Nabii Muhammad: Putin atuma ujumbe kwa India baada ya kumtusi Mtume Mohammad

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mataifa ya kiarabu yamelaani vikali matamshi yenye utata yaliyotolewa na Msemaji wa zamani wa chama tawala nchini India BJP Nupur Sharma kumuhusu Mtume Muhammad, kulingana na mitandao ya kijamii , na Rais wa Urusi Vladimir Putin pia ameelezea kutofurahishwa kwake na matamshi yenye utata kumuhusu Mtume Mohammad katika serikali ya India.

Kauli za Putin zimesambazwa sana katika mitandao ya kijamii nchini India pamoja na nchi za Kiarabu kwa kipindi cha saa 24 zilizopita baada ya Putin aliyeishauri India wakati wa mkutano wake wa mwaka na waandishi wa habari, alisema, "Matusi dhidi ya Mtume Mohammad ni ukiukaji wa uhuru wa dini na kuwakashifu Waislamu. "

Kauli za Bw Putin zimesambazwa pakubwa katika mitanda ya kijamii hususan Twitter, ambapo zimeshirikishwa zaidi ya mara 50,000 nchini India na katika Ulimwengu wa Kiarabu.

Nini alichosema awali Putin kuhusu Uislamu na Mtume Muhammad.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, Rais wa Urusi Vladimir Putin, katika mkutano wake wa mwaka na waandishi wa habari Disemba 23 mwaka jana, alisema taarifa kuhusu kibonzo tata cha Charlie Hebdo nchini Ufaransa.

Alisema kuwa: "Sio sehemu ya sheri aya uhuru wa kuzungumza kwamba kila mmtu anafikiri anaweza kuelezea maoni yake vyovyote atakavyo."

"Matusi dhidi ya Mtume yanakiuka uhuru wa kuabudu na kukiuka hisia za Waislamu ," Putin alinukuliwa na Shirika la habari la Urusi TASS.

Rais Putin amesisitiza kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ulipizaji kisasi wa makundi yenye itikati kali kama vile shambulio dhidi ya ofisi za gazeti la Charlie Hebdo mjini Paris baada ya kuchapisha vibonzo vilivyodaiwa kumdhalilisha Mtume Mohammad.

Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

Aliwataka watu wa Urusi kuheshimu tamaduni na dini za kila mmoja wao, na kuongeza kuwa nchi yake ni "tofauti sana" na tofauti na maeneo mengine ya duniani.

Milki za Kiarabu (UAE), Oman, Indonesia, Iraq, Jordan, the Maldives, Bahraine, Libya na Bahrain ni miongoni mwa nchi zilizokokatika orodha ya Mataifa ya Kiarabu ambazo zimelaani kauli iliyotolewa na Msemaji wa zamani wa chama tawala cha India.

Mapema, taarifa hiyo ililaaniwa na Kuwait, Iran na Qatar na kuwaita mabalozi wa India kuelezea hasira yao. Saudi Arabia pia ililaani taarifa hiyo Jumatatu wiki hii.

Wanadiplomasia wa India wamejaribu kutuliza hasira ya matataifa haya ya Kiarabu, kwani wana mahusiano ya kirafiki ya muda mrefu nan chi hizi - lakini juhudi zao zimeishia patupu.

Nupur Sharma,ambaye ni Msemaji rasmi wa chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP), alitoa kauli hizo kwenye mdahalo wa televisheni, na afisa mkuu wa habari wa chama hicho Naveen Jindal, akatuma kauli hiyo kwenye mtandao wa Twitter.

Kauli hizi hususan za M Sharma - zimewaudhi hususan Waislamu ambao ni wachache nchini India, na kuibua maandamano katika maeneo mbali mbali katika baadhi ya majimbo.

Maafisa wawili walitoa taarifa ya kuomba msamaha na chama kikamsimamisha kazi kwa muda Sharmaa.