Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uvamizi wa Ukraine: Je Putin atafyatua kombora la nyuklia?
- Author, Steve Rosenberg
- Nafasi, BBC News, St Petersburg
Ngoja nianze kwa kukiri . Mara nyingi nimefikiri : "Putin hawezi kufanya hili." Halafu anaendelea na kulitekeleza. Nilifikiria
"Hangeweza kuitwaa Crimea, kusema kweli?" alifanyahivyo.
"Hangeweza kuzanzisha vita katika Donbas." Alifanya hivyo.
"hangeweza kuanzisha uvamizi kamili wa Ukraine ." Ameanzisha.
Nimehitimisha kwamba maneno "hawezi kufanya" sio ya Vladimir Putin.
Na hilo linaibua swali lisilopendeza:
"Hawezi kubonyeza mtambo wa nyuklia. Je Atafanya hivyo?"
Sio swali la kinadharia. Kiongozi huyu wa Urusi ameviweka kwenye tahadhari ''maalumu'', vikosi vyake vya nyuklia akilalamika kuhusu "taarifa za uchokozi" kuhusu Ukraine zinazotolewa na viongozi wa Nato.
Sikiliza kwa ukaribu kile ambacho Rais Putin amekuwa akijaribu kusema. Alhamisi iliyopita alipotangaza kwenye televisheni "operesheni yake maalumu " (katika uhalisia, uvamizi kamili wa Ukraine ), alitoa onyo kali: "kwa yeyote ambaye angekuwa na uwezekano wa kuingilia kutoka nje -kama ukifanya hivyo, utakabiliana na athari kubwa kuliko ambazo hakuna hata mmoja wenu amewahi kukabiliana nazo katika historia ."
"Maneno ya Putin yalisikika kama tisho la moja kwa moja la vita ya nyuklia ," anaamini mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dmitry Muratov, mhariri mkuu wa gazeti la Novaya Gazeta.
"Katika hotuba ile ya televisheni, Putin alikuwa hajifanyi kama Bwana wa Kremlin, bali kama Bwana wa sayari; kwa njia iliyo sawa na aitumiayo mmiliki wa gari la kifahari anavyotumia vidole vyake kubonyeza bonyeza mataa ya ufunguo wa gari lake, Putin alikuwa anachezesha mtambo wa nyuklia.
Amesema mara nyingi: Kama kungekuwa hakuna Urusi, ni kwanini tunahitaji sayari? Hakuna aliyejali kumsikiliza. Lakini hili ni tisho kwamba kama Urusi itatutendea vile inavyotaka ,hata kila kitu kitaangamizwa."
Katika Makala ya 2018, Rais Putin alisema kwamba "…kama mtu anaamua kuiangamiza Urusi, tuna haki ya kisheria ya kujibu. Ndio, litakuwa janga kwa binadamu na kwa dunia. Lakini mimi ni raia wa Urusi na mkuu wa taifa. Kwanini tunahitaji dunia bila Urusi ndani yake?"
Haraka na mapema mwaka 2022. Putin ameanzisha vita kamili dhidi ya Ukraine, lakini vikosi vya Ukraine vimeweka upinzani mgumu; mataifa ya Magharibi -kwa jambo ambalo halikutarajiwa na Kremlin- yameungana kuweka vikwazo vikali vya kiuchumi na kifedha dhidi ya Moscow. Uwepo halisi wa mfumo wa Putin huenda umewekwa mashakani
"Putin amebanwa," anaamini mchambuzi wa masuala ya ulinzi mwenye makao yake Moscow Pavel Felgenhauer.
"Hana njia nyingine iliyobakia, pale nchi za Magharibi zitakapofuja mali za Benki kuu ya Urusi na mfumo wa fedha wa Urusi kuporomoka kabisa .Hilo litaufanya mfumo mzima kutoweza kufanya kazi.
"Chaguo moja alilonalo ni kukata mifumo ya usambazaji wa gesi kwa Ulaya, akitumai kwamba hilo litayafanya mataifa ya Ulaya kuporomoka. Chaguo lingine alilonalo ni kulipua silaha ya nyuklia mahali fulani juu ya Bahari ya Kaskazini kati ya Uingereza na Denmark ili kuangalia ni nini kitakachotokea."
Iwapo Vladimir Putin atachagua chaguo la nyuklia, je kuna yeyote miongoni mwa watu wake wa karibu atakayejaribu kumwambia kuwa hilo halifai? Au kumzuwia?
"Wasomi wa Urusi kamwe hawako karibu na watu," anasema mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dmitry Muratov. "Mara kwa mara huwa wanakuwa upande wa mtawala."
Na katika Urusi ya Putin mtawala ndiye mwenye mamlaka ya kila kitu. Hii ni nchi yenye ufuatiliaji mdogi sana wa kile kinachofanywa na mtawala. Ni ofisi ya Waziri mkuu -Kremlin inayofanya kila kitu.
"Hakuna yeyote ambaye yuko tayari kumkosoa Putin," anasema Pavel Felgenhauer. "Tuko katika hali ya hatari."
Vita ya Ukraine ni vita ya Vladimir Putin. Kama kiongozi wa Kremlin atafanikiwa katika malengo yake ya vita, Ukraine kama taifa huru litakuwa mashakani. Kama ataonekana kushindwa na kupata majeruhi wengi, hofu ni kwamba hilo linaweza kuifanya Kremlin kutumia hatua za kukata tamaa. Hususan kama msemo "hawezi kufanya " hautazingatiwa tena.
Unaweza pia kusikiliza: