Vita vya Ethiopia: Ushahidi wa mauaji ya watu wengi wanaochomwa - mashahidi

Ethiopians who fled the ongoing fighting in Tigray region, gather in Hamdayet village near the Sudan-Ethiopia border, eastern Kassala state, Sudan November 22, 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watigray wengi walitoroka jimbo lao wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka mwezi Novemba 2020

Mabaki ya miili ya mamia ya watu yanaharibiwa kwa makusudi katika kampeni iliyoandaliwa ya kupoteza Ushahidi wa uangamizaji wa jamii katika jimbo la magharibi mwa Ethiopia la Tigray, kulingana na mahojiano na mashahidi 15.

Madai hayo yanafuatia ripuoti nyingi za kulengwa kwa watu wa jamii ya Watigray wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Pia yanakuja kabla ya uwezekano wa kuwapeleka timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ambayo itaongozwa na Mwendesha mashitaka wa zamani wa Mahakama ya kimataifa ya Fatou Bensouda.

Watu wa vikosi vya usama kutoka jimbo jirani la Amhara , ambavyo vinashikilia eneo la magharibi mwa Tigray, wamekwa wakionekana wakichimba makaburi mapya, wakifufua mamia ya miili, wakiichoma na kisha kusafisha masalia nje ya jimbo, walioshuhudia walisema katika mahojianoya simu.

Maafisa wamekiri kuwa makaburi yamekuwa yakichimbwa , lakini wanasema kwamba yanaonyesha ushahidi kwamba vikosi vya Watigray vimekuwa vikifanyya kampeni yake ya kuhamasisha mauaji katika miongo ya hivi karibuni . Watafiti kutika Chuo kikuu cha Gondar wamekuwa pia wakifichua maeneo ya makaburi ya jumla ambayo wameyahusisha na waoiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Pande zote mbili zinazohusika katika vita vinavyoendelea zimekuwa zikishutumiwa kwa kutekeleza mauaji ya watu wengi.

Lakini katika ripoti ya hivu karibuni , makundi ya kutetea haki za binadamu ya Manesty International na Human Rights Watch yaliwashutumu maafisa wa Amhara na vikosi vya usalama kwa kuwa nyuma ya uangamizaji wa kabila dhidi ya Watigray katika eneo hilo.

A destroyed tank is seen in a field in the aftermath of fighting between the Ethiopian National Defence Force (ENDF) and the Tigray People"s Liberation Front (TPLF) forces in Kasagita town, in Afar region, Ethiopia, February 25, 2022.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mabaki ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yanaweza kushuhudiwa kote kaskazini mwa Ethiopia

Mapigano ambayo yalianza mwezi Novemba mwaka 2020, yalifuatiwa na mzozo baina ya serikali ya shirikisho ya Waziri mkuu Abiy Ahmed na TPLF, chama chenye Watigray wengi.

Mwezi Disemba mwaka Last December, baraza la Umoja wa Mataifa la haki za kibinadamu lilipitisha azimio la kuanzisha uchunguzi huru kuhusu maasi yaliyotekelezwa na pande zote zinazohusika na mzozo.

Serikali ya Ethiopia ilipinga azimio hilo na kuapa kutoshirikiana na wapelelezi , ikisema azimio lilikuwa ni "chombo cha shinikizo la kisiasa".

Katika kura mwezi Machi, azma ya Ethiopia ya kuzuwia ufadhili kwa ajili ya jopo la uchunguzi ilifeli. Urusi na Uchina zilikuwa zimeunga mkono serikali ya Ethiopia katika jaribio la kuzuwia ufadhili.

Walioshuhudia wamesema kuwa siku tatu baada ya kuidhinishwa kwa ufadhili, kampeni ya kupoteza Ushahidi wa maasi ilianzishwa magharibi mwa Tigray.

"katika kipande cha ardhi nyuma ya shule ya Hamele Hamushte, iliyopo katika mji wa Humera , miili 200 ya raia wa jamii ya 200 Tigray ilizikwa kwenye makaburi mawili ya watu wengi. Hawa ni raia waliouawa katika miezi ya mwanzoni ya vita,''alisema shahidi kutoka katika kikundi cha kabila la Welkyat wanaoishi katika eneo la Humera.

Wakati Watigray ama walitoroka eneo hilo wakati wa mapigano au wamefungwa watu wa kikundi cha Welkyat wamebakia na wametoa ripoti za ushuhuda.

"Tarehe 4 Aprili, twanamgambo wa Amhara na Fano, kikundi cha [wanamgambo] vijana kilifufua masalia ya miili. Walikusanya kuni, wakapulizia kitu ambacho hatujawahi kukiona kablana kuchoma masalia waliyokuwa wameyakusanya. Masalia yalinyauka na kubadilikuwa kuwa jivu."Ushahidi huo ulisalia kuwa huo huo kutoko kwa mashahidi wengine waliozungumzia kuhusu tukio hilo.

Wanamgambo wa Amhara na vijana wa Fano waliharibu masalia ya miili iliyokuwa imezikwa katika sehemu nyingine ya Humera, mashahidi walisema.

"Miili hiyo ni ya raia walioonyeshwa mbele za watu kutoka kwenye kambi za mahabusu.

Ilikuwa ni karibu miili 100 iliyozikwa pamoja nyuma ya ardhi ya ofisi ya umma ya taasisi ya kilimo ya Humera, alisema shahidi mwingine.

