Uchaguzi wa Kenya 2022: Washawishi wa mtandaoni wanaolipwa kusukuma 'hashtag'

Illustration showing hand holding strings acting as puppeteer over three mobile phones, which contain a person using a speaker phone to symbolise influencers. Surrounded by thumbs up emoji icons

Ushawishi katika mitandao ya kijamii unakuwa na ina nafasi ya kuwa biashara yenye kipato kikubwa kwa vijana nchini Kenya, huk uwanasiasa wakivutiwa na njia hii mpya ya kunadi sera zao.

"Wata watajua unaendesha hashtag, kila mtu kwenye Twitter anajua kwamba unalipwa kufanya hivyo kwa niaba ya mwanasiasa," anasema, mwandishi wa kujitegemea na anayetaka kuwa mshawishi kwenye mitandao ya kijamii kutoka Nairobi.

"Lakini wanasiasa hawatakubali hadharani kwamba wamelipa mshawishi kueneza ujumbe wa kampeni. Wanajaribu kufanya ionekane kama hawana uhusiano wowote nayo."

Huku uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali wa tarehe 9 Agosti, wengi wanahofia mfumo wa ushawishi wa kulipia unaweza kusababisha udanganyifu na kuenea kwa simulizi hatari.

Video zinazohoji uadilifu wa uchaguzi wa Kenya umeenea kwenye TikTok
Maelezo ya picha, Video zinazohoji uadilifu wa uchaguzi wa Kenya umeenea kwenye TikTok

Nick, ambaye yuko katikati miaka yake -20, alianza kufanya matangazo ya bidhaa mitandaoni kupata pesa wakati alipo kuwa mwanafunzi au kutafuta kazi.

Alipokuwa akipata wafuasi, makampuni ya kamari, vituo vya televisheni, watu wanaotaka kuzindua bidhaa walimwendea ili kuwatangaza kwenye Twitter. Pia alipewa kazi ya kisiasa, ambapo anaweza kupata 1000ksh (kama £7) kwa kazi ya saa chache - mshahara bora wa kila siku kuliko kazi nyingi za kawaida.

Nick anasema kuwa anapendelea kunadi bidhaa anazopenda, badala ya wanasiasa lakini anaweza kutuma ujumbe kwenye Twitter kumuunga mkono mgombea ambaye hatampigia kura.

th

"Binafsi mradi hawaendelezi chochote kibaya au cha vurugu au kikabila, sijali. Nani atakataa pesa za ziada?"

Hata hivyo, kwa vyama na wagombea ni biashara kubwa.

"Ni shughuli kubwa. Wakati wa msimu wa kisiasa mabilioni yanabadilishana mikono," anasema Gordon Opiyo, mshauri wa muda mrefu wa kisiasa, ambaye anafanya kazi na wateja wanaomuunga mkono naibu rais na mgombeaji William Ruto.

Gordon anasema kwa watu walioajiriwa na wateja kupanga kampeni, kazi ya kwanza ni kuajiri kundi la wale wanaoitwa microinfluencers - mtu yeyote aliye na wafuasi kati ya 10,000 na 500,000. Kisha wanaunda gumzo la kikundi na kuelezea mkakati, ambapo maagizo ya lebo ya hashtag, picha na sehemu za mazungumzo zitakazotumiwa husambazwa.

Gordon Opiyo

Chanzo cha picha, Gordon Opiyo

Maelezo ya picha, Gordon Opiyo amefanya kazi kama mshauri wa kisiasa kwa miaka kadhaa

Lengo ni kudhibiti masimulizi yanayomhusu mgombea au mada fulani, na kukwepa vyombo vya habari vya kawaida kwa kwenda moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii.

Watumiaji wanaofanya kazi katika vikundi vya hadi 200 mara nyingi hupata akaunti butu ili kukuza hashtag mahususi, ambayo huwa inatumika kuibua mada zinazogawanya zaidi.

