Mashambulizi ya Israel huko Lebanon yana athari gani?

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Katika mitaa ya Beirut, mji mkuu wa Lebanon, watu wanatumia simu zao za mkononi na vifaa vingine kwa wasiwasi wakihofia shambulio jingine.
Lakini kuna tisho kubwa linalojitokeza katika eneo hilo - uwezekano wa vita vya muda mrefu kati ya Israel na Hezbollah ya Lebanon, na Iran inayouwaunga mkono.
Watu 37 waliuawa na wengine zaidi ya 2,600 kujeruhiwa baada ya maelfu ya vifaa vya mawasiliano vya pager kulipuka nchini Lebanon siku ya Jumanne, yakifuatiwa na mashambulio dhidi ya simu za upepo siku ya Jumatano, yote yakiwalenga wanachama wa Hezbollah.
Israel inashutumiwa kuhusika na mashambulizi hayo, ingawa haijathibitisha hilo, na siku ya Jumatano, waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Galant alitangaza "awamu mpya ya vita."
Haya ni yale yanayoweza kutokea nchini Lebanon:
1. Israel itaendelea na mashambulizi yake kwa matumaini ya kupata ushindi ''mkubwa", ikiamini kuwa Hezbollah imedhoofishwa.
Huku kukiwa na hofu ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, waziri wa afya wa Lebanon Firas Abiad anasema Lebanon inahitaji kujiandaa kwa hali mbaya zaidi, akielezea: "Nadhani tunahitaji kujiandaa kwa matukio mabaya zaidi. Mashambulizi mawili yaliyotokea katika siku mbili zilizopita yanaonyesha kuwa nia yao [ya Israeli] sio kufikia suluhisho la kidiplomasia."
"Ninachojua ni kwamba msimamo wa serikali yangu uko wazi. Tangu siku ya kwanza, tumeamini kuwa Lebanon haitaki vita," Al-Abyad aliongeza.
Mchambuzi wa masuala ya Kiarabu Ehud Yaari anasema mashambulizi hayo yalitengeneza "fursa ya kipekee" kwa Israel kuchukua hatua kali dhidi ya Hezbollah na maghala mengi ya silaha za makombora yanayoongozwa kulenga kwa usahihi vilishambuliwa, huku mifumo ya mawasiliano ya kundi hilo ikivurugwa na idadi kubwa ya makamanda wake wa kivita walijeruhiwa, baadhi yao wakiwa na majeraha makubwa.
"Hali hii ya sasa haitajirudia wakati wowote hivi karibuni," Yaari anaandika kwenye tovuti ya habari ya Israeli N12. Hezbollah kwa sasa iko katika hali mbaya zaidi tangu kumalizika kwa vita vya pili vya Lebanon mwaka 2006.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya ulinzi Paul Adams anasema vita vya Israel sasa vimebadili na mwelekeo wake kwa sasa ni vinaangazia eneo la kaskazini, huku vita vya Gaza vikiendelea.
Lakini bado haijafahamika ni vipi Israel inatarajia kutumia fursa hii adimu, na iwapo mzozo mpana unakaribia au la.
2. Hezbollah sasa inaweza kuishambulia Israel, na Israel inaweza kujibu kwa uvamizi wa ardhini Lebanon.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah alitoa hotuba yake kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni siku ya Alhamisi, akisema Israel imevuka mipaka yote, sheria na mistari nyekundu.
Nasrallah alikiri kuwa lilikuwa pigo kubwa kwa kundi hilo lenye silaha, lakini uwezo wake wa kuongoza na kuwasiliana ulibaki kuwa sawa, akiongeza kuwa uchunguzi umefunguliwa kuhusu jinsi tukio hilo lilivyotokea.
"Tunaweza kuyaita uhalifu wa kivita au tangazo la vita - chochote tunachochagua kuyaita, kinastahili. Hii ilikuwa nia ya adui," Nasrallah alisema.
Aliapa adhabu kuwa kutakuwa na adhabu ya haki dhidi ya Israel , lakini la kushangaza ni kwamba, hakutoa ishara ya jibu litakuwa ni lipi.
Ameongeza kuwa mashambulizi ya mpakani dhidi ya Israel yataendelea hadi pale ambapo kutakuwa na usitishaji mapigano Gaza, akisisitiza kuwa wakazi wa kaskazini mwa Israel ambao wameachwa bila makao kutokana na ghasia hizo hawataruhusiwa kurejea nyumbani.
Ameongeza kuwa mashambulizi ya mpakani dhidi ya Israel yataendelea hadi pale ambapo kutakuwa na usitishaji mapigano Gaza, akisisitiza kuwa wakazi wa kaskazini mwa Israel ambao wameachwa bila makao kutokana na ghasia hizo hawataruhusiwa kurejea nyumbani.
