Mzozo wa Ukraine: Jinsi mikakati ya Urusi ilivyobadilika katika awamu ya pili ya vita

wanajeshi wa Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Uu usi

Tarehe 19 vita vya Ukraine vilichukuwa mkondo muhimu sana.

Baada ya awamu ya kwanza ambapo vikosi vya Urusi vilishambulia miji ya Ukraine kwa pamoja , juhudi zilizofanywa na rais Vladmir Putin zilielekezwa hususan eneo la jimbo la mashariki la Donbas , ambapo analenga kuteka eneo kubwa zaidi kwa madai ya kuwalinda raia wanaounga mkono Urusi.

Mabadiliko ya kieneo ambayo yaliandamana na mkakati mpya wa kijeshi yalitekelezwa na jeshi vamizi.

Iwapo awamu ya kwanza ya mkakati huo ulishirikisha majaribio ya kuivamia kwa haraka kupitia urushaji wa mabomu , na ufyatuaji wa makombora pomoja na msafara mrefu wa magari ya kijeshi kama ulivyoshindwa mjini Kiev, mkakati wa pili unashirikisha uvamizi wa hali ya juu.

"Uvamizi huo unafanyika kwa kasi ya chini ukiwa na lengo sio tu kuteka , lakini pia kudhibiti maeneo yaliotekwa mbali na kupunguza hasara'' , anasema Mathieu Boulegue, mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa Urusi katika taasisi ya Chatham House mjini London, kwa mujibu wa BBCMUndo.

Mkakati mpya ambao kulingana na makabiliano ya wanajeshi wa Ukraine huenda ukasababisha vita hivyo kuchukua muda mrefu zaidi ya ilivyotarajiwa.

Baada ya kuivamia Ukraine kwa kasi ya Juu sasa Urusi imebadilisha mbinu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya kuivamia Ukraine kwa kasi ya Juu sasa Urusi imebadilisha mbinu

Lengo moja lakini mbinu tofauti

''Kulingana na Urusi, lengo la vita hivyo halijabadilika : Kuharibu na kuiwake huru Ukraine'', Boulegue anasema.

''Kuteka maeneo mengi zaidi , kuyadhibiti na kushawishi uamuzi wa kisiasa wa siku zijazo'', anaongezea mtaalamu.

Lakini mbinu hizo za Urusi hazijazaa matunda kama ilivyotaraji .

Ukraine ilijibu kwa njia ambayo haikudhaniwa na Urusi, kulingana na wataalam kuhusu suala hilo. Msafara wa magari ya kijeshi ambao ulitishia mji mkuu wa Kyiv kwa wiki kadhaa ulilazimika kuondoka na kujipanga upya.

Hakuna hata mji mmoja wa Ukraine uliotekwa na Urusi isipokuwa mji wa Kherson . Urusi iliathirika pakubwa kijeshi kama ilivyokiri kremlin.

''Katika awamu ya kwanza Urusi iliingia kwa fujo, na kuanzisha vita katika maeneo matano bila kutumia makombora yao vyema'', Lawrence Freedman profesa wa vita katika chuo kikuu cha Kings College London alielezea BBCMundo.

Msafara wa magari ya kijeshi ya Urusi vita vilipoanza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Msafara wa magari ya kijeshi ya Urusi vita vilipoanza

Msomi huyo anaorodhesha makosa kadhaa yaliofanywa na Urusi : Walishindwa katika jaribio lao la kuonesha ubabe wao wa angani. Walitaka kuuteka mji wa Kyiv kwa haraka, huku raia wengi wa Ukraine ndani ya mji huo wakiwakabili. Matokeo yake yalikuwa tatizo la kimkakati na vifaru vilivyowachwa nyuma kwa hofu ya mashambulizi ya kushtukiza.

Ulikuwa mpango ulioambuliwa patupu, alitamatisha.

Hiyo ndio sababu Urusi imekuwa ikifanya mashambulizi yake kwa uangalifu mkubwa.Kuchukua hatua moja baada ya nyengine . Hakuna haja ya kutekeleza mashambulizi kutoka maeneo mengi tofauti.

Je Urusi inatumia mbinu gani hivi sasa?

Wataalamu wanakubaliana katika kuelezea mbinu mpya ya Urusi kama njia ya kizamani.

"Tunaielezea kama mbinu ya utekaji na kudhibiti maeneo yaliotekwa, na uvamizi wa kasi ya chini . Walianza kwa mashambulizi ya mizinga ya masafa marefu hadi kulazimika kuwasukuma wanajeshi wa Ukraine kutoka ardhini kwa ufupi," says Boulegue.

''Waliyatambua maeneo ya kushambulia, wakatumia makombora ya masafa marefu, na baadaye wakawasukuma wanajeshi wa Ukraine kwa vifaru na baadaye wakajiandaa kujlinda maeneo walioyateka'', Freedman adds.

Kwa mtazamo wa kijeshi na wa kimantiki, mkakati huu una maana zaidi kulingana na wataalam na, kama ungetumika tangu mwanzo, pengine Urusi ingekuwa na mafanikio zaidi katika malengo yake kwenye uwanja wa vita, wanasisitiza.

Ukweli ni kwamba BBC Urusi inasema kwamba mkakati huo mpya wa Urusi unapiga hatua katika jimbo la Donbas na pia unapunguza hasara iliopatikana katika awamu ya kwanza , ijapokuwa kwa wataalamu huenda Urusi imechelewa.