Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Picha za kughushi za utupu za maelfu ya wanawake zimesambazwa mitandaoni
Picha ghushi za utupu za zaidi ya wanawake 100,000 zimetengenezwa kutoka kutoka kwenye picha za mitandao ya kijamii kisha kuchapishwa mtandaoni, kutokana na ripoti mpya.
Nguo zinavuliwa kutoka kwenye picha za wanawake kwa kutumia teknolojia ya kidigitali, kisha kusambazwa kwenye app ya ujumbe ya Telegram.
Baadhi ya wanaolengwa ''walionekana kuwa na umri wa chini ya miaka 18'', ripoti ya kampuni ya intelijensia ya sensity imeeleza.
Lakini kwa wale wanaoendesha huduma hiyo wamesema kuwa ni ''burudani '' tu.
BBC imejaribu programu hiyo na kupata matokeo mabaya.
Sensity imedai kuwa teknolojia ya ''deepfake'' ilitumika.
Teknolojia hii ya kompyuta, moja ya matumizi yake ni kutengeneza video za uongo za watu maarufu.
Lakini Mtendaji Mkuu wa Sensity, Giorgio Patrini amesema kuwa mabadiliko ya kutumia picha za watu binafsi ni hatua mpya.
"Kuwa na akaunti ya mtandao wa kijamii na picha zinazoweza kufikiwa na Umma inatosha kabisa kwa mtu yeyote kulengwa," altahadharisha.
Akaunti ya Telegramu
Teknolojia hiyo huwa ndani ya mtandao binafsi wa ujumbe wa Telegramu. Watumiaji wanaweza kutuma picha ya mwanamke kwenye programu hiyo, kisha kidigitali itaivua picha hiyo nguo ndani ya dakika kadhaa bila gharama yoyote.
BBC ilijaribu picha kadhaa , zote kwa ridhaa ya wamiliki wa picha hizo na hakuna hata moja iliyokuwa na ukweli- matokeo yetu yalijumusha picha ya mwanamke aliyekuwa amevalia nguo juu ya kitovu
App ta kufanana na hiyo ilifungwa mwaka jana, lakini inaaminika kuna programu za namna nyingine.
Msimamizi anayeendesha huduma hiyo, anayejulikana tu kama "P" alisema: "Sijali hilo. Hii ni burudani ambayo haihusishi unyanyasaji.
"Hakuna mtu atakayemdhalilisha mtu yeyote na hii, kwa kuwa ubora huo sio wa kweli."
Alisema pia timu inaangalia picha gani zinazosambazwa, na "tunapoona watoto tunamzuia mtumiaji kabisa."
Lakini uamuzi wa kusambaza picha kwa wengine ni wa yeyote aliyetumia programu hiyo kuitengeneza, alisema.
Akitetea kiwango chake cha athari aliongeza: "Kuna vita, magonjwa, mambo mengi mabaya ambayo ni hatari ulimwenguni." Amedai pia hivi karibuni ataondoa picha zote.
Telegram haijazungumzia suala hilo.
Sensity iliripoti kuwa kati ya mwezi Julai mwaka 2019 na 2020, karibu wanawake 104,852 waamelengwa na picha zao zilisambazwa mitandaoni.
Uchunguzi wake ulibaini kuwa baadhi ya picha zilizosambazwa zilikuwa za wasichana wa chini ya miaka 18.
''Tovuti nyingi au app hazifanyi kazi hii kwa kificho kwa kuwa hakuna udhibiti ,'' amesema Patrini.
''Mpaka hali hiyo ikibadilika madhara makubwa yatakuwa yamejitokeza''.