'Watu wengi wanafikiria kimakosa kuwa Putin anajaribu kuunda tena Umoja wa Kisovieti'-Mwandishi wa wasifu wake

Vladimir Putin

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Vladimir Putin, Rais wa Urusi

Vladimir Putin ni mmoja wa viongozi mpatanishi katika miongo ya hivi karibuni nawakati huo huo ni mtu ambaye ni vigumu sana kumuelewa.

Je, tunafahamu nini kumhusu kiongozi huyu ambaye ameibua mgogoro wa kimataifa? Ni nini kinachomsukuma? Je, mtu huyu mwenye nguvu nyingi anamheshimu nani?

Mwandishi wa habari Steven Lee Myers alitumia miaka saba kama mwandishi wa habari wa Moscow kwa New York Times.

Wakati huo aliweza kukutana na kufanya mahojiano na Vladimir Putin, na pia kuchambua mabadiliko yake madarakani.

Katika mahojiano na BBC Mundo, Myers anamtaja Putin kama mzungumzaji mkuu, mtu ambaye kwake utaratibu na utulivu ni muhimu sana, mwenye kujitolea kwa "kidini" kwa nchi yake na ambaye ana chuki dhidi ya Magharibi.

Katika mahojiano hayo, Myers aliambia BBC kinachompatia motisha Putin, kile kinachojulikana kuhusu wandani wake wa karibu na ni matukio gani yanaweza kumngoja katika vita vyake na Ukraine.

Myers ni mwandishi wa wasifu wa "The New Tsar: The Rise and Reign of Vladimir Putin," na kwa sasa ni Mhariri Mkuu wa New York Times mjini Beijing.

Steven Lee Myers.

Chanzo cha picha, Michael Lionstar

Maelezo ya picha, Steven Lee Myers.
Línea

Umemtaja Putin kama "mtu ambaye anashinda wakati wote",unamaanisha nini?

Namaanisha katika miaka 20 aliyokuwa madarakani, kumekuwa na nyakati kadhaa ambapo watu walidhani mtu huyu hawezi kustahimili changamoto alizokutana nazo.

Kwanza ilikuwa vita vya Chechnya. Kisha wakamlaki kwa maandamano aliporejea kwenye kiti cha urais baada ya kuwa waziri mkuu. Kulikuwa na maandamano makubwa. Wakati fulani kulikuwa na watu milioni moja kwenye mitaa ya Moscow. Watu walikuwa wakisema, "unawezaje kustahamili hali hii?"

Kisha, baada ya kunyakuwa Crimea mwaka wa 2014, uchumi wa Urusi uliathirika sana. Thamani ya ruble ilianguka kwa kiasi kikubwa na haijawahi kuimarika.

Hata hivyo, Putin aliweza kusalia madarakani na kwa namna fulani aliweza kusalia kama kiungo muhimu katika siasa za Urusi.

Ndio maana nikasema, hivyo na kufikia sasa Putin ameweza kuwakatisha tamaa wale waliokuwa na matarajio kuwa atalazimika kuondoka madarakani.

Chechenia, 1994.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Chechenia, 1994.

Mkutano wa ana kwa ana na Putin ukoje?

Nadhani inategemea sana mtu na labda pia na mazingira.

Nilipokutana naye, nilikuwa nimeangazia matukio ya Urusi kwa muda, kwa hiyo nilikuwa tayari nimemfahamu.

Yeye ni mzungumzaji mzuri sana, watu wengine wanahusisha hilo na kazi yake ya KGB. Anakuja kwenye mikutano yake akiwa amejitayarisha vyema.

Anaweza kukumbuka takwimu na kuzungumza juu ya mada mbalimbali kwa undani wa ajabu, bila kuandikiwa maelezo ya ziada.

Ni mtu mkali sana, anaweza pia kuwa na hasira kidogo, na tumeona hilo wakati mwingine anapofoka kwa ghadhabu.

Tazama hotuba yake siku chache zilizopita ambapo alitumia maneno kama "takataka" na "wasaliti." Lugha kama hiyo imekuwa ikisisitiza maoni yake kila wakati, lakini inaonekana sasa anatumia kuliko hapo awali.

Ijapokuwa watu wengine wanamfahamu na wanafurahishwa na mtindo huo, kwa jinsi anavyojihusisha na mazungumzo, hukufanya usikike.

Watu wanaomjua zaidi kuniliko, kama Angela Merkel, kwa mfano, wakati wa mzozo wa Crimea alimwambia Obama kwamba Putin lived anaishi katika ulimwengu mwingine.

Mshauri wa Macron siku chache zilizopiwa alisema kitu kama hicho.

Kwa hivyo nadhani kuna hisia hii ambayo Putin ni, tusiseme mdanganyifu, lakini anaiona tu ulimwengu kwa mtazamo tofauti na watu wanaomzunguka.

Ángela Merkel y Vladimir Putin, reunidos en Moscú en 2020.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Angela Merkel and Vladimir Putin meeting in Moscow in 2020.

Je, kuna tukio lolote katika utoto au ujana wa Putin ambalo limeashiria maono yake ya ulimwengu?

Kuna mambo kadhaa… Naanza kitabu changu kwa kuzungumza juu ya babake Putin na uzoefu wake katika Vita vya Kidunia vya pili. Alikuwa askari ambaye alipigana katika kuzingirwa kwa Leningrad, mzozo wa kutisha kabisa ambao mamilioni ya watu walikufa.

Kwa hivyo vita viliathiri karibu kila familia katika Muungano wa Sovieti, na hiyo inabaki kwenye kumbukumbu ya kihistoria ya utamaduni wao hadi leo.

Nadhani, kwa njia fulani, hatutambui kwamba nchi pekee iliyokuwa na kiwango sawa cha uharibifu ilikuwa Ujerumani yenyewe.

Alikuwa wakati ambapo Muungano wa Sovieti ulianza kutambua juhudi hizo.

Umoja wa Kisovieti, Stalin, haijalishi unawachukuliaje, walishinda Ujerumani ya Wanazi. Inabidi uwape sifa kwa hilo.

Nadhani uzoefu huo, na mazingira ya vita ni kitu ambacho Putin alikua nacho na ni msingi wa tabia yake.

Pia kuna hadithi ambayo yeye mwenyewe anasimulia, na mtu hajui ni kweli kwa kiasi gani.

Anazungumzia hayo katika tamthilia ya kitabu cha 1968 kinachoitwa "The Shield and the Sword."

Ilikuwa mfululizo tamthilia vita ambapo kulikuwa na mhusika ambaye alikuwa kama jasusi aliyejipenyeza katika jeshi la Nazi, na ambaye alisaidia kushinda vita.

Putin alipenda sana tamthilia hiyo, na amesema aliguswa sana hivi kwamba alijaribu mara moja kujiandikisha katika KGB, ingawa alikuwa mchanga sana.

Kwa hivyo, hiyo ilikuwa sehemu ya wazo lao la kutumikia kazi hii kuu dhidi ya Wanazi, ambayo, kama tulivyoona, pia ni sehemu ya lugha yao katika vita vya leo dhidi ya Ukraine.

Putin

Chanzo cha picha, BSTU