Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
"Ninahitaji silaha , sio safari ," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Ijumaa, akikataa ofa ya usaidizi kutoka kwa Marekani ya kumuondosha Ukraine. Na ombi lake lilisikilizwa na jamii ya kimataifa.
Huku Urusi ikiivamia Ukraine, uvamizi ambao ulianza tarehe 24 Februari , nchi kadhaa zinaendelea kuiunga mkono kwa kutuma silaha kwa nchi hiyo, hatua ambayo haikuwahi kushuhudiwa kabla.
Ni nani ambaye ameamua kutuma usaidizi? Wameahidi kutuma kiwango gani? Na ni kwanini Ujerumani ilibadili msimamo wake
Katika idadi
Jumamosi, Marekani, Ujerumani , Australia na Uholanzi zilitangaza juhudi za kusafirisha kwa meli silaha kwa ajili ya kuisaidia Ukraine katika juhudi zake za vita dhidi ya Urusi.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani iliahidi kutuma silaha zenye thamani ya dola milioni 350 , ikiwemo mitambo aina ya Javelin ya kuzuwia makombora, mifumo ya kuzuwia mashambulio ya anga na fulana za kuzuwia risasi kupenya mwilini.
Kwa upande wake, serikali ya Ujerumani ilisema kuwa itaisambazia Ukraine zana 1,000 za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini na makombora 500 aina ya Stinger (yaliyotengenezwa kwa ajili ya kuyapatia majeshi ya ardhini njia ya kukabiliana na ndege na helikopta za mashambulizi zinazopaa kwa kimo cha chini) yatakayotumiwa wakati wa dharura.
Uholanzi ilitangaza kuwa itaitumia silaha aina ya 50 Panzerfaust-3 anti-tank na roketi 400.
Nchi hizo mbili zinaangalia uwezekano wa kutuma mfumo wa pamoja wa ulinzi wa mashambulio ya anga kikundi cha mapigano cha NATO kilichopo Slovakia.
Sweden, ambayo imekuwa ikifahamika kwa nafasi yake ya kutoegemia nchi yoyote na kuwa mpatanishi katika mizozo, pia imetangaza Jumapili hii kwamba itatuma msaada wa kijeshi kwa Ukraine, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya kitu kama hiki tangu mwaka 1939 wakati Muungano wa Usovieti ulipoivamia Finland.
Msaada huo unajumuisha kofia 5,000 aina ya helmeti, fulana za kuzuwia risasi 5,000 kuingia mwilini, na silaha 5,000 zinazoongozwa , pamoja na chakula kwa ajili ya wanajeshi 135,000, alisema Waziri mkuu Magdalena Andersson.
Kwa upande wake, Canada aliahidi kutuma kwa Ukraine msaada wa vifaa vya kijeshi visivyoua wa thamani yad ola milioni 19.6 (kofia za helmeti, fulana za kuzuwia risasi, barakoa za kujikinga na gesi na vifaa vya kusaidia kuona nyakati za usiku) ili kukamilisha mpango wake wa usambazaji wa kwanza ambao ilitangaza wa vifaa vya thamani yad ola milioni 5.5.
Rais wa Tume ya Muungano wa Ulaya, Ursula von der Leyen, alitangaza Jumamosi kwamba EU , kw amara ya kwanza katika historia , "itadhamini kifedha ununuzi na uwasilishaji wa silaha na vifaa vingine kwa nchi inayoshambuliwa ."
Wakati huo huo, NATO ilianza kupeleka vikosi vyake Ulaya Mashariki " kujibu haraka kwa dharura."
Hatimaye, Australia ilitangaza Jumapili kuwa itafadhili silaha kwa Ukraine kuisaidia kupambana na vikosi vya Urusi. Lakini hakutoa maelezo zaidi juu ya usaidizi huo.
Kubadilika kwa msimamo
Tangazo la Ujerumani la kutuma silaha kwa Ukraine ilifungua mabadiliko mapya katika sera yake ya kijeshi.
Hadi Jumamosi, Ujerumani, ilikuwa na msimamo wa muda mrefu wa kuzuwia usafirishaji wa silaha zinazoua katika maeneo ya mzozo.
Lakini hili limebadilika
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema kuwa Jumamosi kwamba uvamizi wa Urusi dhid ya Ukraine unafungua mabadiliko mapya.
" Uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine unaanzishwa mabadili ya enzi. Inatishia hali yetu yote baada ya vita. Katika hali hii, ni wajibu wetu kuisaidia Ukraine kwa kadri ya uwezo wetu katika kujilinda dhidi ya uvamizi wa jeshi la Vladimir Putin," Olaf Scholz, Waziri wa mambo ya nje alisema.
Serikali ya Muungano wa vyama vitatu ya Ujerumani, inayojumuisha Wasosholisti, Waliberali na chama cha kijani , inakabiliwa na changamoto ya kuwa na jibu la pamoja kuhusu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Lakini watu maarufu ambao wameelezea huruma kwa Moscow katika siku zilizopita wamekuwa kimya aukusema kuwa hawakuwa sahihi.
Wajerumani, wakati huo huo, walishitushwa na vitendo vya Rais Vladimir Putin nchini Ukraine na kutaka serikali yake ichukue hatua kali zaidi dhidi ya Kremlin.
"Dunia yetu ni tofauti baada ya viya ya Putin ya uchokozi. Hukutukishitushwa na ukiukaji huu wa sheria ya kimataifa ,hatujakosa nguvu," Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alituma ujumbe kwenye Twitter.
"Hiyo ndio maana tutawasaidia wanajeshi wa Ukraine wanaoigania nchi yao kwa silaha na kujikinga na mabomu na makombora ya Stinger ," aliongeza.
Unaweza pia kusoma:
Ujerumani ni mojawapo ya wazalishaji wakuu wanaoongoza katika wauzaji wa nje wa silaha duniani, huku mauzo yao yakiongezeka kwa 21% baina ya mwaka 2016 na 2020, kulingana na Taasisi ya kimataifa ya Stockholm ya utafiti wa amani - Stockholm International Peace Research Institute.
Wateja wake wakuu walikuwa ni Korea Kusini, Algeria na Misri Egypt , linaeleza shirika la habari la Ujerumani - Deutsche Welle. Ukraine pia hununua silaha kutoka Ujerumani.
Katika mwaka 2020 na ingawa nusu ya kwanza ya 2021, Ujerumani iliidhinisha mauzo 97 yenye thmanini ya jumla yad ola milioni 5.8, kulingana taarifa za serikali.