Kwaheri
Asante sana kwa kufuatilia matangazo yetu ya moja kwa moja leo.
Unaweza pia kuendelea kuzisoma taarifa zetu kupitia Chaneli yetu ya WhatsApp kwa kubofya hapa.
Tukutane tena kesho panapo majaaliwa .

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah anasema kulipua vifaa vya mawasiliano ni "tangazo la vita" ambalo "halikuwa na tahadhari kwa watu wasio na hatia".
Na Ambia Hirsi,Yusuf Jumah & Dinah Gahamanyi
Asante sana kwa kufuatilia matangazo yetu ya moja kwa moja leo.
Unaweza pia kuendelea kuzisoma taarifa zetu kupitia Chaneli yetu ya WhatsApp kwa kubofya hapa.
Tukutane tena kesho panapo majaaliwa .

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wawili wameuawa karibu na mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon.
Wanaume hao wawili, wenye umri wa miaka 43 na 20, "waliangushwa wakiwa vitani ", imesema taarifa, na kuongeza kuwa waliuawa karibu na mpaka wa Lebanon.

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Gabon Ali Bongo ametangaza kujiondoa kwenye ulingo wa siasa mwaka mmoja baada ya kuondolewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi.
"Ningependa kuthibitisha kujiondoa kwangu kutoka kwa maisha ya kisiasa na kukataa kabisa azma yoyote ya kitaifa," Bw Bongo alisema katika barua aliyoandikia raia wa Gabon.
Ali Bingo mwenye umri wa miaka 65 pia alitoa wito wa kuachiwa kwa mkewe na mwanawe ambao wako kizuizini wakisubiri kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi.
Haijabainika ikiwa kauli hiyo inafuatia mazungumzo kati yake na utawala wa kijeshi, au ikiwa anatumai kwamba kwa kukubali kujiondoa kwenye siasa, atapata uhuru wa familia yake.
Bw Bongo alipatwa na kiharusi mwaka wa 2018 na hali ya afya yake ilitia ilizua hofu wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa urais wa 2023.
Jeshi lilichukua mamlaka Agosti mwaka jana, muda mfupi baada ya Bw Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo ambao ulipingwa na upinzani.
Alikuwa ameongoza nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta tangu 2009 alipomrithi babake ambaye alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40.
Familia hiyo ilikuwa na uhusiano wa karibu na Ufaransa, koloni la zamani la Gabon.
Maelezo zaidi:

Chanzo cha picha, Reuters
Israel imefanya shambulizi la hivi punde dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon.
Katika taarifa, Jeshi la Ulinzi la Israel linasema linafanya kazi ya "kusambaratisha" "uwezo na miundombinu ya kigaidi" ya Hezbollah.
"Kwa miongo kadhaa, Hezbollah imekuwa ikihifadhi silaha katika makazi ya raia, kuchimba handaki chini ya nyuma zao, na kutumia raia kama ngao za binadamu - na kugeuza kusini mwa Lebanon kuwa eneo la vita," taarifa hiyo ilisema.
Lengo lake, taarifa hiyo inasema, ni "kuleta usalama kaskazini mwa Israel ili kuwarejesha makwao wakazi waliotoroka na kufikia malengo ya vita".
Kanda zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mashambulizi ya anga yakiendelea katika baadhi ya maeneo ya Lebanon.
Maelezo zaidi:

Chanzo cha picha, Reuters
Sasa tunapata maelezo kutoka kwa hotuba ya kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.
Anaita mashambulizi yavifaa vya mawasiliano wiki hii "uhalifu wa kivita au angalau tamko la vita".
Anailaumu Israel kwa mashambulizi ya vifaa vya 'pager' na redio za mawasiliano -walkie-talkie, ambayo alisema haikuzingatia maisha ya watu wasio na hatia na maisha ya watoto. Takriban 'pagres' 4,000 zililengwa, anaongeza.
Baadhi ya waliouawa bado hawajajumuishwa katika takwimu rasmi, anasema.
Nasrallah anaishutumu Israel kwa kujaribu kuua watu 4,000 kwa wakati mmoja, na anasema shambulio la Jumatano pia lilikusudiwa kuwaua takriban elfu moja zaidi.
"Huu ni ugaidi mtupu. Tutayaita mauaji ya Jumanne na mauaji ya Jumatano. Huu ni uhalifu wa kivita au angalau kutangaza vita," anasema.
"Mungu ni wa rehema na alizuia vifo na majeruhi zaidi. Idadi kubwa vifaa hivyo havikuwa vikitumiwa au kuzimwa. Baadhi vilikuwa bado vimehifadhiwa'
Anasema katika siku mbili zilizopita, Israel ilijaribu kuua 5,000 katika dakika mbili, na kwamba milipuko hiyo haikuwa na kifani katika historia ya Lebanon na dunia.
Hakuna shaka "tumekiukwa", anasema.
Israel bado haijazungumzia moja kwa moja kuhusu mashambulizi hayo.
Nasrallah: 'Mapambano ya Lebanon hayatakoma kabla ya uvamizi Gaza kukoma'
Nasrallah sasa anazungumzia jinsi Hezbollah inakusudia kujibu.
"Kwa jina la wale wote ambao tumewapoteza kama mashahidi, ambao walijeruhiwa, kwa jina la wale wote ambao wamepigana kwa jina la Gaza, tunawaambia Netanyahu na Gallant, kwa adui, kwamba mstari wa Lebanon hautasimama kabla ya uvamizi huko Gaza kukoma," anasema.
"Upinzani nchini Lebanon hautaacha kuunga mkono watu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.
Waisraeli hawatarejea kaskazini hadi mapigano yaishe Gaza - Nasrallah
Nasrallah anageukia kiapo cha Israel cha kuwarejesha watu waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Hezbollah kaskazini mwa nchi hiyo.
Takriban watu 60,000 wamehamishwa kutoka kaskazini mwa Israel kwa sababu ya mashambulizi ya karibu kila siku ya Hezbollah katika nchi jirani ya Lebanon.
"Tunawaita walowezi na wavamizi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu," kiongozi wa Hezbollah anasema.
"Mmetupa changamoto, na tutaijibu changamoto hiyo. Ninawaambia Netanyahu na Gallant: hamtafikia lengo hili. Hamtaweza kuwarudisha watu hawa kaskazini. Njia pekee ya kufanya hivi ni kwa kukomesha uvamizi wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hii ndiyo njia pekee.
Adhabu na majibu yapo njiani-Kiongozi wa Hezbollah
Nasrallah sasa anasema mashambulizi yatakabiliwa na jibu "kwa njia ambayo wanaweza kutarajia na ambayo wanaweza kutotarajia".
"Sitazungumza juu ya mahali, wakati, eneo, maelezo," anaongeza.
"Mtajua itakapotokea. Adhabu hii itatokea. Maelezo, hatutafichua sasa, kwa sababu sasa tuko katika hatua nyeti sana ya vita."
Nasrallah anamaliza hotuba yake.
Maelezo zaidi:

Chanzo cha picha, Getty Images
Lebanon ikiendelea kukabiliana na hofu ya kulipuka kwa vifaa vingine vya kielektroniki, mamlaka zinajaribu kupunguza hatari hiyo.
"Vikosi maalum vya jeshi vinaharibu vifaa vya mawasiliano vinavyotiliwa shaka katika maeneo tofauti," jeshi limesema katika chapisho la mtandao wa X, zamani Twitter.
Ulipuzi uliyodhibitiwa kama pia ilifanyika usiku wa kuamkia jana, na jeshi linaendelea kuwahimiza raia waepuke maeneo ambayo milipuko inatokea na kutoa taarifa kuhusu "kifaa au kitu chochote kinachotiliwa shaka.
Wakati huo huo idadi ya watu walifariki katika milipuko ya kifaa vya mawasiliano nchini Lebanon siku ya Jumatano sasa imeongezeka na kufikia 25, waziri wa afya wa nchi hiyo anasema.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, Firass Abiad pia ametoa taarifa kuhusu idadi ya watu waliojeruhiwa katika milipuko hiyo ya Jumatano.
Takriban watu 608 wamejeruhiwa, anasema, idadi ambayo ni inazidi makadirio ya awali ya 450.
Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi yote mawili sasa imefikia 37, kwani takriban watu 12 waliuawa kutokana na milipiko ya siku ya Jumanne.
Na Carine Torbey
Akiripoti kutoka Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Hospitali ya Mount Lebanon ya Beirut

Onyo: Chapisho hili lina maelezo ya kuogofya
Daktari wa macho Prof Elias Warrak ananieleza jinsi kwa usiku mmoja alifanya upasuaji wa kung'oa macho zaidi ya aliyokuwa amewahi kufanya katika muda wote wa taaluma yake.
"Nilitaka kuokoa angalau jicho moja la waathiriwa (ili kuokoa macho yao) na wakati mwingine sikuweza, ilibidi nitoe macho yote mawili kwa sababu mabaki ya milipiko yalikuwa yameingia moja kwa moja kwenye macho."
Wakati akizungumza nami ofisini kwake Beirut, Dk Warrak anaonekana kuwa mtulivu i lakini pia mwenye huzuni sana, anapotafakari kile kilichotokea na kile alichokiona.
"Ilikuwa vigumu sana," anasema. "Wagonjwa wengi walikuwa vijana wa umri wa miaka ishirini na wakati mwingine ilibidi nitoe macho yote mawili. Katika maisha yangu yote sikuwa nimeona matukio yanayofanana na niliyoyaona jana."
Maelezo zaidi:

