Marianna Vyshemirsky: 'Picha yangu ilitumiwa kueneza uvumi kuhusu vita vya Ukraine'

Marianna Vishegirskayaakisimama nje ya hospitali ya Uzazi iliyoshambuliwa kwa makombora mjini Mariupol, Ukraine, Jumatano, March 9, 2022. Vishegirskaya aliponea shambulio hilo na baadaye akajifungua mtowa kika katika hospitali nyingine ya Mariupol siku chache baadaye.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mshawishi wa ulimbende mtandaoni alituhumiwa kufanya maigizo baada ya picha yake kuchapishwa.

Picha ya mwanamke mjamzito akikimbia hospitali ya uzazi iliyoshambuliwa kwa bomu ilikuwa mojawapo ya picha iliyozua hisia kali kuhusu vita vita vya Ukraine. Lakini picha hiyo lililengwa na kampeni ya ajabu ya upotoshaji ya Urusi ambayo ilikosolewa vikali na pande zote.

Picha ya Marianna Vyshemirsky akiwa amejifunika duvet na paji lake la uso likitoka damu ilionekana kote duniani.

Ilikuwa imeandikwa picha unayoiona hapo juu ilipigwa baada ya shambulio la Urusi mjini Mariupol. Ilizagaa mitandaoni , kwenye kurasa za kwanza za magazeti na pia ilijadiliwa katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini bada ya kuponea shambulio hilo, Marianna anakabiliwa na shambulio lingine- la upotoshaji na chuki inayoelekezwa kwake na familia yake.

Huku Urusi ikijaribu kueneza taarifa za uwongo kuhusu shambulio hilo, Marianna mwenye umri wa miaka 29 alilaumiwa kimakosa kwa "kuigiza". Wanadiplmasia wa Urusi walidai kuwa "ameigiza" zaidi ya mara moja kama wanawake wawili tofauti.

Marianna akiwa kwenye simu ya video wakati wa mahojiano na BBC
Maelezo ya picha, Marianna akiwa kwenye simu ya video wakati wa mahojiano na BBC

Nimezungumza kwa kina na marafiki na jamaa zake, lakini nimekuwa nikijaribu kumhoji somo yangu kwa wiki kadhaa. Lakini hatimaye alipojitokeza kwa skrini ya simu ya simu, kidogo unahisi uzito wa jambo linalomkabili. Alisimulia BBC jisnsi alivyotoroka hospitali ya uzazi, na unyanyasaji wa mtandaoni uliofuatia tukio hilo.

"Nilipokea vitisho kwamba wananitafuta na wakinipata, wataniua, na mwanangu kukatwa vipande vipande,"anasema.

Haya ni mahojiano yake ya kwanza katika vyombo vikuu vya habari vya Magharibi baada ya kuokolewa na kupelekwa mji uliopo karibu ambao ni sehemu ya Donbas inayodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na ambao wanaungwa mkono na Urusi.

Marianna alikuwa ametulia, na hukutoa masharti yoyote wakati wa mahojiano yake na mwandishi wa BBBC lakini alikuwa na mwanabologu anayeunga mkono waasi hao wanaotaka kujitenga.

Alimuelezea mwandishi jinsi alivyojihisi baada ya kujipatata kati kati ya vita vya habari gushi - wakati akijifungua binti yake Veronika katika mazingira ya vita.

"Aliamua kujitokeza wakati mgumu," anaelezea, "lakini ni vyema alijitokeza katika mazingira hayo badala ya kukwepa kabisa."

'Mambo yalibadilika'

Maisha mjini Mariupol yalikuwa tofauti sana kabla ya kuzuka kwa vita. Marianna alikuwa akinadi bidhaa za urembo katika mitandao ya kijamii, naye mume wake Yuri alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha chuma cha Azovstal.

"Tuliishi maisha ya kawaida," anasema, "lakini, ndio hivyo tena mambo yalibadilika."

Akaunti yake ya Instagram inaonyesha jinsi alivyotazamia kwa furaha kuwa mama.

Marianna aliweka picha kwenye Instagram mwishoni mwa Februari, akiwaomba mashabiki wake kubashiri ikiwa mtoto wake ni wa kiume ama wa kike.

Chanzo cha picha, Instagram

Maelezo ya picha, Marianna aliweka picha kwenye Instagram mwishoni mwa Februari, akiwaomba mashabiki wake kubashiri ikiwa mtoto wake ni wa kiume ama wa kike.

Lakini wakati Marianna alipolazwa hospitali, Mariupol ilikuwa mji ambao umeshambuliwa zaidi kwa mabomu nchini Ukraine.

Mnamo Machi 9, alikuwa akizungumza na wanawake wengine wakati mlipuko ulipotikisa hospitali hiyo.

Alijifunika blanketi kichwani. Mara mlipuko wa pili ukatokea tena.

"Ungelisikia jinsi vitu vilivyotawanyika kila mahali, vingine vilikuwa silaha butu," anasema. "Mlio wa king'ora ulikuwa kwenye masikio yangu kwa muda mrefu."

Wanawake walipewa hifadhi pamoja na raia wengine katika vyumba vya chini ya ardhi. Marianna alijeruhiwa usoni na vigae vya kio vilikuwa vimekwama kwenye ngozi yake, lakini daktari alimwambia hahitaji kushonwa.

Kitu ambacho alihitaji, ilikuwa kuchukua vitu vyake kutoka kwa vifusi vya hospitali hiyo. Alimuomba afisa wa polisji kusaidia.

"Kila kitu nilichokuwa nimemnunulia mwanangu kilibaki kwenye wodi ya uzazi," anasema.

