Vita vya wenyewe kwa wenyewe Ethiopia: Hospitali Tigray yaishiwa na chakula kwa watoto walio na njaa

Chanzo cha picha, Getty Images
Surafeal Mearig mwenye umri wa miezi mitatu amelala bila msaada wowote katika hospitali kubwa zaidi katika jimbo lililokumbwa na vita la Tigray.
Macho yake yamefunguka wazi, na mbavu zake zinaonekana zikipanda na kushuka ndani ya nyembamba yenye makunyanzi. Ni miongoni mwa watoto wengi wanaoumia kutokana na utapiamlo, kwasababu ya vita vya wenywe kwa wenyewe vya miezi 14 ambavyo vimesambaa katika majimbo jirani ya Afar na Amhara.
Daktari wa watoto anayemshugulikia Surafeal katika hospitali ya rufaa ya Ayder Referral katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ana uzito wa mwili wa kilo 2.3, kilo moja chini ya kilo alizokuwa nazo alipozaliwa.
Onyo: Baadhi ya wasomaji wanaseza kusumbuliwa na picha iliyopo chini kwenye taarifa hii
Kulingana na maelezo kwa waandishi wa habari yaliyochapishwa na mhudumu wa hospitali, maziwa ya mama yake yalikuwa yamenyauka na wazazi wake, ambao wote hawana ajira, hawawezi kununua maziwa ya watoto ili kuweza kumpatia mtoto wao.
Muhimu ni kwambamhudumu wa hospitali anasema wanaishiwa na vyakula vinavyoweza kuwatibu watoto utapiamlo kama Surafeal.
"Ni miezi sita sasa tangu tusambaziwe vyakula hivi kutoka Adis Ababa ( mji mkuu wa serikali kuu ya shirikisho]," daktari ambaye hakupenda jina lake katika hospitali aliiambia BBC kwani anahofia familia yake kulengwa.
"Tunakaribia kumaliza kile tulichokuwa tumepewa tangu msaada wa kwanza ulipowasili mwezi Juni. Kila kitu kinaisha," aliongeza.
Wiki hii wafanyakazi wa tiba katika hospitali ya Ayder waliwasilisha ripoti kwa mashirika ya kimataifa ya misaada wakiomba usaidizi.
Surafeal alikuwa mmoja wa wale waliotolewa kama mfano wa watoto wenye ukosefu wa msaada wa lishe.

Chanzo cha picha, Reuters
Madaktari wanasema zaidi ya 40% ya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano wanaokuja hospitali wanakabiliwa na utapiamlo- mara dufu ya kiwango cha mwaka 2019.
Medhaniye ambaye alizaliwa akiwa mwembamba pia amelala kwenye kitanda cha hospitali , akila kwa kutumia mrija uliounganishwa kupitia puani kwake.
Ripoti yake ya matibabu inasema alianza kuugua kutokana na utapiamlo baada ya wanajeshi kuishambulia nyumba ya familia yake na kuwachinja ngobe, kuharibu na kupora mali zao.
BBC haikuweza kupata dur uhuru za kuthibitisha maelezo hayo katika ripoti ya daktarin kwani kwa kiasi kikubwa Tigra imekuwa haina mawasiliano tangu mwezi Novemba 2020, wakato mzozo ulipoibuka baina ya wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF), ambao wanadhibiti eneo kubwa la jimbo, na serikali ya shirikisho.
Waandishi wa habari hawajaweza kutembelea Tigray tangu mwezi Julai. July.
Kuzuwia utokwaji wa damu kwa mikono mitupu
Katika ripoti yao madaktari wamelaumu "kufungwa kwa eneo" kwa miezi sita kulikofanywa na vikosi vya shirikisho na washirika wake kwa kusababisha uhaba mkubwa wa madawa na vifaa vya tiba jambo ambalo wanasema linasababisha vifo visivyoweza kuepukika.
"Tangu jimbo lilipokumbwa na mapigano, wagonjwa wengine 35 wamepoteza maisha yao kutokana na ukosefu wa huduma ya mashine ya kusukuma damu kwa wagonjwa wa figo-dialysis service," inasema ripoti.
Madaktari wanasema wamelazimika kuzuwia uvujaji damu kwa kutumia mikon yao mitupu na glovu zilizotumika au kutengeneza vitakasa mikono wenyewe.
Katika jibu lake, msemaji wa serikali Legesse Tulu aliiambia BBCkwamba ripoti inaponekana "kutaka kujenga hadithi " kwa TPLF na "kuigiza" madai yake ya kuzuiwa kwa Tigray.
"Kwa upande wa serikali, hakuna vikwazo vya makusudi katika Tigray ambavyo vinawaumiza watu wetu," he said.
Lakini tangu vita vilipoanza, mashirika ya misaada yamekuwa yakilalamika kuhusu kutoweza kupata taarifa za kutosha ndani ya Tigray.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya haki za binadamu (Ocha) tarehe 30 Disemba, msafara wa magari ya msaada haujafika bado Tigray tangu katikati ya mwezi wa Disemba kwasababu ya urasimu wa ucheleweshaji na ukosefu wa usalama.
Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, linakadiria kwamba malori 100 yaliyobeba misaada yalihitajika kufika Tigray kila wiki ili kukidhi mahitaji ya zaidi ya watu milioni tano, lakini kulingana na Ocha ni 12% ya misaada iliyohitajika iliyoweza kufika katika jimbo hilo.
Akijibu malalamiko hayo kuhusu kupelekwa kwa misaada Legesse alisema: "Zaidi ya magari 840 kati ya 1,100 ya misaada na madawa yaliyokwenda Tigray bado hayajarudi.
Yanashukiwa kutumiwa na TPLF kubeba makurutu, wanajeshi na zana za kijeshi ."
TPLF imekanusha madai kuwa inazuwia misaada, lakini vikosi vyake pia vimekuwa vikishutumiwa kwa uporaji wa magala ya misaada na majengo ya afya katika maeneo inayoyashikilia katika majimbo ya Amhara na Afa.r
Daktari katika hospitali ya Ayder Hospital aliiambia BBC kwamba hata familia za wafanyakazi pia zinaathiriwa na mzozo.
"Mtoto wangu ana ugonjwa wa Kiambatisho na hawezi kupata matibabu ," alisema.
Na huku ukosefu wa huduma za afya ukiendelea alisema hawatakuwa na chaguo bali kuacha upasuaji wote kufikia wiki ijayo.
"Hatuna vifaa. Hapo ndipo tulipofikia sasa,ndio maana tunataka dunia ifahamu. hospitali nyingi zinafungwa."












