Ni nchi gani huwapeleka wanaoomba hifadhi katika mataifa ya ng'ambo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Uingereza imetangaza mpango wa kuwatuma baadhi ya wakimbizi wanaovuka kwa maboti Rwanda, Afrika, kuishi huko.
Mfumo huo unawalenga wanaume wasio na familia wanaoingia Uingereza kinyume cha sheria kwa boti au kwa kujificha ndani ya lori. Yaliyo muhimu katika mpango huo ni pamoja na:
- Wale wanaoingia Uingereza kinyume cha sheria kwa njia hii wanakabiliwa na hatari ya kupelekwa Rwanda, Afrika, ambako maombi yao ya uhamiaji yataangaliwa.
- Watakuwa na mahala pa kuishi na kuwa huru kuja na kwenda wakati wowote ule huku maombi yao yakishugulikiwa.
- Wale ambao maombi ya uhamiaji wao yataidhinishwa watasaidiwa kuanza "maisha mapya" nchini Rwanda, ambapo wataweza kupata elimu na usaidizi mwingine wa hadi miaka mitano.
- Watu ambao maombi yao yatakataliwa watakuwa na fursa ya kuomba kubaki Rwanda, au nchi nyingine ambako wana haki ya kuishi
- Uingereza sio nchi ya kwanza kuwapeleka wanaotafuta hifadhi katika nchi za ng'ambo. Je ni vipi sera sawa na hii inavyotumika katika nchi nyingine?
Australia
Australia ilianza kwanza kutumia vituo vya wahamiaji katika nchi za kigeni mwaka 2001.
Katika mwaka 2013, Australia iliiimarisha sheria zake za uhamiaji kwa kukataa kuwapatia vibali vya kuishi nchini humo (visa) wanaotafuta hifadhi wanaowasili Australia kwa njia ya boti.
Maelfu ya watu wanaotafuta hifadhi walihamishiwa nje ya Australia katika kipindi hiki, huku mamlaka za mpaka za Australia zikisema kuwa zaidi ya watu 4000 walioingia kwa njia hiyo walipewa makazi katika nchi za ng'ambo katii ya mwaka 2012 na 2019.
Takriban wakimbizi na wahamiaji kwa sasa wanapatiwa makazi katika taifa la kisiwa- Pacific linaloitwa Nauru, huku mpango unaofanana na huo uulifanyika katika kisiwa cha Manus katika Papua New Guinea ukikamilika 2021, ambapo watu 120 walipatiwa makazi huko. Watu wanaweza kuchagua kubakia katika eneo hilo au kuhamia Nauru.

Chanzo cha picha, Getty Images
Makundi ya haki za binadamu na Umoja wa Mataifa wamekuwa wakikosoa mara kwa mara mazingira duni na hali za vituo vya makazi ya wahamiaji vilivyoanzishwa na Australia.
Jumla ya wahamiaji 13 waliopelekwa katika Nauru na Papua New Guinea wamekufa kutokana na ghasia, ukosefu wa huduma za matibabu na kujiua.
Mwandishi mkimbizi Mkurdi kutoka Iran Behrouz Boochani aliiambia BBC mwaka 2019 kwamba vituo vya makazi ya wahamiaji katika kisiwa cha Manus Island vilikuwa kama magereza, akisema mgfumo wa makazi wa Australia ulikuwa kama wa "kutudhalilisha na kutuangamiza".
Alisema kuwa Australia iliwapeleka "kutoka kwenye bahari'' moja kwa moja mpaka katika kisiwa cha Manus- Manus Island na kuwaacha bila usaidizi wowote, na alihisi haki za binadamu zilikiukwa.
Australia inasema ina maana kuwa na mfumo wa sera ya kituo cha wahamiaji , kwasababu inawazuwia wanaotafuta uhamiaji kufa ndani ya bahari, ambacho maafisa wanakadiria kuwa kiligarimu hadi pauni milioni milioni 460 kati ya mwaka 2021-22.
Katika mwezi Machi 2022, Australia na New Zealand zilitangaza makubaliano ya ambapo wanaotafuta uhamiaji wapatao 450 watahamishwa kutoka katika vituo vya makazi ya wenyeji vya Australia na kupelekwa kwenye vituo vya wahamiaji nchini New Zealand.
Israel
Katika kukabiliana na idadi inayoongezeka ya watu wanaothafuta uhamiaji na wahamiaji wengine haramu, wengi wao kutoka mataifa ya Sudan na Eritrea, Israel ilifanya mkataba nchi ya tatu "salama" itakayokubali idadi ambayo haijulikani ya wahamiaji.
Israel bado haijafichua ni nchi gani mbili ambazo ilikubaliana nazo , lakini taarifa za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa nchi hizo mbili ni Rwanda na Uganda
Mpango huo ambao ulianza mwaka 2015, unawapatia waombaji wa uhamiaji na wahamiaji wengine haramu chaguo la kurejea katika nchi zao za asili, au wapokee dola 3,500 na nauli ya ndege ya kwenda nchi nyingine ya tatu, ambako watafungwa iwapo wangeishi Israel.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika mwaka 2018, Israel ilisema kwamba kulikuwa na watu wapatao 65,000 ambao waliingia Israeli kinyume cha sheria, na takriban 20,000 walikuwa wameondoka Israel kupitia mojawapo ya mpango wake wa makazi katika nchi ya ng'ambo.
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa mpango wa "kurejea kwa hiaria katika nchi ya asili " kwani huwapa wanaotafuta uhamiaji dhana potofu ya kwenda katika nchi ambayo haiwezi kuwahakikishia hadhi yao ya kisheria au kwamba hawatarejeshwa katika nchi yao ya asili.
Mpango mwingine wa Israel wa kulazimisha kuwatuma wanaoomba uhamiaji na wahamiaji wengine haramu katika nchi ya tatu, waliripotiwa Uganda na ulisitishwa na Mahakama ya juu zaidi ya Israel.
Denmark
Serikali ya Denmark haijawahi kuwa na aibu ya kuwa na lengo la kuwa "bila mkimbizi " katika Denmark.
Katika mwezi Juni, 2021, Denmark ilipitisha sheria inayoiruhusu serikali kuhamisha maombi ya waombaji wa uhamiaji katika nchi ya tatu nje ya Muungano kwa ajili ya kuishi huko.
Hatua hiyo yenye utata imekuwa ikikosolewa vikali na Tume ya Muungano wa uLya na makundi ya haki za binadamu, wakihoji uhalali wake wa kisheria.
Ziara ya Waziri wa Uhamiaji wa Denmark Matthias Tesfaye nchini Rwanda katika mwaka 2021 iliibua fununu kubwa kwamba Denmark inamalengo ya kufungua kituo cha makazi ya wahamiaji nchini Rwanda.
Pande mbili zilisaini makubaliano, lakini hakuna mafanikio thabiti kwa sasa kuhsuu vituo vyovyote vya makiazi ya wakimbizi.
"Tuna mazungumzo na Rwanda, yenye misingi ya ushirikiano mpana, lakini hakuna makubaliano kuhusu uhamisho wa wanaoomba uhamiaji ," Tesfaye alisema.
"Ninakubaliana na mfumo wa maombi ya uhamiaji wa serikali za Rwanda na Uingereza hauwezi kuimarishwa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Denmark ilikuwa ni nchi ya kwamba kusaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa wakimbizi katika mwaka 1951, lakini katika miaka ya hivi karibuni serikali imekuwa ikiweka sheria kali za uhamiaji.
Katika mwaka 2021, Denmark ilianza kukataa maombi ya vibali vya makazi vya mamia ya Wasyria, jambo ililoibua utata, lakini serikali ya Denmark inasema wanaweza sasa kurudi kwa usalama nchini Syria.
Denmark, hatahivyo, ina mtazamo tofauti kabisa kwa Ukraine, ikiazimia kuwapatia makazi hadi watu 100,000 kutoka Ukraine na kuwapatia vibali vya kazi.












