Uchaguzi Kenya 2022: Mfahamu Naibu rais mteule Mathira Rigathi Gachagua

Chanzo cha picha, Twitter/Rigathi Gachagua
William Samoei Ruto, wakati wa kuelekea kuanza kampeni alimtangaza mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua kuwa mgombea wake mwenza katika uchaguzi wa 2022.
Jina la Gachagua kama mtu aliyemsaidia William Ruto , katika uchaguzi , linamaliza uvumi ambao umekuwepo kwa muda mrefu miongoni mwa Wakenya.
Dkt Ruto alisema kuwa Kenya Kwanza ilioanisha ajenda ya vyama tofauti ili kuafiki mpango wa kiuchumi wa Kenya Kwanza baada ya mkutano wa saa 17.
Bw Gachagua kama mtu anayechukua nafasi ya Dkt Ruto, kunahitimisha mchezo wa kubahatisha ambao umedumu kwa miezi kadhaa.
Waliokuwa wakiwaniwa kuwa mgombea mwenza wa Kenya Kwanza ni Ndindi Nyoro, Wahome Alice, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, na Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru.
Ruto hakuwa na shaka kumtangaza bwana Gachagua, wabunge wengi wa eneo la mlima kenya walikuwa wakimpigia debe Profesa kindiki. Pia kulikuwa na viongozi mbadala walioteuliwa ili kupunguza joto hilo la kisiasa.
Lakini Je Rigathi Gachagua ni nani?

Chanzo cha picha, Twitter/Rigathi Gachagua
Rigathi Gachagua alizaliwa mwaka 1965 na ni ndugu ya aliyekuwa gavana wa Nyeri Nderitu Gachagua.
Kiongozi huyo alisomea katika shule ya msingi ya Kibiruini kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Kianyaga School.
Anamiliki shahada ya Sanaa na ile ya sayansi ya kisiasa Pamoja na ile ya fasihi kutoka chuo kikuu cha Nairobi ambapo alisoma kati ya mwaka 1985 hadi 1988.
Baada ya kumaliza chuo kikuu alijiunga na taasisi ya mafunzo ya polisi 1990.
Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma
UNAYOFAA KUJUA:Uchaguzi Kenya 2022: Je Naibu wa rais wa Kenya William Ruto anakabiliwa na changamoto gani katika kumteua naibu wake wa rais?
Alifanya kozi ya Utawala wa Umma katika chuo cha Umma cha Kenya School of Government kati ya 1999 na 2000.
Mapema alifanya kazi katika ofisi ya rais kama kadeti katika afisa ya mkuu wa Wilaya 1990. Baadaye alipanda ngazi na kuwa msaidizi mkuu wa waziri wa masuala ya umma mwaka 1991.
Vilevile alihudumu kuwa afisa mkuu wa wilaya huko Ng'arua , wilayani Laikipia kutoka 1997 hadi 1999.
Pia alihudumu kuwa msaidizi wa Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa waziri wa serikali za mitaa.

Chanzo cha picha, RUTO Campaign
Kwa kipindi cha miaka minne kati ya 2002 na 2006, Rigathi Gachagua alikuwa msaidizi binafsi wa rais Uhuru Kenyatta.
Akiwa mgombea wa chama cha KANU 2002, bwana Kenyatta alisafiri na bwana Gachagua nchi nzima akifanya kampeni yake ya urais.













