Urusi na Ukraine: Cargo 200 -Tunachofahamu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine kufikia Juni

Kulingana na vyanzo huru vya BBC idhaa ya Kirusi , majina ya zaidi ya wanajeshi wa Urusi 3,500 waliokufa katika vita nchini Ukraine tayari yanafahamika . Sipo wote waliofariki wanaoripotiwa na maafisa nchini humo. Kila wiki tunapata Ushahidi mpya kuhusu mazishi wa wanajeshi katika makaburi mbali mbali katika miji ya Urusi, ambayo hayajaripotiwa.

Idhaa ya BBC Urusi huweka orodha ya waathiriwa wanajeshi wa Urusi wanaokufa nchini Ukraine kwa ushirikiano na Mediazona (''wakala wa kigeni wa habari'' wanaotambuliwa nchini Urusi ) na timu ya wahudumu wa kujitolea.

Kufikia tarehe 10 mwezi Juni, tuliweza kuthibitisha taarifa kuhusu vifo vya takriban wanajeshi 3,502 na maafisa.

Idadi hii haijumuishi wanajeshi wa Urusi waliopotea , kwani haiwezekani kubaini makadirio ya idadi yao, na wafu waliokuwa wamejiunga na majeshi ya kile kilichojitangazia kama jamuhuri ya Donbass kabla ya 24 Februari, 2022.

Taarifa tulizokusanya hazionyeshi kiwango sahihi cha wanajeshi waliouawa katika ripoti za wazi zilizothibitishwa. Lakini taarifa kwa ujumla zinaturuhusu kuelewa na kutathmnini kile kinachotokea kwa wanajeshi wa urusi wakati wa vita.

Majina mapya kutoka katika makaburi

Kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili zilizopita, BBc imeweza kubaini kuhusu makaburi mapya ya wanajeshi katika makaburi mbali mbali ya Khabarovsk, Voronezh na kijiji cha Borisovka karibu na Novorossiysk.

Katika kila eneo la makaburini , ilibainika kuwa mwanajeshi aliyezikwa alizikwa baada ya tarehe 24 februari. Picha za wanajeshi waliovalia magwanda ya jeshi zinaonekana zikiwa zimewekwa kwenye misalaba na mashada ya maua yaliyowekwa na Wizara ya ulinzi yamelazwa juu ya makaburi .

Baada ya kuanza kwa vita vya Ukraine tarehe 18 makaburi ya kijeshi yalionekana katika eneo la makaburi la Khabarovsk. Majina 15 kati yao (ambayo ni saw ana 80%) hayakuandikwa majina ya wazi n ahata hawakutajwa kwenye mitandao ya kijamii. Wakati huo huo, wanajeshi sita walifariki Machi, na wanne walifariki katika mwezi Aprili.

Kuna makaburi sita katika eneo la makaburi karibu na Novorossiysk, majina ya wanajeshi watano hayakuwa yametangazwa awali. Baada ya kuchunguza makaburi hayo katika Voronezh cemetery, iliwezekana kuyatambua majina matatu ya wanajeshi, ambayo awali hayakutangazwa wazi.

Kwa ujumla BBC, ilifuatilia hali katika makaburi 14 katika miji na vijiji vya Urusi katika kila moja ya makaburi ya wanajeshi hao ambao kifo chao hakikuripotiwa wazi.

Hivyo basi, tunaweza kufikiria kuwa orodha ya vifo vilivyothibitishwa ya BBC inaweza kuwana majina machache kwa 40-70% ya wafu ambao waliuliwa zaidi ya wale ambao walizikwa nchini Urusi.

Kulingana na ujasusi wa Uingereza, kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, Urusi ilikuwa imepoteza wanajeshi wapatao 15,000 nchini Ukraine. Kulingana na Mkuu wa majeshi wa Urusi, idadi ya vifo vya wanajeshi wa Urusi imezidini zaidi ya 30,000.

Wizara ya ulinzi ya Urusi mara ya mwiho iliripoti kuhusu vifo vya wanajeshi wake mwishoni mwa mwezi Machi. Tarehe 1 juni, mwenyekiti wa kamati ya taifa ya bunge ya masuala ya ulinzi alisema kwamba Urusi "iliacha kupoteza watu" katika Ukraine. Kwa mara ya kwanza, katika majimbo kadhaa ya Urusi, mazishi ya kijeshi yanafanyika kila siku.

Wanajeshi wa kujitolea wanaofariki

Kufikia tarehe 10 Juni, BBC ilibaini ripoti za vifo vya takriban Warusi 113, waliotajwa katika machapisho ya wapiganaji wa kujitolea. Hali za watu hawa huwa sio za wazi kila mara.

Baadhi yao walipigana katika Ukraine kama sehemu ya kuitenga Cossack , wengine waliingia katika mkataba wa muda mfupi wa vita na Wizra ya Ulinzi au ulinzi wa taifa (National Guard).

46% ya wanajeshi wa kujitolea ni watu wenye miaka zaidi ya 40, asilimia 20 walikwenda kupigana wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 50.

Wanaojitolea kujiunga na jeshi hupewa mafunzo kwa njia za kitamaduni zaidi. Kuna nafasi za kazi sasa za wanajeshi wa kujitolea zilizotangazwa kwenye wavuti wa Wizara ya ulinzi pekee. Katika 30% ya visa vingi, vituo vya kuwachagua kwa ajili ya kujiunga na jedshi viko katika miji ya Dagestan - Makhachkala, Khasavyurt, Kaspiysk, Derbent na Buynaksk. Huadiwa mshahara unaoanzia ruble elfu 300. Kwa majimbo mengi ya Urusi ambako hakuna ajira za kijamii, kuhudumia jeshi kwa mkataba ndio njia pekee ya kupata pesa.

Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi