Kura za maoni za uchaguzi wa Marekani: Nani anaongoza - Harris au Trump?

Kamala Harri (kushoto) na Donald Trump.
    • Author, Na Visual Journalism pamoja na Data teams
    • Nafasi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Raia wa Marekani watapiga kura tarehe 5 Novemba kumchagua rais wao ajaye.

Awali uchaguzi huo ulikuwa wa marudio ya kinyang'anyiro cha 2020 lakini ulisitishwa mnamo Julai wakati Rais Joe Biden alipojiondoa kwenye kampeni na kumuidhinisha Makamu wa Rais Kamala Harris.

Swali kuu sasa ni - je, matokeo yatamaanisha muhula wa pili wa Donald Trump au rais wa kwanza mwanamke wa Marekani?

Siku ya uchaguzi inapokaribia, tutakuwa tukifuatilia kura za maoni na kutathmini athari ya matukio makubwa kama vile mjadala wa urais wa Jumanne yanavyokuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Ikulu ya Marekani.

Nani anaongoza kura za maoni kitaifa?

Miezi kadhaa kabla ya uamuzi wa Biden kujiondoa kwenye kinyang'anyiro, kura za maoni mara kwa mara zilionyesha akiwa nyuma ya rais wa zamani Donald Trump. Ingawa wakati huo ilikuwa kama kiashiria, kura nyingi za maoni zilipendekeza Harris hangefanya vyema.

Lakini kinyang'anyiro hicho kiliimarika baada yaHarris kuibuka kidedea kwenye kampeni na kupata uongozi mdogo dhidi ya mpinzani wake katika wastani wa kura za maoni za kitaifa ambazo amedumisha tangu wakati huo. Wastani wa hivi punde wa kitaifa wa kura za wagombea hao wawili umeonyeshwa katika jedwali zifuatazo.

Katika chati hizi za ufuatiliaji wa kura hapa chini, mwelekeo unaonyesha jinsi wastani huo umebadilika tangu Harris aingie kwenye kinyang'anyiro na nukta zinaonyesha kuenea kwa matokeo ya kura binafsi.

Harris alifikia 47% wakati wa kongamano la siku nne la chama chake huko Chicago, ambalo lilimalizika Agosti 22 kwa hotuba ya kuahidi "mwanzo mpya wa kusonga mbele" kwa Wamarekani wote. uungwaji mkono wake umesonga kidogo tu tangu wakati huo.

Wastani wa uungwaji mkono wa Trump pia umesalia kuwa thabiti, ukizunguka karibu 44%, na hakukuwa na ongezeko kubwa licha ya kuidhinishwa na Robert F Kennedy, ambaye alijiondoa kama mgombea huru mnamo Agosti 23.

Ingawa kura hizi za maoni za kitaifa ni mwongozo muhimu wa jinsi mgombeaji anavyojulikana kote nchini kwa ujumla, si lazima kuwa njia sahihi ya kutabiri matokeo ya uchaguzi.

Hii ni kwa sababu Marekani hutumia mfumo wa wajumbe maalum kumchagua rais wake, hivyo kushinda kura nyingi zaidi kunaweza kuwa na umuhimu mdogo kuliko pale watakaposhinda.

Kuna majimbo 50 nchini Marekani lakini kwa sababu wengi wao karibu kila mara hupigia kura chama kimoja, kwa kweli kuna majimbo machache ambapo wagombea wote wana nafasi ya kushinda. Haya ndiyo maeneo ambayo uchaguzi utashinda na kushindwa na yanajulikana kama majimbo yenye ushindani mkali.

Nani anashinda katika majimbo yenye ushindani mkali?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa sasa, kura za maoni zinaonyesha ushindani mkali katika majimbo saba, ambayo inafanya kuwa vigumu kujua ni nani hasa anaongoza kinyang'anyiro hicho. Kuna kura chache za kura za majimbo kuliko kura za kitaifa kwa hivyo tuna data ndogo na kila kura ina nakisi ambayo inamaanisha kuwa nambari zinaweza kuwa juu au chini.

Kama ilivyo, kura za maoni za hivi majuzi zinaonyesha kuwa wagombea hao wawili wamepishana kwa chini ya asilimia moja katika baadhi ya majimbo. Hiyo inajumuisha Pennsylvania, ambayo ni muhimu kwa kuwa ina idadi kubwa zaidi ya kura za wajumbe maalum ambao humuwezesha mshindi kufikia kura 270 zinazohitajika.

Majimbo ya Pennsylvania, Michigan na Wisconsin ambazo zimekuwa ngome za chama cha Democratic kabla ya Trump kuzigeuza kuwa nyekundu kwenye harakati zake za kushinda uchaguzi wa urais 2016. Biden aliyachukuwa tena mwaka wa 2020 na ikiwa Harris anaweza kufanya vivyo hivyo mwaka huu basi atakuwa na nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi.

Katika ishara ya jinsi kinyang'anyiro hicho kimebadilika tangu Harris awe mteule wa chama cha Democratic, siku ambayo Joe Biden alijiondoa katika kinyang'anyiro hicho alikuwa nyuma ya Trump kwa takriban asilimia tano kwa wastani katika majimbo haya saba yenye ushindani mkali.

Je, viwango hivi vya wastani vinaundwaje?

Takwimu ambazo tumetumia kwenye michoro iliyo hapo juu ni wastani iliyoundwa na tovuti ya uchanganuzi wa kura 538, ambayo ni sehemu ya mtandao wa habari wa Marekani wa ABC News.

Ili kuziunda, 538 hukusanya data kutoka kwa kura za maoni za watu binafsi zilizofanywa kitaifa na katika majimbo yenye ushindani mkali kupitia makampuni kadhaa yanayoandaa kura za maoni kura.

Kama sehemu ya udhibiti wao wa ubora, 538 inajumuisha tu kura kutoka kwa makampuni ambayo yanakidhi vigezo fulani, kama vile kuwa wazi kuhusu idadi ya watu waliopiga kura, wakati kura ilipopigwa na jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa (simu, ujumbe mfupi, mtandaoni, n.k. ).

Je, tunaweza kuamini kura za maoni?

Kwa sasa, kura za maoni zinaonyesha kuwa Kamala Harris na Donald Trump wana asilimia kadhaa ya alama sawia kitaifa na katika majimbo yenye ushindani mkali - na wakati wagombea wanapishana kwa alama chache, ni vigumu sana kutabiri mshindi.

Kura za maoni zilikadiria uungwaji mkono wa Trump katika 2016 na 2020. Kampuni zinazoendesha kura za maoni zitakuwa mbioni kujaribu kutatua tatizo hilo kwa njia kadhaa, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kufanya matokeo yao kuwa na nakisi ya idadi ya wapiga kura.

Marekebisho hayo ni magumu kupata haki na wapiga kura bado wanapaswa kufanya makadirio ya kina kuhusu vipengele vingine kama vile ni nani atakayejitokeza kupiga kura tarehe 5 Novemba.

Mchoro unaoonyesha rangi nyekundu ya chama cha Republican na bluu yanchama cha Democratic, ikiwa na nyota nyeupe kwa juu.

Maelezo zaidi kuhusu Uchaguzi wa Marekani

Imeandikwa na Mike Hills na Libby Rogers na kutafsiriwa na Ambia Hirsi.