"Walichukua masalia kwenye uwanja wa taasisi na kuigeuza kuwa jivu kwa kutumia kuni, moto na kemikali ambayo hatuijui. Wakati walipokuwa wanafanya hivyo nyuso zao zilikuwa zimefunikwa kwa barakoa na walivaa glovu."

Map

Adebay ni mji mwingine uliopo magharibi mwa Tigray ambako mashahidi walielezea kuharibu ushahidi kwa kuhamisha masalia ya miili ya binadamu.

"Asubuhi ya tarehe 10 Aprili, wanamgambo wa Amhara walichimba makaburi manne ya watu wengi katika Kanisa la St Abune Argawi," mkazi wa Adebay alisema.

"Ilikuwa ni miili 150 ya raia waliuawa katika wimbi la mwezi Agosti la kuangamiza kabila. Walipakia miili ndani ya lori. Hatujui walikopeleka masalia ."

Shuhuda alisema kwamba katika siku hiyo hiyo kaburi la watu wengi lililopo nyuma ya ofisi ya utawala ya Adebay lilifukuliwa. Raia walikuwa wamedai raia thelathini na tisa walikuwa wamezikwa pale mwezi Oktoba, 2021 baada ya kuzingirwa katika mji wa Adi Gosh na wakakamatwa walipokuwa wakijaribu kutoroka.

Kulingana na ushuhuda masalia ya miili yalipakizwa ndani ya lori na kuhamishiwa mahala pasipojulikana.

Katika mji mwingine, Beaker, uliopo kati ya Tirkan na Rawyan, shahidi mwingine alielezea shuguli sawa na hiyo.

"Miili hiyo ilikuwa ni ya raia 70 ambao walikuwa wamekamatwa katika Beaker.Waliuliwa miezi tisa iliyopita," mkazi alisema.

"Tarehe 11 Aprili wanamgambo wa Amhara waliwafufua na kuwapeleka khadi sanja, mji uliopo katia jimbo la Amhara."

Mashahidi walisema kampeni ya kuharibu ushahidi ilianza tarehe 4 Aprili na iliongozwa na wataalamu kutoka Chuo kikuu cha Gondar kilichopo katika jimbo la Amhara.

"Yote ilianza kufuatia ziara ya wataalamu kutoka Chuo kikuu Gondar''

Walipokuja, walikuja na malori ambayo yalikuwa yamejazwa kemikali zilizokuwa kwenye magaroni meupe . Wataalamu walikuwa mjini humo kwa wiki kadhaa wakitoa mafunzo kwa wanamgambo wa Amhara kuhusu jinsi ya kutupa masalia ya miili na halafu wakarejea," shahidi alisema.

Wakazi watatu walisema kwamba wanamgambo walikuwa wakizungumzia wazi kuhusu uhusiano wao na Chuo kikuu cha Gondar na kujigamba wakisema kuhusu jinsi ambavyo ushahidi wa mauaji hautagundulika.

Chuo kikuu hakijajibu ombi la kukitaka kutoa kauli yake kuhusu madai yaliyotolewa kukihusu.

Lakini mwezi uliopita, shirika la taifa la utangazaji liliripoti kwamba watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gondar wamekuwa wakifanya kazi kwenye maeneo 12 ya makaburi ya watu wengi na wamepata ushahidi kuwa TPLF walihusika na vitendo vya mausji ya kimbari.

Wataalamu wamethibitisha kwamba inawezekana kuharibu mabaki ya miili ya binadamu kwa kutumia kemikali fulani.

Profesa wa kemia ya katika University College London, Andrea Sella, alisema kuteketeza miili inawezekana ili mradi kiwango cha juu cha joto kilifikiwa.

Gebrekidan Gebresilassie, ambaye ni dokta katika uhandishi wa kemikali katika Chuo kikuu cha Ujerumani cha RWTH Aachen , pia alisema inawezekana kuharibu ushahidi wa utambuzi wa miili kwa usaidizi wa kemikali ambazo tayari zinapatikana.

"Kemikali hizi huharibu ushahidi wa utambuzi wa miili…Lakini kwa kutumia kemikali hata majivu yanaweza kuonyesha baadhi ya ushahizi fulani . Ni vigumu kuuhari wote ," alisema.

Ofisi ya Waziri mkuu haijajibu ombi la kuitaka itoe kauli yake na spika wa Bunge la Shirikisho, Agegnehu Teshager, alikanusha shutuma kwamba ushahidi wa utaratibu wa kuharibiwa kwa ushahidi.

Alisema kwamba ufufuaji ulikuwa unaendelea lakini kwamba miili ilikuwa inondolewa ilikuwa ni nile ya watu wa kabila la Amhara ambao walikuwa wameuawa mika 40 iliyopita.

"Haiwezekani kufukua makaburi ya watu wengi na kuionyesha dunia siku hizo kwasababu TPLF walikuwa wanaongoza nchi ," alisema . TPLF kilikuwa ni chama chenye mamlaka zaidi katika muungano ambao uliiongoza Ethiopia kuanzia miaka ya 1990 hadi 2018, wakati Bw Abiy alipoingia mamlakani.

Bwana Agegnehu pia alikanusha ripoti za kuangamizwa kwa kabila magharibi mwa Tigray ikiwa ni pamoja na zile zilizotolewa na Amnesty na Human Rights Watch. Alizielezea kama ripoti za uongo. "Ni ripoti za kusisimua ambazo hazizingatii hali halisi katika eneo ," alisema.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Vita Ethiopia: Kwanini kinaendelea Tigray ni muhimu?