Amjad Iraqi, mshirika katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika taasisi ya Chatham House, anasema kuwa kupitia mashambulizi hayo, Israel ilituma "ishara za uchochezi" kwa Hezbollah jambo ambalo linaweza kuongeza uwezekano wa mgogoro wa kikanda katika eneo hilo.
"Hezbollah sasa inakabiliwa na shinikizo la kuongezeka kwa mzozo, jambo ambalo linaweza kulipatia jeshi la Israeli aina fulani ya kisingizio cha kuzindua kile kinachodaiwa kuwa uvamizi wa ardhini," Iraq aliiambia BBC, na kuongeza kuwa Israeli "haijafanikiwa kufikia malengo yake ya msingi huko Gaza", na hivyo dkuifanya serikali ya Israeli kuhisi kuwa lazima "ithibitishe dhana kwenye mpaka wa kaskazini na Hezbollah".
3. Mashambulizi yanaweza kuidhoofisha Hezbollah na kupunguza uwezekano wa mgogoro kuwa mdogo.
Mwandishi wa BBC Nafiseh Kohnavard yuko Beirut na aliifuatilia hotuba ya Hassan Nasrallah kutoka huko.
Anasema mashambulizi hayo yalikuwa pigo kubwa - huku Nasrallah akisema yalikuwa muhimu na kuyaelezea kama "mtihani mkubwa" ambao kundi hilo halijawahi kukabiliana nao hapo awali.
Aliongeza kuwa hii inaonyesha jinsi hali ilivyo ngumu kwa kundi hilo, kwani wengi wa waliojeruhiwa ni sehemu ya wasomi wapiganaji vijana, waliopewa mafunzo ya hali ya juu, na makabiliano ya kijeshi yanaendelea kati ya pande hizo mbili hadi leo.
Nafiseh anaeleza kuwa kilichotokea hakitalizuia kundi hilo kuchukua hatua zaidi, lakini mashambulio yamewaathiri.
Ikumbukwe kuwa Hezbollah ina washirika, na washirika hawa kwa mfano, Iran, vikundi vya kijeshi vya Kishia vya Iraq, na Wahouthi nchini Yemen wanasisitiza kwamba sio tu Hezbollah, bali Lebanon kwa ujumla ni mstari mwekundu.
Mwanajeshi mmoja hivi karibuni aliiambia BBC kwamba wanachama wao tayari wanaizunguka Lebanon na wana vitengo vinavyoisaidia Hezbollah. Kundi hilo limekuwa likipigana nchini Syria kwa miaka kadhaa sasa, na sasa Hezbollah inaweza kutegemea msaada wao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa ingawa mashambulizi nchini Lebanon yamekuwa na ufanisi, Hezbollah kama kundi linaungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.
4. Mashambulizi ya 'pager' nchini Lebanon hayakuwa sehemu ya mkakati mpana.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Gordon Corera anasema nadharia nyingine ni kwamba shirika la ujasusi la Mossad la Israel limeweza kupata uwezo wa kufikia vifaa vya mawasiliano vya pager vya Hezbollah iwapo kutakuwa na mzozo kamili nchini Lebanon.
Lakini Hezbollah ilikuwa na mashaka na vifaa hivyo , hivyo Mossad iliamua "kuvitumia au vinginevyo isingeweza kuvitumia tena ," na kuzilipua pager hizo iku ya Jumanne na kisha simu za upepo siku ya Jumatano.
Ikiwa hii ni kweli, haijulikani kabisa ikiwa kulikuwa na mpango mpana nyuma ya shambulio hilo, Corera anaongeza.
Amjad al-Iraqi wa Chatham House anasema kuwa mchakato wa kubadilisha pager na simu za hewa kuwa vifaa vya kulipuka umekuwa katika mipango kwa miezi, kama sio miaka, na kwa nini ilitokea sasa ni suala la tetesi zinazojadiliwa katika ripoti mbalimbali za habari.
"Baadhi ya taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa Hezbollah ilikuwa inafahamu ukweli kwamba vifaa hivi vinaweza kuwa vimefungwa kwa namna fulani," Al-Iraqi anasema. "Wengine wanasema kuwa kulikuwa na juhudi za kimkakati na za kuratibu, ikimaanisha kwamba huku Waisraeli walikuwa wakimaliza shughuli zao huko Gaza, wanajiandaa pia sasa na kusonga zaidi na zaidi kuelekea Lebanon."
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi












