Mambo matano kuhusu Gabon ambayo huenda huyajui

Chanzo cha picha, Getty Images
Siku moja baada ya wanajeshi wa Gabon kuupindua utawala wa Rais Ali Bongo matukio katika nchini hiyo ya Afrika Magharibi yamekuwa yakiwavutia wasomaji wapya.
Kwa hiyo, kwa wale wasioifahamu vyema nchi hiyo, hapa kuna mambo machache ambayo huenda huyajui kuhusu koloni la zamani la Ufaransa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali ambalo limekuwa likitawaliwa na familia ya Bongo baada ya uhuru.
1.''Emirati ndogo ya Afrika ya kati''
Ilipewa jina la "emirate ndogo ya Afrika ya kati" kwa sababu ya mafuta yake ambayo yaligunduliwa katika miaka ya 1970. Kwa idadi ndogo ya watu, hii imeruhusu tabaka la kati lenye nguvu kukua - na mafuta ni 60% ya mapato ya nchi.
2. Asilia 90 ya Gabon imefunikwa na msitu

Chanzo cha picha, Getty Images
Takriban 90% ya Gabon imefunikwa na msitu wa mvua wa kitropiki, ambao huchukua kaboni zaidi kuliko ile inayotolewa na nchi, na ambapo makundi makubwa ya tembo wa misitu, sokwe na wanyamapori wengi huishi.
3. Mwanamazingira wa Uingereza Lee White alikua waziri wa misitu
Mwanamazingira wa Uingereza Lee White alikua waziri wa misitu, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka wa 2019, akiongoza njia ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupokea malipo ya kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa kulinda misitu yake ya mvua.
4. Pierre - Emerick Aubameyang
Mchezaji kandanda Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ambaye sasa anaichezea Marseille, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Gabon. Ingawa alizaliwa nchini Ufaransa, baba yake ni raia wa Gabon na mchezaji wa zamani wa taifa hilo.
5. Rais Bongo alitaka kuwa mwimbaji wa pop enzi za ujana wake

Chanzo cha picha, Reuters
Rais Bongo alitaka kuwa mwimbaji wa pop enzi za ujana wake, alitoa albamu ya funk mwaka 1978 alipojulikana kwa jina la Alain Bongo. Hiki ni kiunga cha wimbo mmoja wa I Wanna Stay with You, ambamo anaimba: "Nilidhani kwamba ilikuwa vyema, kuvunja sheria zote."












