerekodi vifo vingi zaidi vya akina mama duniani- MSF
Chanzo cha picha, AP
Shirika la madaktari
wasio na mipaka Médecins Sans Frontières - MSF, linaonya kuhusu mgogoro mkubwa
wa kiafya katika eneo la Sudan Kusini mwa Darfur.
Katika
ripoti mpya, shirika hilo linasema vifo mia moja na kumi na nne (114) vya akina
mama vilirekodiwa kati ya Januari na Agosti, huku maelfu ya watoto sasa
wakikabiliwa na baa la njaa.
Shirika hilo
linasema wanawake wajawazito, akina mama na watoto wachanga wanakufa kutokana
na masuala ya kiafya yanayoweza kuzuilika huku mfumo wa afya wa eneo hilo
ukiporomoka.
MSF
inazitaka pande zinazozozana kukomesha unyanyasaji, hasa dhidi ya wanawake na
watoto, na kuruhusu misaada ya kuokoa maisha kuwafikia watu waliokimbia makazi
yao.
Ripoti hiyo pia inatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua
hatua za haraka ili kuzuia kupoteza maisha zaidi.
Hii inafuatia ripoti za vyombo vya habari vya ndani
kuhusu mashambulizi ya anga ya jeshi la Sudan kwenye uwanja wa ndege huko
Darfur Kusini siku ya Jumanne.
Mashambulizi hayo yanadaiwa kulenga ndege za mizigo
zinazopeleka vifaa kwa wanamgambo wa RSF ambao wamekuwa wakipambana na jeshi la
Sudan tangu Aprili mwaka jana.
Vita vya
wenyewe kwa wenyewe hadi sasa vimeua maelfu ya watu na mamilioni ya wengine
kuyahama makazi yao kote Sudan.
Israel yazuia kombora la Kwanza la Hezbollah lililorushwa Tel Aviv
Hezbollah imesema ilirusha kombora la balistiki kuelekea
Tel Aviv saa kumi na mbili unusu asubuhi ya leo - ili kuunga mkono "mapigano
ya kishujaa na ya heshima" ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na
"kuilinda Lebanon na watu wake".
Msemaji huyo
alisema wamelenga makao makuu ya shirika la kijasusi la Israel Mossad, wakidai
"linahusika na mauaji ya viongozi na kulipua vifaa vya mawasiliano vya umeme
na vile visivyotumia umeme".
Israel
imelaumiwa kwa mashambulizi hayo yaliyoanzisha mapigano wiki iliyopita, lakini
haijadai kuhusika nayo.
Chombo cha
habari cha Israel Haaretz Ynet kimesema hii ni mara ya kwanza kabisa kwa
Hezbollah kulenga eneo la mji mkuu wa Tel Aviv.
Jeshi la Israel
linasema ving'ora vya mashambulizi ya anga vilisikika karibu na Tel Aviv na
Israel ya kati, lakini kombora hilo lilinaswa na hakukuwa na ripoti za
uharibifu au majeruhi.
Imetoa
ramani hii, ikisema haya yalikuwa maeneo ambayo ving'ora vililia:
Chanzo cha picha, Israel Defence Forces/X
Maelezo ya picha, Ramani ya maeneo ambapo ving'ora vililia Jumatano asubuhi
Israel
yasema ni 'mara ya kwanza kabisa' kombora la Hezbollah kufika Tel Aviv - AFP
Msemaji wa
jeshi la Israel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "ni mara ya
kwanza kwa kombora la Hezbollah kufika eneo la Tel Aviv",
Kundi
linalojihami la Lebanon linasema kuwa lilikuwa likilenga makao makuu ya
kijasusi ya Israel, ambayo yako karibu na Tel Aviv.
Tel Aviv na
vitongoji vinavyozunguka jiji hilo ndio eneo la mijini lenye watu wengi zaidi
nchini Israeli.
China yalifanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa
Chanzo cha picha, Getty Images
China imesema kuwa ilifanikiwa kurusha kombora la balestiki
linalovuka mabara (ICBM) lililobeba kichwa cha nyuklia kuelekea Bahari ya
Pasifiki.
Kombora la ICBM lilirushwa saa 08:44 kwa saa za eneo siku
ya Jumatano na "lilianguka katika maeneo ya bahari yaliyotarajiwa",
wizara ya ulinzi ya Beijing ilisema, na kuongeza kuwa majaribio hayo ni
"kawaida" na sehemu ya "mafunzo yake ya kila mwaka".
Aina ya kombora na njia yake ya kupaa haijafahamika,
lakini vyombo vya habari vya serikali ya China vilisema Beijing
"imeziarifu nchi zinazohusika mapema".