Mwelekeo wa uwongo

Alipokuwa amesimama nje ya hospitali, kusubiri kuchukua vitu vyake, alipigwa picha na wanahabari wa Associated Press. walimpiga picha tena alipokuwa akishuka ngazi kutoka kwenye jengo hilo.

An injured pregnant woman walks downstairs in a maternity hospital damaged by shelling in Mariupol, Ukraine, Wednesday, March 9, 2022

Chanzo cha picha, AP

Picha hizo kwa haraka zilisabaa mitandaoni. Na hapo ndipo madai ya uwongo kwamba picha hizo zilikuwa za "kuigizwa" zilianza kuonekana katika chaneli ya Telegram ambayo inaunga mkono-Kremlin. Blogu Blogu ya Marianna inayoangazia masuala ya urembo ilitumiwa kuashiria kwamba alikuwa "muigizaji" ambaye alitumia alikuwa ametumia vipodozi kutengeneza majeraha bandia.

Uongo huu ulirudiwa na kukuzwa na maafisa wakuu wa Urusi na vyombo vya habari vya serikali.

Pia walidai picha ya mwanamke mwingine mjamzito kwenye machela alikuwa Marianna, ingawa ni wazi kuwa picha hizo ni za watu tofauti. Mwanamke aliyekuwa kwenye machela na mwanawe ambaye alikuwa hajazaliwa alifariki kutokana na majeraha aliyopat akatika mashambulio hayo.

This tweet from the Russian Embassy in London containing false information was taken down by Twitter

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, This tweet from the Russian Embassy in London containing false information was taken down by Twitter

Kutoroka mashambulio bila uwezo wa kufikia mtandao wa intaneti, Marianna hakuziona picha hizo hadi siku kadhaa baadaye.

Kufikia wakati huo, Instagram yake ilijaa jumbe za shutuma na vitisho. Alijipata akishambuliwa mtandaoni kwa tuhuma za uwongo..

"Nilisikitika sana kwasababu nilishuhudia kila kitu kiuhalisia," alisema. Lakini alijizuia ukosoaji wa moja kwa moja wa maafisa wa Urusiambao walieneza taarifa ghushi kumhusu.

Badala yake alikosoa shirika la habari la Associated Press.

"Nilichukizwa kwamba waandishi wa habari ambao walikuwa wamechapisha picha zangu kwenye mitandao ya kijamii hawakuwa na mahojiano na wanawake wengine wajawazito ambao wanaweza kuthibitisha kwamba shambulio hili kweli lilifanyika."

Anasema hatua hiyo ingesaidia kuelezea watu walioshawishika kwamba ni "maigizo". Lakini kwa mujibu wa Marianna yeye alikuwa miongozi wa wagonjwa wa mwisho kuondolewa katika hospitali hiyo, na wakati huo ndipo waandishi wa habari wa AP walipofika eneo la tukio. Wanahabari hao walihoji watu wengine waliokuwepo mahala hapo. Na hawakuhusika kwa vyovyote na taarifa ya uwongo iliyosambazwa baadaye na maafisa wa Urusi. BBC iliwasiliana na AP kupata kauli yake.

Kumtafuta Marianna

Siku kadhaa baada ya shambulio hilo, Marianna alijifungua mtoto Veronika katika hospitali nchingine.

Marianna katika hospitali nyingine akiwa na mwanawe mchanga, siku chache baada ya shambulio la bomu mjini Mariopol

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Marianna katika hospitali nyingine akiwa na mwanawe mchanga, siku chache baada ya shambulio la bomu mjini Mariopol

Sawa na maelfu ya wengine, Marianna na Yuri walikuwa wakijizatiti kutoroka mjini Mariupol. Kwa wiki kadhaa, Na ilikuwa vigumu kuwasiliana nao. Baadaye jamaa za Marianna waliambia BBC kwamba wanandoa hao walikuwa wameondoka mji huo na hawakuwa na uhakika wamekimbilia wapi. Kisha mwanzoni mwa April, wakaibuka tena katika eneo la Donbas.

Alifany amahojiano na Denis Seleznev, mwanablogu ambaye ni mfuasi wa waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Kulikuwa na uvumi uliohoji ikiwa alikuwa huru kusema alichotaka

Marianna alimwambia mwandishi wa BBC: "Ilinibidi nisimulie kila kitu kilichotokea, kama nilivyoshuhudia kwa macho yangu."

Katika mahojiano yetu naye yaliyowezeshwa kupitia Denis. Marianna anazungumzia kisa hicho kutoka nyumbani. Alikuwa naye wakati wa mahojiano hayo lakini hakuingilia kati. Jamaa wa Marianna na marafiki zake wametuhakikishi akwamba sasa yuko salma.

line

Vita vya Ukraine: Maelezo zaidi

line

Kuweka pamoja ukweli

Mengi ya yale anayosema katika mahojiano yake na BBC yanadhoofisha upotovu wa serikali ya Urusi.

Kremlin ilipendekeza kimakosa na mara kwa mara hospitali iliyoshambuliwa kuwa hospitali namba moja ya Mariupol, na kwamba ilikuwa haifanyi kazi tena.

Lakini kitengo cha habari cha BBC kiligundua hospitali ambayo Marianna alikuwa - ni hospitali nambari tatu.

map of hospitals in Mariupol

Tuliwasiliana na Ubalozi wa Urusi huko London kwa maoni.

Marianna anathibitisha kwamba hospitali hiyo ilikuwa ikimtibu yeye na wagonjwa wengine - kinyume na madai ya Urusi kwamba haikuwa ikifanya kazi kama kituo cha afya.

Urusi pia ilidai kuwa hospitali hiyo ilikuwa imetekwa na kikosi cha Azov - kikundi chenye utata cha kitaifa cha Ukraine ambacho kimehusishwa na Wanazi mamboleo, madai ambayo wao wenyewe wanayakanusha.