Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Ni kwanini Urusi inasema Kuna hatari "kubwa" ya Vita Kuu ya III
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov anaamini kuna hatari "kubwa " ya Vita vya III kufuatia uvamizi wa Urusi wa Ukraine.
Katika mahojiano ya televisheni na kituo cha Urusi - Channel , siku ya Jumatatu (4/25), Lavrov alizishutumu nchi za Muungano wa kijeshi -NATO kwa kuchochea "wakala" katia Ukraine kwa kutoa silaha na msaada wa vifaa kwa Waukraine.
Kulingana na Waziri huyo wa Urusi, hii "inamwaga hata zaidi mafuta juu ya moto'' -na akaongeza juhudi zote zinapaswa kufanyika kuepuka vita ya tatu ya dunia.
Bw Lavrov aliulizwa kuhusu kauli ya rais wa Marekani Joe Biden kwamba mzozo wa nyuklia unapaswa kuepukwa.
"Harari ni za juu sana [za vita ya tatu]. Sitaki kusema hilo kwa mzaha ," Lavrov alisema, kulingana na nakala iliyopo kwenye wavuti wa Wizara ya mambo ya nje ya Urusi. "Hatari ni kubwa, halisi. Haipaswi kupuuzwa."
Lavrov alisema kwamba Moscow na Washington zinapaswa kufufua utekelezwaji wa ahadi zilitotolewa na viongozi wa zamani wa Urusi na marekani Mikhail Gorbachev na Ronald Reagan kwamba "hapawezi kuwa na washindi katika vita vya nyuklia ".
Bw. Lavrov pia alitaka kulinganishwa hatari za malumbano ya nyuklia leo kwa kuzingatia uzoefu wakati wa mzozo wa makombora wa Cuba katika mwaka 1962 baina ya Marekani na Muungano wa Usovieti.
"Wakati wa mzozo wa makombora wa Cuba, hapakuwa na sheria nyingi zilizoandikwa, lakini sheria zilizotumiwa zilikuwa wazi vya kutosha. Urusi ilielewa tabia ya Washington.
Washington jinsi Moscow ilivyotenda. Leo, zimesalia sheria chache," anajibu Lavrov.
Je ni jaribio la Urusi kuitisha dunia ?
Waziri wa Ulinzi anazichukulia kauli za Waziri wa mambo ya nje wa Urusi kuwa tu kama za "kutisha".
"Utambulisho wa Lavrov, kwa zaidi ya miaka 15 kama Waziri wa mambo yan je wa urusi, ni aina hii ya vitisho. Sidhani kuna tisho lolote la hali mbaya kwa sasa . ", James Heappey aliisisitia BBC.
"Kile ambacho nchi za Magharibi zinakifanya kuwasaidia washirika wake katika Ukraine kimepangwa vizuri sana."
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Urusi kutumia silaha za ''kimkakati'' za nyuklia, Bw Heappey alisema anaamini kuna uwezekano wa "kupungua" uwezekano wa kuongezeka kwa hali mbaya. Bw Heappey alisema kwamba huku NATO ikiimarisha usaidizi wake katika eneo la mashariki, haitoi msaada wa kijeshi.
Serikali ya Uingereza inasema sio sahihi kuonyesha vita katika Ukraine kama juhudi za NATO dhidi ya Urusi.
"Hii sio juhudi ya NATO, bali ni kuungana kwa nchi wahisani katika kutoa mchango wa ushirikiano kwa Waukraine na msaada huu hutolewa hata nje ya mipaka ya NATO " , tWaziri wa Uingereza aliiambia BBC.
"Ni dhana inayoifaa Kremlin kudai kuwa wako katika makabiliano ya namna fulani na NATO. Walikuwa wanasema hilo hata kabla vita havijaanza , lakini haina maana na Lavrov analijua hilo ."
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kulebo alisema kauli za Lavrov lilikuwa ni jaribio la Urusi la "kuitisha dunia isiisaidie Ukraine".
Hofu ya kuongezeka kwa mzozo katika Ukraine kuelekea kuwa vita vya nyuklia, au hata vita ya tatu ya dunia ( inayohusisha NATO na Urusi), imekuwa ikiendelea tangu mwanzoni mwa uvamizi.
Mwezi Machi, siku kadhaa baada ya kuanza kwa uvamizi, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza utayari wa "vikosi vya kuzuwia" - tangazo ambalo lilieleweka kumaanisha silaha za nyuklia- kuwa katika "utayari wa vita"
Hii imeibua uoga kwamba Urusi inatumia silaha za nyuklia za "kimkakati" , ambazo zinaweza kutumiwa kwa umbali mfupi. Hatahivyo, hakuna lolote kati ya haya lililothibitishwa hadi sasa.
Jumanne (26/4), Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliulizwa iwapo anahofu kwamba mzozo katika Ukraine utageuka kuwa wa nyuklia. Alijibu, "Hapana."
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine