Agni-V: Je, ni kipi cha kipekee katika kombora la India lenye uwezo wa kushambulia China?

hj

Chanzo cha picha, ANI

Maelezo ya picha, Uzinduzi wa kombora la Agni-V

India imetangaza kurusha kwa mafanikio kombora la Agni-V lenye uwezo wa kubeba vichwa vingi vya silaha na kushambulia shabaha nyingi kwa wakati mmoja.

Agni-V limeundwa kwa teknolojia ya Multiple Independently Targetable Re-entry (MIRV). Ni nchi chache tu ulimwenguni ambazo zina teknolojia hii. Kombora moja linaweza kugonga shabaha nyingi kwa umbali mrefu.

Kwa mafanikio ya jaribio hili, Waziri Mkuu Narendra Modi aliwapongeza wanasayansi kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii.

"Wanasayansi wamefanikiwa kurusha kombora la Agni-V, ni jambo la kujivunia," Waziri Mkuu aliandika kwenye mtandao wa kijamii.

Pia unaweza kusoma

Teknolojia ya MIRV ni nini?

GHVC

Chanzo cha picha, ANI

Maelezo ya picha, Agni V

Kombora la Agni-V linaweza kushambulia kilomita elfu 5. Hii ina maana kwamba linaweza kuharibu shabaha kwa umbali wa kilomita elfu tano.

Agni-V ni muhimu kwa mahitaji ya usalama wa muda mrefu wa India, shirika la habari la PTI lilisema.

China Kaskazini, sehemu za Ulaya na Asia nzima zinaweza kufikiwa na kombora la Agni-V. Makombora ya Agni 1 hadi 4 yana uwezo wa kufika umbali wa kilomita 700 hadi 3500.

Tangu 1990, India imekuwa ikirusha makombora ya Agni na kuyaboresha mara kwa mara.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Teknolojia ya MIRV ilipatikana miaka 50 iliyopita, lakini ni nchi chache tu ambazo zimeweza kutumia teknolojia hiyo, imeripoti makala ya Indian Express.

Makala hiyo inasema kuwa Urusi, China, Marekani, Ufaransa na Uingereza ndio nchi pekee zilizo na teknolojia hii hadi sasa.

Agni-V pia inaweza kubeba silaha za nyuklia.

Pakistan pia inajaribu kutengeneza mfumo kama huo wa makombora. Kuna maswali ikiwa Israel ina mfumo kama huo au inajaribu kuwa nao.

Katika miaka ya 1970, Marekani ilipata teknolojia ya MRV. Umoja wa Soviet nayo iliipata teknolojia hiyo. Sasa India pia imepata nafasi ya kuwa nayo.

Agni-V imejaribiwa kwa ufanisi mara kadhaa tangu 2012, kulingana na makala ya The Indian Express. Kombora hili linaweza kurushwa kutoka barabarani au njia ya reli.

India ilitangaza 2007 kwamba itaunda kombora la Agni-V. Wanasayansi wanawake walihusika pakubwa katika mafanikio ya mradi wa Agni-V.

Hadi sasa Jeshi la Ulinzi la India lina Agni-1, Agni-2 (kilomita elfu 2), Agni-3 (kilomita 2500) na Agni-4 (kilomita 3500) ambayo inaweza kufikia malengo ya kilomita 700.

Lina faida gani kwa India?

yghbv

Chanzo cha picha, ANI

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu Modi na Rajnath Singh

Watafiti Joshua T. White na Kyle Deeming wanasema India inatazamia kupata manufaa fulani kwa teknolojia ya MIRV, kulingana na makala ya The Indian Express.

India ina makombora machache yenye uwezo kama makombora ya China. India inatumai kuwa Agni V itaongeza ushindani.

Lakini China iko mbele sana kuliko India kwa upande wa manowari zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia.

Christopher Cleary, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Albany, anaamini kombora la Agni-V lililotengenezwa kwa teknolojia ya MIRV litakuwa jibu kwa uwezo wa kijeshi wa Pakistan, kulingana na jarida la The Hindu Vartha.

Mtaalamu wa masuala ya kimataifa Brahma Chellani alichapisha maoni kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala hili na kusema:

"Uwezo wa nyuklia wa India umeongezeka kwa mafanikio ya uzinduzi wa Agni-V. Kwa upande mwingine pia litafanya kazi ya kuzuia makombora ya nchi nyingine.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah