Netflix kuwachukulia hatua wanaoshirikishana nywila, huku wateja wake wakipungua

Millie Bobby Brown (centre)

Chanzo cha picha, Netflix

Maelezo ya picha, Msururu wa vipindi vyake vipya Stranger Things utarushwa hewani mwezi Mei

Netflix imedokeza kuwa itafanya msako katika nyumba zinazoshirikishana nyula huku ikitafuta wateja wapya wajiunge na mtandao huo kufuatia kupungua kwa idadi kubwa ya wafuasi wake.

Wafuasi wake wapatao 200,000 walijiondoa kwenye huduma hiyo ya matangazo ya ya moja kwa moja katika kipindi cha kwanza cha miezi mitatu yam waka huku ikikabiliw ana ushindani mkubwa kutoka kwa mahasimu wake. Pia inakumbwa na kuondoka kwa wateja wake wakati ilipopandisha garama katika baadhi ya nchi na kuondoa huduma zake nchini Urusi.

Netflix iliwaonya washika dau kuwa wafuasi wake wengine milioni mbili wanaweza kuondoka kwenye mtandao huo katika kipindi cha miezi mitatu kufikia Julai.

"Ukuaji wa mapato yetu umedorora kwa kiwango kikubwa ," kampuni hiyo iliwaambia washikadau Jumanne baada ya kuchapisha matokeo ya mapato ya robo ya kwanza ya mwaka.

"Kupenya kwetu kwa kiwango cha juu katika makazi -wakati tunajumuisha idadi kubwa ya makazi yanayoshirikishana akaunti -pamoja na ushindani, inasababisha kupungua kwaukuaji wa mapato."

Kampuni hiyo kubwa ya utoaji wa hudumua za moja kwa moja za data za kimtandao inakadiria kuwa makazi milioni 100 ya watu yanakiuka sheria zake kwa kushirikishana nywila.

Awali mkuu wa wake Reed Hastings alielezea suala hilo kama "kitu ambacho unanapaswa kuishi nacho", akiongeza kuwa kwa kiasi kikubwa ni kitu "halali'' baina ya wanafamilia. Halafu pia kampuni ilisema ushirikishanaji wa akaunti za Netflix huenda umechochewa na ukuaji kwa kupata watu wengi zaidi wanaotumia Netflix.

Lakini Jumanne Bw Hastings alisema ushirikishanaji wa akaunti miongoni mwa watu wa familia kunaoufanya mtandao huo kuwa na ugumu wa kuwavutia wafuasi wapya wanaojisajiri katika baadhi ya nchi.

"Wakati tlipokuw atunakua haraka, kilikuwa ni kipaumbele cha kwanza kufanyia kazi ushirikishwaji wa akaunti. Na sasa tunahangaika sana juu yake," aliwaambia washikadau.

Kampuni hiyo ilisema kwamba hatua hiyo inalenga kujaribu kukabiliana na ushirikishanaji wa nywila katika Amerika Kusini -na inaweza kuanzishwa katika nchi nyingine, huku zenye akaunti zilizokiuka sheria zikilipishwa garama ya ziada.

Dominic Sunnebo, mchanganuzi katika kamouni ya utafiti ya Kantar,alionya kuwa mpango huo unaweza kuwa na athari mbaya.

"Kuwashawishi hata kikundi kidogo cha watu 100 wanaoshirikishana nywila kuwa wateja kamili wanaolipa sio kazi rahisi, hususan wakati wanunuzi wanatafuta njia za kunusuru pesa zao, sio kutumia zaidi," alisema.

"Kama mfumo wa kukabiliana na ushirikishanaji wa nywila utakwenda haraka na kwa nguvu, pia kutakuwa na hatari ya kuwafanya watazamaji ambao wangetaka kujiunga siku zijazo wajitenge''

Kuathiriwa na garama ya maisha

Netflix ilisema kuondoka kwake nchini Urusi mwezi Machi kulitokana na vita vya Ukraine ambapo ilikosa wafuasi waliojisajiri 700,000.

Watu wengine 600,000 waliacha kutumia huduma ya Netflix katika nchi za Marekani na Canada baada ya kupandisha garama zake mwezi Januari.

Kampuni ilipandisha garama za huduma yake kote.

Mipango yake yote ya Ulaya , huku mpango wake wa kimsingi ukiongeza garama kutoka dola 9 hadi dola 10 kwa mwezi, na wa kawaida kutoka doa 14 hadi dola 15.50.

Nchini Uingereza wakati huo huo mipango yake yote ilikuwa na ongezeko la pauni 1 kwa mwezi na hivyo kufikia garama ya pauni 6.99 na 10.99.

Netflix ilisema kuwa ongezeko la bei itavuna peza zaidi kwa kampuni, licha ya kusitishwa kwa huduma zake.Lakini wachambuzi wanasema kuongezeka kwa garama ya huduma za Netflix kutaziathiri familia kadri gharama ya maisha inavyozidi kuongezeka.

Nchini Uingereza makazi milioni 1.5 yalisitisha usajiri wa huduma za Netflix katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka, huku 38% wakisema walitaka kutunza pesa zao.

The Featheringtons

Chanzo cha picha, LIAM DANIEL/NETFLIX

Maelezo ya picha, Moja ya misururu ya vipindi maarufu vya Netflix , Bridgerton, ulizindua msururu wake wa pili mwezi uliopita.

Akionekana kukubali hili, Bw Hastings alisema Netflix ilikuwa inataka kuanzisha huduma huru inayosaidiwa na matangazo ya biashara kama tu washindani wake Disney na HBO.

Wachambuzi wanasema inaweza kufunga mapato mapya muhimu kwa kampuni hiyo ambayo imeepuka matangazo ya biashara.

Wachambuzi wanasema tisho kubwa zaidi kwa Netflix ni ushindani mkubwa kutoka katika makampuni kama vile Amazon, Apple na Disney, ambayo yanamwaga pesa katika huduma zao za matangazo ya moja kwa moja ya mtandao.

Kuhama kwa wateja

Hisa katika kampuni kubwa ya matangazo ya mtandaoni Netflix zilishuka kwa 25% saa chache baada ya mauzo kutokana na matoke yake, na kuondoa zaidi ya dola bilioni 30 kwenye tathmini ya thamani ya soko.

Kampuni hiyo- ambayo bado inaendelea kuongoza duniani kwa utoaji wa huduma za huduma ya matangazo ya moja kwa moja ya mtandaoni ikiwa na zaidi ya wafuasi milioni 220 - ilishuhudia ukuaji wa wafuasi waliojisajiri katika kipindi cha robo ya mwaka bila kuingiliwa tangu Oktoba 2011.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Filamu ya kwanza ya Kitanzania yaanza kuoneshwa Netflix