Wataalamu wanasema kuwa karibu kila jaribio la kupata alama ya reli ya kisiasa huenda hulipwa.

"Ukiona yaliyomo kwenye hashtag, ujue mwisho wa mchezo ni kutengeneza mtindo wa wa hashtag," anasema Brian Obilo, ambaye ametafiti mitandao hii kwa niaba ya Wakfu wa Mozilla nchini Kenya.

"Wanaweza kudai kuwa vitambulisho vinatumika kuhamasisha wafuasi, lakini ukiangalia akaunti zinazoendesha lebo hizo, utaona akaunti zinahusika na kueneza taarifa potofu mtandaoni. Utajua kuna mtu anaifilisi."

Wanasiasa huwa wanajitenga kabisa na masuala hayo, Gordon anasema.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Raila Amollo Odinga

Muungano wa Azimio la Umoja

  • Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
  • Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
  • Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
  • Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
  • Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
  • Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
  • Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  • Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
  • Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

William Samoei Ruto

Muungano wa Kenya Kwanza

  • Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
  • Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
  • Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
  • Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
  • Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
  • Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
  • Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
  • Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
  • Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
  • Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC

George Wajackoyah

Chama cha Roots

  • Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
  • Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
  • Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
  • Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
  • Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
  • Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
  • Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
  • Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito

David Mwaure Waihiga

Chama cha Agano

  • David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
  • Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
  • Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
  • Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
  • Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
  • Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
  • Kupambana na ufisadi uliokithiri.
  • kuunda nafasi za ajira.
  • Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

"Wafadhili wakuu kwa kawaida hutengwa. Huwezi kamwe kuwafanya kuwa na mkataba wowote rasmi... kwa sababu wanajua kwamba ni eneo ambalo halijarasimishwa."

Kulingana ya Code for Africa's iLAB, timu inayoendesha ugunduzi wa mapema wa matamshi ya chuki na kuratibu kampeni za upotoshaji, lebo ya #RutoMalizaUfungwe ilikuwa nambari moja. Mwenendo kwenye Twitter baada ya kukuzwa na msingi wa akaunti mpya zinazoonekana kuwa feki.

Wengi wao walirejelea ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007, ambazo zilipelekea Bw Ruto kushtakiwa huko The Hague, na baadhi ya machapisho yalikuwa na matamshi ya chuki.

Image shows William Ruto removing a mask of the IEBC chairman. Labelled "no evidence"
Maelezo ya picha, Machapisho ya mitandao ya kijamii yamelishutumu baraza la kitaifa la uchaguzi kwa kumuunga mkono William Ruto

Sawa na miaka iliyopita kumekuwa na juhudi za kuhoji uadilifu wa Tume ya Uchaguzi.

Isaac anataka kujiunga na taaluma ya siasa. Amekuwa akipigia debe kampeni ya Bw Ruto na anasema amekuwa akilipwa kutuma jumbe 30 za Twitter 30 kwa siku.

Mwezi uliopita alisukuma hashtag akidai mkuu wa Tume ya Kitaifa la Uchaguzi hawezi kuaminiwa.

Mnamo Juni, Twitter ilifungia akaunti 41 zilizohusika katikaukuzaji wa hashtag hiyo na hiyo ikipendekeza Bw Wafula Chebukati, mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), alikuwa akimuunga mkono Bw Ruto, kwa kukiuka sera yake ya udukuzi na taarifa za upotoshaji.

Twitter iliiambia BBC kuwa inakataza "majaribio ya kutumia huduma zetu kuendesha au kuvuruga michakato ya kiraia, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa taarifa za uongo au za kupotosha kuhusu taratibu au mazingira yanayohusu ushiriki katika mchakato wa kiraia".

