'Mpango wa Uingereza wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda 'ni kinyume cha Mungu' - Welby

Chanzo cha picha, PA Media
Mpango wa serikali wa kuwatuma baadhi ya wahamiaji kutoka Uingereza kwenda Rwanda ni "kinyume na asili ya Mungu ", Askofu Mkuu wa Canterbury alisema.
Katika mahubiri yake yake ya Pasaka , Justin Welby alisema kuwa kufufuka kwa Kristo haukuwa muda wa "kuwapatia wengine majukumu yetu".
Pia alitoa wito wa usitishwaji wa mapigano nchini Ukraine ambapo alizungumzia kuhusu hofu yake juu ya gharama ya kuishi iliyotokana na mzozo.
Serikali inasema mabadiliko yanahitajika kuyalinda maisha ya watu dhidi ya wasafirishaji haramu wa watu.
Chini ya mpango wa pauni milioni 120-uliotangazwa wiki iliyopita - watu walioonekana kuingia Uingereza watasafirishwa vibaya katika nchi ya Afrika Mshariki, ambako wataruhusiwa kuomba haki ya kuishi.
Upelekwaji wa wahamiaji hao nchini Rwanda, umekabiliwa na upinzani, huku mashirika zaidi ya 160 ya misaa na makundi ya kutetea haki za binadamu yakiwataka mawaziri waachane na kile wanachokielezea kama sera "katili".
Pia imekosolewa na vyama vya upinzani na baadhi ya wafuasi wa Conservative.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imejitetea kutokana na ukosoaji wa Askofu Welby , ikisema kuwa Uingereza ina "historia ya kujivunia" ya kuwasaidia wale wenye shida na mipango ya kuwasaidia kuishi imetolewa " njia salama na za kisheria kwa ajili ya hali zao bora za zijazo " kwa ajili ya maelfu.
"Hatahivyo dunia inakabiliwa na mzozo wa dunia wa uhamiaji kwa viwango ambavyo havikutarajiwa na mabadiliko yanahitajika ili kuzuwia wasafirishaji haramu wa watu kuyaweka maisha ya watu hatarini na kutengeneza mfumo wa dunia kuhusu wahamiaji uliovunjika ," msemaji alisema.
Wizara ya mambo ya ndani ilisema Rwanda ni "salama " na itatatua madai kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Chanzo cha picha, Reuters
Mpango huo, awali utalenga wanaume wasio na familia wanaotaka kuvuka kivuko kwa boti au kwa kutumia lori kutoka Ufaransa.
Waziri Mkuu alisema "itaokoa maisha ya watu mengi" na kuvunja mtindo wa biashara ya wasafirishaji haramu", lakini wanaharakati wameutaja mpango huo kama "usio wa kibinadamu".
Vivuko viwili zaidi vya wahamiaji vilirekodiwa Ijumaa asubuhi licha ya ukungu mwingi, mwandishi wa BBC Simon Jones alisema.
Andrew Griffith Mbunge na mkurugenzi wa kitengo cha sera katika ofisi ya waziri mkuu, alisema mpango huo mpya hautahitaji sheria mpya na unaweza kutekelezwa chini ya "mikataba iliyopo".
Mpango wa Rwanda ni sehemu ya mkakati mpana zaidi wa kupunguza idadi ya watu wanaoingia Uingereza kwa kuvuka bahari kwa boti ndogo.
Unaweza pia kusoma:
Jeshi la Wanamaji la Kifalme limechukua uongozi wa vivuko kadhaa kutoka kwa mpaka wa kikosi cha Uingereza katika juhudi za kugundua kila mashua inayoelekea Uingereza.
Mwaka jana, watu 28,526 walivuka bahari, ikiwa ni ongezeko la 8,404 la mwaka 2020.
Tony Smith, mkurugenzi mkuu wa zamani wa kikosi cha Mipaka cha Uingereza, alisema inaweza kuchukua wiki kabla ya kuwa wazi kama mpango huo mpya utatimizwa".
Katika hotuba yake siku ya Alhamisi, Boris Johnson alisema makubaliano na Rwanda yatatoa "njia salama na za kisheria kwa wanaotaka hifadhi".
"Wahamiaji wa kiuchumi wanaotumia fursa ya mfumo wa hifadhi hawataweza kukaa Uingereza, wakati wale walio na mahitaji ya kweli watalindwa ipasavyo," alisema.
Alisema mpango huo utashughulikia mtu yeyote ambaye amefika Uingereza kinyume cha sheria tangu kuanza kwa mwaka huu.












