Patrice Lumumba: Patrice Lumumba: Je jino lake litakaporudishwa Congo litafanywa nini?

gett

Chanzo cha picha, Getty Images

Ubelgiji itamrudishia rasmi Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, jino ambalo kamishna wa polisi wa Ubelgiji anadai ililitoa kwenye mwili wa Lumumba alipomsaidia kutoweka.

Baada ya kuahirishwa mara kadhaa kwa sababu za kama vile janga la Covid-19 na mipango ya makumbusho, urejeshaji wa jino sasa umepangwa Juni 20.

Watoto wa Lumumba watakuwa sehemu ya ujumbe wa Congo ambao utapokea mabaki hayo, kama sehemu ya hafla binafsi ya kifamilia kama walivyotaka, waziri mkuu wa Ubelgiji alisema katika taarifa yake.

Kwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Kongo, Catherine Katsungu Furaha, nchi hiyo ina wajibu wa kurejesha mabaki yamwili wa Patrice Emery Lumumba na kuzika katika ardhi ya Congo ili kuruhusu familia yake ya damu kumaliza maombolezo yaliyodumu kwa miongo kadhaa.

"Ni katika hali hiyo ambapo serikali ya DRC imeungana na familia hiyo ili kujibu ombi lao la kuwapa heshima inayostahili. Kama shujaa wa taifa anahitaji kutambuliwa hivyo", alisisitiza waziri wa utamaduni.

ddd

Chanzo cha picha, Getty Images

Tumefikaje hapa?

Ni kwa takriban miaka 30 ambapo familia ya Patrice Emery Lumumba ilisema iliwasilisha malalamishi dhidi ya Ubelgiji.

Patrice Emery Lumumba alikuwa raia wa kwanza wa Kongo kuteuliwa kuwa waziri mkuu baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.

Aliuawa Januari 1961, miezi kadhaa baada ya kupata uhuru wa taifa lake kutoka kwa ufalme wa kikoloni wa Ubelgiji. Mazingira ya kuuawa kwake hayajulikani hadi leo.

Mnamo 2001, Ubelgiji ilitambua "wajibu wake wa kimaadili" katika kifo cha Lumumba baada ya tume ya uchunguzi ya bunge.

Septemba 2020, mahakama ya Ubelgiji ilijibu ombi la familia ya Patrice Lumumba la kurudisha jino lililokamatwa nchini Ubelgiji.

Kwa François Lumumba, mtoto mkubwa wa waziri mkuu wa zamani, familia inataka zaidi. Kwa msaada wa mawakili wake, anaiomba serikali ya Ubelgiji kutoa maelezo ya kina kuhusu kifo cha baba yao na kurejesha nyaraka zote zinazohusiana na kifo chake.

"Maombolezo yetu hayataisha kwa kurejeshwa kwa mabaki ya baba yetu. Tunataka kujua ukweli wote kuhusu kifo chake na wahalifu ambao bado wako hai wanaadhibiwa," aliongeza.

ddd

Chanzo cha picha, Getty Images

Kumbukumbu ya Patrice Emery Lumumba (MPEL)

Mamlaka ya nchini humo imeunda kamati inayohusika na kutayarisha shughuli zinazohusiana na shirika la Patrice Emery Lumumba Memorial (MPEL) na Bw. Freddy Lokaso, mshauri wa Rais Félix Tshisekedi ndio mratibu.

Sherehe za kumuenzi Waziri Mkuu huyo wa zamani zitaanza nchini Ubelgiji Juni 21 na zitamalizika mjini Kinshasa Juni 29, baada ya kuzunguka nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Utamaduni na Sanaa Catherine Katsungu Furaha, mwili wake utapokea heshima za kijeshi, kabla ya kuzunguka nchi.

"Ziara hii itaanza katika ardhi yake ya asili kwa sababu familia yake bado iko katika maombolezo ili kuyamaliza. Mabaki hayo yatapita katika miji ya Lumumba-ville (katika jimbo la Sankuru, katikati mwa DRC), Kisangani (kaskazini). mashariki) na Shilatembo (Haut-Katanga, kusini-mashariki), kabla ya kuzikwa Kinshasa ambapo kaburi litajengwa," aliongeza.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa François Lumumba, mpango huu bado ni wa muda kwa sababu mazungumzo yanaendelea kati ya familia na kamati ya maandalizi, hasa kuhusu uchaguzi wa miji ya kutembelea au hata mahali pa kuzikwa.

Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani alibainisha kuwa gharama ya sherehe hii itajulikana mwishoni mwa mazungumzo na serikali.

Kwenye eneo la Limeté lililochaguliwa na serikali kwa mazishi yake, kazi ya ujenzi kwenye kaburi bado haijaanza. Lakini heshima za mwisho zitafanyika kuanzia Juni 21 hadi 29, kama alivyosema Bw. Bakupa Kanyinda mmoja wa wanaosimamia kamati.

Mwishoni mwa tafrija hiyo Bw.Balufu Bakupa-Kanyinda, msanii wa filamu kutoka Kongo, atatangaza utengenezaji wa filamu kuhusu mazishi na kurejeshwa kwa jino la Patrice Emery Lumumba.

Toleo la pili ni makala inayosimulia maisha ya waziri mkuu wa zamani kama alivyoonekana na Lumumba mwenyewe kupitia kumbukumbu, mashahidi, wataalam, waandishi wa wasifu ambao wamechambua kazi yake.