Chanzo cha picha, AFP
Zaidi ya watu 70 waliuawa na wengine takriban 200 kujeruhiwa kufuatia shambulizi la Jumanne katika mji mkuu wa Mali Bamako na wanamgambo wa kijihadi, AFP imebaini, ikinukuu vyanzo vya usalama.
Ufichuzi huo unakuja huku mamlaka ya Mali ikisita kutoa rasmi takwimu za majeruhi kutokana na shambulio hilo ambapo walidai kupoteza wanafunzi kadhaa.
Kundi la kijihadi lenye uhusiano na Al Qaeda JNIM lilidai kuhusika na shambulio hilo dhidi ya chuo cha gendarmerie na uwanja wa ndege wa kijeshi, kusababisha hasara kubwa ya binadamu na mali.
Mji mkuu wa Mali Bamako kwa kawaida huepushwa na mashambulizi, lakini tukio la mshangao la Jumanne linazua maswali kuhusu mkakati wa usalama wa jeshi.
Pia ilitilia shaka madai ya kiongozi wa mapinduzi Kanali Assimi Goita kwamba wanajihadi wamedhoofishwa.
Kufuatia shambulio hilo, mamlaka ya Mali ilisema mpango umeanzishwa ili kutoa msaada wa kisaikolojia kwa jinsia za wanafunzi, wafanyikazi, na familia za wahasiriwa.
Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS imelaani shambulio hilo la kijihadi, ikieleza wasiwasi wake kuhusu athari za matukio hayo kwa amani na usalama wa eneo zima la Afrika Magharibi.
Soma pia:

Chanzo cha picha, EPA
Waziri wa Afya wa Lebanon Firass Abiad ameiambia BBC kwamba anasema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni - ambapo vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa kundi la Hezbollah vililipuka - ni uhalifu wa kivita.
Mashambulizi hayo - ambayo yalisababisha vifo vya watu 32 wakiwemo watoto wawili - yamehusishwa na Israel, ambayo haijadai kuhusika.
Waziri huyo anasema Lebanon imeitisha mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo na inatumai kuwa na "majadiliano yenye tija kuhusu suala hilo".
Anasema "silaha za teknolojia" ni muhimu sana, sio tu kwa Lebanon lakini pia kwa ulimwengu mzima, na kwa migogoro mingine.
"Sasa tunapaswa kufikiria mara mbili kabla ya kutumia teknolojia," alisema.
Waliofariki na kujeruhiwa nchini Lebanon ni pamoja na wapiganaji wa Hezbollah - kundi la wapiganaji linaloungwa mkono na Iran ambalo limeorodheshwa kuwa la kigaidi na Uingereza na Marekani.
Lakini watu wa familia zao pia wameuawa au kujeruhiwa, pamoja na watu wasio na hatia.
"Dunia nzima inaweza kuona kwamba mashambulizi haya yalitokea sokoni," anasema.
"Hawa hawakuwa watu ambao walikuwa kwenye uwanja wa vita. Walikuwa katika maeneo ya raia pamoja na familia zao.”
Huku kukiwa na hofu ya vita kuzuka kati ya pande hizo mbili waziri huyo anasema Lebanon inahitaji kujiandaa kwa hali mbaya zaidi.
"Kwa hiyo, nadhani tunahitaji kujiandaa kwa hali mbaya zaidi," anasema.
"Mashambulizi mawili ya hivi punde, yanaonyesha kwamba dhamira yao (Israel) si kuelekea suluhu la kidiplomasia."
"Ninachojua ni msimamo wa serikali yangu uko wazi. Tangu siku ya kwanza, tunaamini kwamba Lebanon haitaki vita."
Maelezo zaidi:

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni ya kutengeneza ''walkie-talkie' ya Japan imejitenga na vifaa hivyo vya mawasiliano zenye nembo yake iliyolipuka nchini Lebanon, ikisema ilisitisha utengenezaji wake miaka kumi iliyopita.
Takriban watu 20 waliuawa na wengine 450 kujeruhiwa baada ya mamia ya mazungumzo, baadhi ya yakitumiwa na kundi lenye silaha la Hezbollah kulipuka kote Lebanon siku ya Jumatano.
Vifaa hivyo, kulingana na picha na video ya matokeo ya shambulio hilo, vinaonekana kuwa transceivers za IC-V82 zilizotengenezwa na Icom, mtengenezaji wa vifaa vya mawasiliano huko Osaka.
Lakini Icom inasema haijatoa au kusafirisha IC-V82, wala betri zinazohitajika kuziendesha, kwa miaka 10.
Hiyo ni kampuni ya pili ya bara la Asia kukumbwa na visa vya milipuko nchini Lebanon wiki hii, baada ya milipuko ya maelfu ya ''pager'' inayohusishwa na kampuni ya Taiwan ya Gold Apollo kuua takriban watu 12 na kujeruhi zaidi ya 2,000.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lililoandaliwa na Wapalestina na lisilofunga sheria na kuitaka Israel ikomeshe "uwepo wake kinyume cha sheria katika eneo linalokaliwa kimabavu la Palestina" ndani ya miezi 12.
Azimio hilo lilipigiwa kura 124 za kuunga mkono na 14 dhidi ya, ikiwa ni pamoja na Israel, 43 hawakupiga kura. Kama nchi isiyokuwa mwanachama, Palestina haikuweza kupiga kura.
Azimio hilo linatokana na maoni ya ushauri ya Julai kutoka kwa mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa ambayo ilisema Israel inakalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi,
Jerusalem Mashariki na Ukanda wa Gaza kinyume na sheria za kimataifa. Balozi wa Palestina aliita kura hiyo kuwa hatua ya mabadiliko "katika mapambano yetu ya uhuru na haki".
Lakini mwenzake wa Israel alikashifu hilo kama "ugaidi wa kidiplomasia".

Chanzo cha picha, EPA
Raia mmoja wa wa Israel amekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika njama ya Iran ya kumuua Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu, idara za usalama za Israel zimesema.
Polisi wa Israeli na ujasusi wa ndani walisema mtu huyo alisafirishwa kwa magendo mara mbili hadi Iran na kupokea malipo ya kutekeleza "misheni" hiyo.
Katika taarifa yao ya pamoja, walisema mshukiwa huyo alikuwa mfanyabiashara ambaye alikuwa akiishi Uturuki na alikuwa na washirika wa Uturuki ambao walimsaidia kuingia Iran.
Tangazo hilo linakuja wakati wa mvutano unaoongezeka kati ya Iran na Israel, maadui wa eneo hilo.

Chanzo cha picha, X
Shambulio la pili nchini Lebanon limesababisha vifaa vya mawasiliano vya mkononi au simu za hewa kulipuka. Jana majeruhi lebabon ilishuhudia idadi kubwa ya majeruhi na kuongezeka kwa hofu kwamba mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah utaongezeka.
Ufuatao ni muhtasari wa matukio ya kile kilichojiri kwa siku 2 za mashambulio:

Chanzo cha picha, EPA
Leo ni siku mbaya zaidi ya mauaji nchini Lebanon tangu kuanza kwa mapigano ya mpakani kati ya Hezbollah na Israel karibu mwaka mmoja uliopita, yaliyochochewa na vita vya Gaza.
Israel inaripotiwa kuwa sasa inapeleka vikosi vyake zaidi katika mpaka wa kaskazini na Lebanon. Katika matamshi yake jana usiku akitangaza "hatua mpya" ya vita, waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant alisema wanapeka wanajeshi kaskazini.
Eneo lote sasa litasikiliza kwa karibu hotuba ya mkuu wa Hezbollah Hassan Nasrallah, atakapokuwa akizungumza katika kwenye televisheni mchana huu, inayotarajiwa saa saa tisa adhuhuri
Kundi lake la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran limeumizwa na kudhalilishwa na mashambulizi ya ajabu katika mtandao wake wa mawasiliano na limeapa kutoa kile kilichotajwa kama "adhabu ya haki".

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanamuziki wa muziki wa hip-hop Sean "Diddy" Combs amenyimwa dhamana tena baada ya mawakili wake kubishana kwa mara ya pili kwamba anapaswa kuachiliwa kutoka kwenye hali "ya kutisha" ya jela wakati akisubiri kesi ya biashara ya ngono inayomkabili.
Jaji wa shirikisho mjini New York alimuweka rumande mwanamuziki huyo siku ya Jumanne baada ya waendesha mashtaka kudai kwamba kulikuwa na "hatari kubwa ya [mshukiwa] kutoroka".
Bw Combs, 54, alikamatwa wiki hii, akishutumiwa kwa kuendesha biashara ya uhalifu kuanzia mwaka 2008 iliyohusisha dawa za kulevya na unyanyasaji ili kuwalazimisha wanawake "kutimiza tamaa zake za ngono", kulingana na waendesha mashtaka.
Combs amekana mashtaka yote.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya uamuzi huo, wakili wa Bw Combs, Marc Agnifilo, aliwaambia waandishi wa habari kwamba uamuzi huo "haukuenda tunavyotaka," na kuongeza "mapambano yanaendelea".
Shtaka la kurasa 14 linamshtaki Bw Combs kwa ulaghai, biashara ya ngono kwa nguvu na usafiririshaji haramu wa watu ili kwa ajili ya kutumikishwa ukahaba.
Iwapo atapatikana na hatia ya makosa yote matatu, rapa huyo na mtayarishaji rekodi anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 hadi kifungo cha maisha jela.