Hii ni sehemu ya kampeni pana ya kukashifu taasisi, ambayo imekuwa ikiongezeka, na imesababisha ghasia za uchaguzi siku za nyuma, anasema Mwanasiasa wa Code for Africa Allan Cheboi. Shirika hilo limeona juhudi za kukashifu IEBC kwenye TikTok na katika makala ambayo hayakujulikana ambayo yameenea kwenye WhatsApp.

Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Chagua suala ambalo linakuvutia

Sera za kila chama

  • Azimio La Umoja One Kenya Coalition

  • Roots Party of Kenya

  • Chama cha Agano

  • Kenya Kwanza Alliance

Mwongozo huu ni muhtasari wa sera kuu zinazotolewa na kila chama.

Pata maelezo zaidi kuhusu wagombea urais wa Kenya hapa

End of Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Kuunganishwa kwa uchumi wenye ushawishi na siasa kunaonekana kukua nchini Kenya. Wakala wa uuzaji wa ushawishi wa Twitter, ambaye anaonekana kutumia jukwaa lake kufanya kazi na kampeni za kisiasa, hakutaka kutoa maoni kuhusu kwa nini haijaorodhesha huduma hii kwenye tovuti yake.

Kufurika kwa mitandao ya kijamii yenye alama za reli ni moja tu ya mikakati inayotumiwa.

Abraham Mutai, mtaalamu wa mikakati wa kidijitali ambaye amewashauri wanasiasa kuhusu kushawishi miradi, anaamini kuwa mbinu mwafaka zaidi inahusisha kuwalipa washawishi wakuu wa kisiasa kuzungumza kuhusu mada fulani kwa muda wa wiki moja. Badala ya hashtag inayoshirikiwa kwa haraka na vidokezo vya kuzungumza vilivyoandikwa mapema, inaonekana halisi.

"Kwa wanasiasa, wanaona kuwa mazungumzo ya kikaboni yana nguvu kwa sababu yanaonekana kutolipwa…lakini kwa hakika yanalipwa. Yote ni kuhusu mtazamo," anasema Abraham, ambaye yuko kwenye kampeni na kambi ya Raila Odinga.

Pesa nyingi hufadhili shughuli hizi za mitandao ya kijamii. Kutoka kwa kazi tatu za kawaida kila mwezi, mshawishi mkuu (wafuasi wanaokaribia alama milioni moja) au mtaalamu wa mikakati anaweza kupokea ksh milioni tano (£ 35,000), ambayo pia inashirikiwa kati ya washawishi wadogo.

Madai kuhusu rais aliyepo madarakani Uhuru Kenyatta na kuwa mkuu wa IEBC pia zimesambazwa
Maelezo ya picha, Madai kuhusu rais aliyepo madarakani Uhuru Kenyatta na kuwa mkuu wa IEBC pia zimesambazwa

Lakini ingawa kuna pesa za kujipatia, baadhi ya washawishi hawafurahii waajiri wao.

"Tunaweza kusambaza taarifa za uongo kuhusu mwanasiasa fulani, na siku nyingine kuwasifu wapinzani wao. Inategemea nani analipa kazi hiyo," anasema Alex, si jina lake halisi, kupitia WhatsApp. Baada ya akaunti yake kuu kusimamishwa kwenye Twitter anahisi kuchanganyikiwa kwa kukosa kufanya kazi.

"Ni kama mti. Sisi ni majani tu. Kwa nini nasema hivi? Kwa sababu washawishi wanaweza kubadilishwa wakati wowote."

Kama Alex, Nick hana shauku juu ya safu hii ya kazi. Anasema kazi za kisiasa ni mbaya sana kwa sababu moja muhimu.

"Kuna nafasi kubwa kwamba hutalipwa. Sio sawa na kazi nyingine ya uuzaji," anasema. "Kwanza huamini kabisa unachofanya, unafanya kwa ajili ya pesa tu na pesa hizo zinaweza zisije. Binafsi mimi si shabiki wake."

.

Unaweza pia kusoma

,