Wachambuzi
walisema maelezo ya Beijing ya jaribio hilo kama "kawaida"
yanashangaza kwa sababu jaribio la mwisho kama hilo lilifanyika mnamo 1980.
Majaribio ya silaha za nyuklia za China kwa kawaida
hufanyika ndani ya nchi na hapo awali ilifanyia majaribio ya mamkombora ya
kuvuka mabara ICBM magharibi kwenye Jangwa la Taklamakan katika eneo la
Xinjiang.
"Labda iwe kuna kitu sikielewi, nadhani hii ni mara
ya kwanza kutokea - na kutangazwa namna hiyo – katika kipindi cha muda
mrefu," Ankit Panda, mtaalamu wa silaha za nyuklia katika jopo la washauri
la Carnegie Endowment for International Peace, aliandika kwenye mtandao wa X.
Aliongeza kuwa maelezo ya Beijing ya jaribio hilo kama
"kawaida" na "ya kila mwaka" yalikua yanashangaza,
"ikizingatiwa kuwa kawaida hawafanyi kitu cha aina hii na pia sio cha kila
mwaka".
Wizara ya
ulinzi ya Japan ilisema hakuna uharibifu wowote kwa meli zake kuanzia alasiri
ya Jumatano.
"Tutaendelea
kukusanya na kuchambua habari kuhusu mienendo ya jeshi la China na tutachukua
tahadhari zote zinazowezekana katika umakini na ufuatiliaji wetu," wizara
ilisema, kulingana na shirika la utangazaji la Japan NHK.
Kesi ya 11 dhidi ya Sean 'Diddy' Combs yawasilishwa akiwa bado gerezani
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamuziki wa Hip-hop Sean "Diddy" Combs kwa sasa
yuko chini ya ulinzi wa serikali akisubiri kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za
ulaghai na utumwa wa ngono.
Kukamatwa kwake wiki iliyopita mjini New York kulitokea huku kukiwa na msururu wa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa
kimwili, dhidi yake na mengine yakianzia miaka ya 1990.
Mlalamishi wa 11 na
wa hivi punde kujitokeza ni Thalia Graves, anadai Combs na mlinzi wake walimpa
dawa za kulevya , kumfunga na kumbaka mnamo 2001, na kurekodi tukio hilo.
Rapa huyo mzaliwa wa Harlem amekana makosa ya jinai.
Kesi ya jinai inahusu nini?
Combs, 54, alikamatwa Jumatatu Septemba 16 katika hoteli ya
New York kwa tuhuma za kula njama, kuendesha biashara ya utumwa wa ngono na
uhalifu mwingine .
Waendesha mashtaka wa serikali kuu wamemshutumu kwa "kuunda biashara ya
uhalifu" ambapo "aliwanyanyasa, kutishia, na kulazimisha wanawake na
wengine walio karibu naye kutimiza tamaa zake za kingono, kulinda sifa yake, na
kuficha tabia yake".
Walisema Combs ametumia dawa za kulevya, vurugu na nguvu ya
hadhi yake "kuwavutia waathiriwa wa
kike" katika vitendo vya ngono katika karamu zake zinazoitwa "Freak Offs".
Pia walifichua walikuwa wamepata bunduki, risasi na chupa zaidi ya 1,000 za
mafuta wakati wa uvamizi katika nyumba
za Combs huko Miami na Los Angeles mnamo Machi.
Trump aonywa na huduma za usalama Marekani juu ya vitisho vya mauaji ya Iran - kambi yake ya kampeni
Chanzo cha picha, EPA
Donald Trump
amefahamishwa na idara ya kijasusi ya Marekani kuhusu vitisho kutoka kwa Iran
vya kutaka kumuua, kambi yake ya kampeni ilisema.
Mgombea
urais wa chama cha Republican alifahamishwa "kuhusu vitisho vya kweli na
mahususi kutoka kwa Iran vya kutaka kumuua katika juhudi za kuyumbisha na
kuzusha machafuko nchini Marekani", kambi yake ya kampeni ilisema katika
taarifa.
Haikufafanua madai hayo, na haikufahamika mara moja iwapo
vitisho iliyokuwa inarejelea ni vipya au viliripotiwa awali.
Serikali ya Iran haikujibu mara moja ombi la maoni yake,
lakini Tehran hapo awali ilikanusha madai ya Marekani ya kuingilia masuala ya
Marekani.
"Maafisa wa ujasusi wamegundua kuwa mashambulizi
haya yanayoendelea na yaliyoratibiwa yameongezeka katika miezi michache
iliyopita," mkurugenzi wa mawasiliano wa kambi ya kampeni ya Trump, Steven
Cheung alisema katika taarifa hiyo.
"Maafisa wa utekelezaji wa sheria katika mashirika
yote wanafanya kazi kuhakikisha Rais Trump analindwa na uchaguzi hauingiliwi,"
aliongeza.
BBC imeenda kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa
nchini Marekani kwa maoni.
Haya yanawadia baada ya Bw Trump kunusurika katika
jaribio la mauaji mnamo Julai 13, alipojeruhiwa na mtu mwingine kuuawa kwa
kupigwa risasi kwenye mkutano huko Pennsylvania.
Nia ya tukio hilo bado haijabainika na bado linachunguzwa.
Siku chache baadaye, vyombo vya habari vya Marekani
viliripoti kwamba maafisa walipokea taarifa za kijasusi kuhusu njama
zinazodaiwa kuwa za Iran dhidi ya rais huyo wa zamani.
Maafisa wa Iran wakati huo walikanusha madai hayo na
kusema ni ya "uovu", iliripoti mshirika wa BBC wa Marekani CBS habari.
"Iwapo 'watamuua Rais Trump,' jambo ambalo linawezekana,
ninatumai kuwa Marekani itaiangamiza Iran, kuifuta kabisa kwenye uso wa Dunia -
Ikiwa hilo halitafanyika, Viongozi wa Marekani watachukuliwa kuwa waoga 'wasio
na ujasiri'!" Bw
Trump aliandika kwenye jukwaa lake la Truth Social platform wakati huo.
Kisha tarehe
15 Septemba, Shirika Maalum la Usalama liliona bunduki ikipenya kwenye uzio
katika Klabu ya Gofu ya Kimataifa ya Trump huko West Palm Beach.
Ofisa wa
shirika hilo alifyatua risasi Bw Trump alipokuwa akicheza gofu.
Starmer awaambia Waingereza waondoke Lebanon mara moja
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu amewaambia raia wa Uingereza walioko Lebanon
"sasa ni wakati wa kuondoka" baada ya mapigano kushika kasi kati ya
Israel na Hezbollah, kundi linalomiliki silaha linaloungwa mkono na Iran ambalo
linatawala nchi hiyo.
Sir Keir Starmer alisema "tunaongeza mipango ya
dharura, nadhani ungetarajia hilo kutokana na ongezeko la mapigano", na
kuongeza kuwa raia wa Uingereza wanapaswa "kuondoka mara moja."
Wizara ya Ulinzi inatuma wanajeshi 700 kwenda karibu na
Cyprus kujiandaa kwa uwezekano wa kuwahamisha raia wa Uingereza kutoka Lebanon
na serikali "inaendelea kutoa ushauri dhidi ya safari zote za kwenda
Lebanon".
Hali nchini humo, ambapo mashambulizi ya Israel
yameripotiwa kuua zaidi ya watu 560 wiki hii, inaelezwa kuwa inazidi kuzorota
"kwa kasi, na matokeo ni mabaya".
Waziri wa
afya wa Lebanon ameiambia BBC kinachoendelea nchini mwake ni
"mauaji", huku hospitali zikijitahidi kukabiliana na idadi ya
waliofariki kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel kwa siku mbili
yanayolenga Hezbollah.
Alipoulizwa
na waandishi wa habari jinsi waziri mkuu wa Uingereza atahakikisha hali hiyo
hairudii machafuko katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul wakati Taliban
walipochukua udhibiti mnamo Agosti 2021, Sir Keir alisema: "Ujumbe muhimu
zaidi kutoka kwangu kwa raia wa Uingereza huko Lebanon, ni kuondoka mara moja.
"Ni
muhimu kwamba tumekuwa wazi kabisa: sasa ni wakati wa kuondoka."
Chanzo kikuu
cha serikali kiliongeza kuwa tofauti, kwa sasa, ni kwamba kulikuwa na ndege za
kibiashara zinazoondoka Lebanon.
Mawaziri wamerudia wito wao wa kusitisha mapigano mara
moja.
Waziri wa Ulinzi John Healey alisema: "Tunaendelea
kuzihimiza pande zote kurudi nyuma kutoka kwa mzozo ili kuzuia hasara zaidi ya kupoteza
maisha.
“Serikali yetu inahakikisha maandalizi yote yanafanyika
kusaidia raia wa Uingereza iwapo hali itazidi kuwa mbaya.
"Nataka kuwashukuru wafanyikazi wa Uingereza ambao
wapo katika eneo hili kwa kujitolea na taaluma yao."