Chanzo cha picha, Reuters
Watu 13 wamejeruhiwa katika eneo la Tver nchini Urusi baada ya shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani za Ukraine kusababisha moto mkubwa huko , wizara ya afya ya Urusi, imesema.
Picha ambazo hazijathibitishwa zimeibuka zinazodaiwa kuonyesha mlipuko mkubwa katika mji wa Toropets.
Kanda za video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha milipuko na moshi mkubwa angani.
Maafisa waliamuru watu kulihama eneo hilo baada ya shambulio hilo lililotokea a Jumatano asubuhi.
Gavana wa mkoa huo baadaye aliwahimiza wakazi kurejea, akisema kuwa miundombinu yote katika mji ilikuwa ikifanya kazi kama kawaida tena.
Mashirika ya habari ya AFP na Reuters yamenukuu vyanzo vya Ukraine vikisema bohari kubwa la risasi limepigwa na kombora lao.
Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty
Wadukuzi wa Iran walisambaza taarifa za udukuzi kuhusu kampeni ya uchaguzi ya Donald Trump kwa watu wanaohusika na kampeni ya Biden, kulingana na FBI na mashirika ya kijasusi ya Marekani.
Maafisa wa Marekani sasa wanaamini kwamba taarifa zilizochukuliwa kutoka kwa kampeni ya Trump zilitumwa kwa barua pepe kwa watu wanaohusika na kampeni mwishoni mwa mwezi Juni na mapema mwezi Julai kabla Biden hajajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais.
Kwa sasa hakuna ushahidi kwamba wavamizi hao walipokea jibu lolote kutoka kwa wapokeaji wowote wa taarifa hizo.
Mwezi Agosti, maafisa walitahadharisha kwamba Iran inatarajia "kuchochea mifarakano" na kudhoofisha imani kwa taasisi za Marekani kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba.
Maafisa wa Marekani walisema kuwa Iran imetumia "uhandisi wa kijamii na juhudi nyingine" kutafuta ufikiaji wa moja kwa moja kwa kampeni za Democrat na Republican, mbinu ambayo walisema imetumiwa na Iran na Urusi katika nchi nyingine ulimwenguni.
Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlipuko umesababisha hali ya machafuko katika eneo la Dahiyeh, ngome ya Hezbollah kusini mwa Beirut, wakati umati wa watu ulipokuwa umekusanyika kuwaomboleza baadhi ya watu waliouawa katika wimbi la mashambulio ya mabomu la Jumanne nchini humo.
Video iliyochukuliwa wakati wa mlipuko huo, ilionyesha mtu mmoja akiwa amelala chini huku watu wakiingiwa na hofu, wengine wakipiga kelele, wakikimbia.
Haya yote, yalitokea muda mfupi kabla ya mazishi ya mvulana wa miaka 11 na wanachama watatu wa Hezbollah waliuawa siku iliyotangulia kuanza.
Katika eneo jirani kulikuwa na mkanganyiko huku sauti za milipuko zikisikika mitaani. Nyimbo zilikoma. Wale waliokusanyika walitazamana kwa mshangao kwa kutoamini kinachotokea.
Baada ya ripoti kuenea kwamba mlipuko huo ulikuwa sehemu ya wimbi la pili la milipuko ambayo sasa inawalenga watu wanaoongea, hakuna vifaa vya kielektroniki vilivyochukuliwa kuwa salama.
Maafisa wa Lebanon walisema takriban watu 20 waliuawa na wengine 450 kujeruhiwa kote nchini, huku moto ukidaiwa kuzuka katika makumi ya nyumba, maduka na magari.
Tayari, mashambulizi ya hivi punde yanaonekana kuwa fedheha nyingine kwa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, na tanaonyesha dalili kwamba huenda mtandao wake wote wa mawasiliano unaweza kuwa umeingiliwa na Israel.
Unaweza pia kusoma: