Majimbo saba yatakayoamua mshindi wa uchaguzi wa Marekani 2024

- Author, James FitzGerald
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 6
Takriban watu milioni 240 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu wa Marekani, lakini ni idadi ndogo tu kati yao ambayo huenda wakatatua swali la nani atakuwa rais.
Wataalamu wanaamini kuna majimbo machache tu ambayo yanaweza kushindwa na mgombea wa chama cha Democratic Kamalas Harris au Donald Trump wa Republican mtawalia.
Majimbo haya saba - Arizona, Georgia, Michigan, Nevada, North Carolina, Pennsylvania na Wisconsin - yanaweza kuuamua atakayepewa ufunguo wa Ikulu ya Marekani.
Katika miezi ya mwisho kuelekea uchaguzi, kambi zote mbili ziko mbioni kuwashawishi wapiga kura ambao hawajaamua katika majimbo haya.
Arizona
Chama cha Democratic kilishinda urais mwaka 2020 baada ya kuungwa mkono na Jimbo la Grand Canyon, ambalo lilipiga kura chache kumuunga mkono mgombea wa chama chao kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1990.
Jimbo hili linapakana na Mexico, na limekuwa kitovu cha mjadala wa uhamiaji wa taifa hilo.
Idadi ya wahamiaji wanaovuka mpaka na kuingia Marekani imeshuka katika miezi ya hivi karibuni na suala hilo limekuwa muhimu zaidi kwa wapiga kura.
Trump amekuwa akishambulia rekodi ya Bi Harris kuhusu uhamiaji, kwa sababu alipewa jukumu hilo na Rais Joe Biden katika juhudi za kupunguza mzozo wa mpakani.
Pia ameapa kutekeleza "operesheni kubwa zaidi ya kuwafukuza" wahamiaji katika historia ya Marekani ikiwa atachaguliwa tena kuwa rais.
Georgia
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Orodha yetu ya majimbo yenye ushindani mkali inalingana kwa karibu na orodha ya mahali ambapo maafisa wa Republican wanaoungwa mkono na Trump walijaribu kuzuia ushindi wa Bw Biden katika uchaguzi wa 2020.
Katika Kaunti ya Fulton ya Georgia, madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi yamemfanya Bw Trump afikishwe mahakamani katika mojawapo ya mashitaka manne ya jinai yaliyokuwa yanamkabili (Trump amehukumiwa katika kesi moja, huku iliyosalia ikiendelea).
Yeye na wengine 18 wanadaiwa kula njama ya kubadilisha ushindi wa Bw Biden katika jimbo hilo. Trump anakanusha madai hayo, na kesi hiyo inaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kusikilizwa kabla ya uchaguzi.
Theluthi moja ya wakazi wa Georgia ni Wamarekani wenye asili ya Kiafrika, mojawapo ya idadi kubwa zaidi ya wakazi weusi nchini humo, na inaaminika kuwa idadi hii ya watu ilimsaidia sana Bw Biden kushinda jimbo hilo mwaka wa 2020.
Kukata tamaa kwa Bw Biden kumeripotiwa miongoni mwa wapiga kura weusi wa Marekani, lakini kambi ya Harris inatarajia kuhuisha eneo bunge hili.

Chanzo cha picha, Reuters
Michigan
Jimbo hili la Maziwa Makuu limemchagua mgombea urais aliyeshinda katika chaguzi mbili zilizopita. Licha ya kumuunga mkono Bw Biden mnamo 2020, limeongoza kampeni ya kitaifa ya kumkosoa rais kwa kuunga mkono Israel katika vita vyake dhidi ya Gaza.
Wakati wa mchujo wa chama cha Democratic katika jimbo la Michigan mnamo Februari, zaidi ya wapiga kura 100,000 waliamua "kutoshiriki" kwenye kura zao, kama sehemu ya kampeni iliyoanzishwa na wanaharakati ambao wanataka serikali ya Marekani kusitisha msaada wake wa kijeshi kwa Israel.
Michigan ina idadi kubwa zaidi ya Wamarekani wenye asili ya Kiarabu- idadi ya watu ambao uungaji mkono wao kwa Bw Biden ulikuwa hatarini. Lakini Bi Harris ameikemea vika Israel, na baadhi ya waandamanaji wa Gaza wameiambia BBC wanatumai kuwa atawahurumia wenzao wa Gaza.
Akizungumzia matukio ya Mashariki ya Kati Trump ametoa wito kwa Israel kuendelea na kampeni yake dhidi ya Hamas huko Gaza, lakini "imalize kwa haraka".

Chanzo cha picha, Getty Images
Nevada
Jimbo hili limemuunga mkono mgombea wa chama cha Democratic katika chaguzi kadhaa zilizopita, lakini kuna uwezekano huenda wakazi wake wakampigia kura mgombea wa Republican katika uchaguzi huu ujao.
Kura ya maoni iliyochapishwa hivi karibuni na kampuni ya kufuatilia kura ya 538 inaonyesha kuwa Trump ana uungwaji mkono mkubwa dhidi ya Bw Biden, lakini idadi hiyo imepungua tangu Bi Harris kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho. Wafuasi wa chama cha Democratic walitarajia mgombea mwenye ushawishi mkubwa angeziba pengo hilo.
Wagombea wote wawili wanawania kushinda idadi kubwa ya watu wa jamii ya Ki tino katika jimbo hilo.
Licha ya kwamba uchumi wa Marekani umekua na kubuni nafasi za ajira tangu Bw Biden achukue urais, ahueni ya baada ya Covid imekuwa polepole huko Nevada kuliko mahali pengine.
Kwa asilimia 5.1, jimbo hilo lina kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira nchini, ikifuatiwa na California na Columbia, kulingana na takwimu za hivi punde za serikali ya Marekani.
Iwapo Trump ataingia madarakani tena, ameapa kurejelea ajenda yake ya kupunguza ushuru na kuondoa vikwazo.

Chanzo cha picha, Getty Images
North Carolina
Kinyang'anyiro katika Jimbo hili kimekuwa kikali baada ya Bi Harris kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Democratic, na baadhi ya wachambuzi wanasema mambo yanaweza "kugeuka" na yeyote anaweza kushinda.
Mtazamo huu huenda ulichangia uamuzi wa Trump kufanya mkutano wake wa kwanza tangu baada ya jaribio la kumuua la mwezi Julai.
"Jimbo hili ni jimbo kubwa sana kushinda," aliuambia umati.
Kwa upande wao, Wademokrat waliamua kutoa jukwaa kwa gavana wa jimbo hilo, Roy Cooper, usiku wa mwisho wa kongamano lao la kitaifa.
North Carolina inapakana na Georgia, na inashiriki baadhi ya masuala yake makuu ya uchaguzi, pamoja na yale ya Arizona, jimbo lingine lenye kinyang'anyiro kikali.
Trump alishinda jimbo la North Carolina mwaka wa 2020 lakini alifanya hivyo kwa zaidi ya kura 70,000, jambo ambalo limeongeza matumaini ya chama Democratic kwamba jimbo hili la "zambarau" linaweza kumuunga mkono mgombea wake katika uchaguzi wa mwaka huu.
Pennsylvania

Chanzo cha picha, EPA
Pande zote mbili pia zimekuwa zikifanya kampeni kwa uangalifu katika jimbo la Pennsylvania, ambako Donald Trump alinusurika katika jaribio la mauaji.
Uchumi ni suala kuu hapa, sawa na maeneo mengine mengi. Mfumko wa bei uliongezeka kote nchini chini ya utawala wa Biden, kabla ya hali hiyo kuimarika polepole.
Bei ya mboga imepanda kwa kasi zaidi katika jimbo hilo kuliko majimbo mengine yoyote, kulingana na Datasembly.
Hapo awali BBC iliripoti jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kustahimili hali katika Erie - na maeneo mengine ya Pennsylvania, ambapo mtu mmoja kati ya wanane wanakabiliwa na "uhaba wa chakula".
Mfumuko wa bei wa hali ya juu ni suala ambalo linaweza kumuathiri Bi Harris kote nchini Marekani kwani kura ya maoni inaonyesha kuwa inawapa wapiga kura mtazamo mbaya wa uchumi.
Trump anatumia suala hili kumshambulia kwa kumbana kwenye sera ya uchumi ya Biden.
Wisconsin

Chanzo cha picha, EPA
Jimbo hili pia lilichangia ushidi wa urais katika chaguzi za 2016 na 2020, kwa tofauti ya zaidi ya kura 20,000 kila mara.
Wataalamu wa mambo wamependekeza kuwa ni katika majimbo ya pembezoni kama hili ambapo athari inaweza kutolewa na wagombeaji wa vyama vya tatu ambao wanafanya kampeni dhidi ya sera za wagombeaji wakuu wawili.
Wafuasi wa chama cha Democratic wamekuwa wakipigania kuondolewa kwa mgombea wa chama cha Green Party Jill Stein, wakisema chama hicho hakikufuata sheria za uchaguzi za majimbo, na pia kimewasilisha malalamiko ya uchaguzi dhidi ya Cornel West, msomi anayeegemea mrengo wa kushoto.
Trump ameelezea hali hiyo kama "muhimu sana ... ikiwa tutashinda Wisconsin, tutashinda uchaguzi mzima". Kongamano la Kitaifa la Republican wakati wa kiangazi lilifanyika katika jiji la Milwaukee.
Bi Harris pia alikuwa akifanya kampeni katika jiji hilohilo wakati wajumbe katika kongamano la chama chake walipomteua rasmi kugombea.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo zaidi kuhusu uchaguzi wa Marekani:
- Muongozo: Yote unayostahili kujua kuhusu kura ya urais
- Uchambuzi: Wajue wagombea wa urais Marekani waliogombea wakiwa gerezani
- Maelezo: 'Je, ni Mwafrika au Mhindi?': Trump ahoji utambulisho wa rangi wa Harris
- Maelezo: Je, sera za Trump na Harris zitakuwaje kuhusu Mashariki ya Kati?
- Soma zaidi kuhusu: Kamala Harris | Donald Trump | Uchaguzi Marekani
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Seif Abdalla