Healey alifanya mkutano na mawaziri wenzake, wakuu wa
kijasusi na wanadiplomasia siku ya Jumanne mchana ili kufanyia kazi mipango ya
serikali.
‘Wafanyakazi wetu ni miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel’ - UN
Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la
Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema mmoja wa wafanyakazi wake na
mmoja wa watoto wake waliuawa katika shambulio la anga la Israel mashariki mwa
Lebanon - mojawapo ya zaidi ya mashambulizi elfu kama hayo katika muda wa siku
mbili zilizopita.
UNHCR
ilisema kuwa nyumba ya Dina Darwiche ilishambuliwa siku ya Jumatatu.
Mumewe na mwanawe mkubwa waliokolewa na wako hospitalini
wakiwa na majeraha mabaya, shirika hilo lilisema.
Bi Darwiche alikuwa amefanya kazi katika ofisi ya UNHCR
ya Bekaa kwa miaka 12.
Wakati huo huo Ali Basma, ambaye alikuwa amefanya kazi
katika ofisi ya UNHCR katika mji wa kusini wa Tiro ambaye anashughulika na usafi,
pia aliuawa.
Katika taarifa, shirika hilo lilisema
"limeghadhabishwa na kuhuzunishwa sana" na mauaji yao.
"Mashambulizi ya anga ya Israel nchini Lebanon sasa yamesababisha
mauaji ya mamia ya raia," mkurugenzi wa kimataifa wa UNHCR Filippo Grandi
alisema Jumanne.
"Na ninasikitika sana kuthibitisha kwamba wenzangu
wawili wa UNHCR pia waliuawa hapo jana."
Marafiki wa Bi Darwiche walimtaja kama "mtu mpole na
mkarimu zaidi tuliyemjua."
"Alikuwa amejitolea kwa kazi yake ya kutoa misaada
ya kibinadamu na UNHCR kwa muda mrefu niwezavyo kukumbuka," aliandika
Profesa Jasmin Lilian Diab, msomi katika Chuo Kikuu cha Lebanon cha Marekani,
kwenye mtandao wa X. "Nimevunjika moyo. Nimeumia kabisa."
Mazishi ya waliouawa yamekuwa yakifanyika kote Lebanon.
Katika mji
wa kusini wa Sidon, Mohammed Hilal alikuwa amekusanyika pamoja na mamia ya
waombolezaji wengine kumuaga bintiye katika mazishi ambayo pia yalifanywa kwa
ajili ya watu wengine wanane.
Wanachama
watatu wa Hezbollah walikuwa miongoni mwa waliozikwa, kulingana na shirika la
habari la Reuters ambalo lilirekodi tukio hilo.
Waendesha
mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka mwanamume aliyekamatwa karibu
na uwanja wa gofu wa Donald Trump wa Florida kwa jaribio la kumuua mgombeaji
urais.
Hili
linawadia siku moja baada ya jalada la mahakama kuonyesha Ryan Wesley Routh
alikuwa ameandika barua miezi kadhaa iliyopita akisema alikusudia kumuua Trump.
Routh, 58, tayari anakabiliwa na hadi miaka 20 jela kwa
mashtaka mawili yanayohusiana na bunduki.
Lakini anakabiliwa na kifungo cha juu zaidi cha maisha
jela ikiwa atapatikana na hatia kwa mashtaka mapya na makubwa zaidi.
"Vurugu zinazolenga maafisa wa umma zinahatarisha
kila kitu ambacho nchi yetu inasimamia," Mwanasheria Mkuu wa Marekani
Merrick Garland alisema katika taarifa, akiapa "kutumia kila chombo kilichopo"
kumuwajibisha Routh.
Trump ameishutumu serikali kwa kushughulikia kesi hiyo
vibaya, akiandika katika ujumbe wa mtandao wa kijamii siku ya Jumatatu kwamba wizara
ya sheria inapaswa "KUACHA FLORIDA ISHUGHULIKIE KESI HIYO!"
Lakini Garland alikataa hilo, akiwaambia waandishi wa
habari siku ya Jumanne kwamba shirika lake "litatafuta kushirikiana na
kupata usaidizi kutoka kwa" maafisa wa serikali "kulingana na
sheria".
Nyaraka za mahakama zinaonyesha kesi hiyo imetolewa bila
kufuata mpango maalumu kwa Jaji wa Wilaya ya Marekani Aileen Cannon.
Bi Cannon ndiye jaji wa Florida Kusini ambaye alipewa kesi
ya hati za siri za serikali ya Trump mwaka jana na ambaye aliitupilia mbali mapema
mwaka huu. Uamuzi wake kwa sasa uko chini ya rufaa.
Jaji tofauti mnamo siku ya Jumatatu aliamuru Routh abaki
rumande baada ya waendesha mashtaka kuhoji kuwa alikuwa na uwezekano wa
kutoroka nchi na hatari kwa jamii.
Mshukiwa
anazuiliwa katika kituo cha kizuizini huko Florida Kusini tangu kukamatwa kwake
tarehe 15 Septemba.
Aina mpya ya ‘Papa zimwi’ yagunduliwa katika maji ya New Zealand
Chanzo cha picha, NIWA
Wanasayansi wa New Zealand wamegundua aina mpya ya
"Papa zimwi" - aina adimu ya samaki ambao ni vigumu sana kuwaona kwa
sababu wanaishi kwenye kina kirefu katika Bahari ya Pasifiki.
Pia anajulikana
kama spookfish au chimera, na wana
uhusiano wa karibu na papa wa kawaida na samaki wa Ray fish. Hawana
magamba na mifupa yao imetengenezwa kwa
katileji kabisa.
Dk Brit Finucci,
mmoja wa wanasayansi waliogundua samaki aina ya Australasian Narrow-nosed
Spookfish, alisema ugunduzi huo ulikuwa "wa kusisimua".
"Makazi yao
yanawafanya kuwa wagumu kusoma na kufuatilia, ikimaanisha kuwa hatujui mengi
kuhusu biolojia yao au hali ya tishio," alisema.
Dk Finucci na
watafiti wengine kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Maji na Utafiti wa Anga ya New
Zealand (Niwa) walimpata kiumbe huyo katika eneo la sakafu ya bahari
linalojulikana kama Chatham Rise, ambalo liko mashariki mwa New Zealand.
Papa zimwi kwa kawaida huishi kwenye kina cha hadi
2,600m (maili 1.6).
Dk Finucci
alisema spishi hiyo ilitofautishwa na pua yake ndefu isiyo ya kawaida, ambayo
inaweza kusheheni nusu ya urefu wa mwili
wake.
Amempa samaki
huyo mpya jina la kisayansi: Harriota avia.
"Avia
inamaanisha nyanya kwa Kilatini, nilitaka kumpa taadhima hii kwa sababu aliniunga mkono kwa fahari
kupitia kazi yangu kama mwanasayansi," Dk Finucci alielezea.
Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yanasababisha 'mauaji ya watu wengi' waziri wa afya asema
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa afya wa Lebanon amesema kinachoendelea nchini
mwake ni "mauaji", huku hospitali zikijitahidi kukabiliana na idadi
ya waliopoteza maisha kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel yaliyoenea kwa
siku mbili yakilenga kundi la Hezbollah.
Dkt Firass Abiad aliiambia BBC ni "wazi" kwamba
wengi wa watu 550 waliouawa katika mashambulizi ya Jumatatu walikuwa raia,
ikiwa ni pamoja na watoto na wanawake.
Israel ilisema ilishambulia mamia ya maeneo ya Hezbollah,
ikilishutumu kundi hilo kwa kuficha silaha katika maeneo ya makazi.
Siku ya Jumanne, jeshi la Israel lilimuua mkuu wa vikosi
vya roketi vya Hezbollah wakati mashambulio hayo yakiendelea, huku Waziri Mkuu
Benjamin Netanyahu akisema kundi hilo lilikuwa linaiongoza Lebanon "kuzimu".
Hezbollah ilijibu kwa kurusha zaidi ya roketi 300
kaskazini mwa Israel, na kujeruhi watu sita, kulingana na jeshi.
Ijapokuwa hakuna upande ulionekana kuwa na nia ya kurudi
nyuma, Rais wa Marekani Joe Biden aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
kwamba mzozo kamili "haukuwa wa maslahi ya mtu yeyote" na kusisitiza
kwamba "suluhisho la kidiplomasia bado linawezekana".
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alionya
kwamba ulimwengu "hauwezi kumudu Lebanon kuwa Gaza nyingine".
Takriban mwaka mmoja wa mapigano ya kuvuka mpaka kati ya
Israel na Hezbollah yaliyochochewa na vita huko Gaza, yameua mamia ya watu
wengi wao wakiwa wapiganaji wa Hezbollah, na maelfu ya wengine kuyahama makazi
yao pande zote mbili za mpaka huo.
Hezbollah imesema inaiunga mkono Hamas na haitakoma hadi
kutakapokuwa na usitishaji vita huko Gaza.
Makundi yote mawili yanaungwa mkono na Iran na yamepigwa
marufuku kuwa mashirika ya kigaidi na Israel, Uingereza na nchi nyinginezo.