Ukraine: Picha za Setilaiti zinaonyesha harakati za kijeshi za Urusi

Chanzo cha picha, Maxar
Picha za hivi karibuni zilizotolewa na kampuni ya ujasusi ya teknolojia ya anga ya Marekani Maxar zinaonyesha kwamba shuguli za kijeshi za jeshi la urusi zimeendelea kuwepo karibu na mipaka yake na Ukraine, licha ya madai ya hivi karibuni ya Urusi ya kuondoa vikosi vyake kwenye mipaka hiyo.
Picha hizo ambazo zilichukuliwa kati kati ya mwezi wa Februali, zinaonyesha kuwa Ukraine bado imeendelea kuzingirwa katika maeneo matatu- kwenye mipaka yake na Urusi na Belarus - na zana za kijeshi za Urusi pamoja na vikosi viko kwenye mipaka hiyo kwa wingi.
Shuguli za vikosi vya Urusi
Kinachotia hofu zaidi ni uwepo wa hospitali za dharura, katika umbali kiasi kutoka kwenye eneo la mazoezi ya kijeshi la Osipovichi kaskazini magharibi mwa Belarus.
Huku hii inaweza kuwa sehemu ya mazoezi makubwa ya kijeshi halali , inaweza pia kuwa ni kiashirio cha maandalizi ya mapigano yanayotarajiwa kusababisha majeruhi kutokana na vita.

Idadi kubwa ya wanajeshi na shuguli za kijeshi pia vinaonekana kuongezeka karibu na mipaka ya Ukraine.
Daraja la kijeshi lililojengwa juu ya mto Pripyat lilipigwa picha tarehe 15 Februari.
Lipo chini ya umbali wa maili 4 (kilomita 6 ) kutoka mpakani mwa Belarus na Ukraine.

Wachambuzi katika huduma za ujasusi katika London-based McKenzie wameonyesha eneo kubwa lililotengwa upande wa nyuma wa mto kama kiashirio cha uwezekano wa kuhamishwa kwa idadi kubwa ya magari.
Picha nyingine ni ya silaha zenye uwezo wa kufanya mashambulizi zenyewe, au aina kubwa ya bunduki inayoweza kupiga kutoka kwenye kifaru, iliyoko kwenye eneo la Brestsky, ambalo liko umbali wa maili 30 (kilomita 50) kutoka kwenye mpaka na Ukraine.

Kuwasili kwa kikosi cha helikopta 20 zenye uwezo wa kuzuwia makombora angani zilizowasili hivi karibuni zilipigwa picha katika uwanjwa wa ndege wa Zyabrovka , uliopo maili 19 (km 30) kutoka kwenye mpaka.
Tathmini ya Kampuni ya huduma za ujasusi ya McKenzie inasema kuna labda helikopta 12 aina ya Hakum za Urusi, Hind tano au Mi-28

Ni muhimu kukumbuka kwamba kuna uwepo wa hivi karibuni wa wanajeshi wa Urusi wapatao 30,000 katika Belarus, wakiwa ni sehemu ya mazoezi ya pamoja yanayojumuisha Ukraine na Nato yaliyopangwa kukamilika tarehe 20 Februari.
Jaribio muhimu la nia za Moscow litakuja baada ya tarehe hiyo wakati picha hizo zitakapofichua iwapo vikosi vya Urusi vilibakia pale au viliondoka.

Picha hizi zinatueleza nini?
Hakuna chochote katia picha hizi kinachothibitisha kabisa kwamba Urusi inakaribia kuivamia Ukraine.
Urusi inaendelea kusisitiza kuwa hili sio lengo lake na kwamba yoyote yanayosemwa kuhusu hilo ni propaganda za magharibi.
Lakini mkuu wa ulinzi wa NATO anaamini kuwa Urusi sasa ina vikosi vya kutosha katika maeneo yanayozingira Ukraine kufanya uvamizi pale Rais Putin atakapotoa agizo la kufanya hivyo.
Kiwango, na ukubwa pamoja na mpango wa Urusi wa upelekaji wa jeshi za zana za kijeshi wa karibu na mipaka yake na Ukraine vinadhihirishwa na kwa mfano, vikosi vya ulinzi vilivyoletwa kutoka maeneo ya mbali kama vile mashariki mwa Siberia ambako ni umbali wa maili maelfu kadhaa.

Chini ya uongozi wa Putin jeshi la Urusi limepitia mabadiliko makubwa kuanzia siku za giza za miaka ya 1990 kufuatia kuanguka kwa Muungano wa Usovieti.
Mambo mawili yametokea ambayo yamelifanya jeshi la Urusi kuwa kikosi cha kutiliwa maanani.
Kwanza kabisa, kiasi kikubwa cha pesa za taifa kimewekezwa katika kuboresha na kuliweka katika hali ya kisasa jeshi, zana , silaha, na ujusi wa mtandao -dhidi ya mashambulio ya hivi karibuni ya kimtandao, kupanga upya vikosi vya vita katika ''Makundi ya bataliani yanayoweza kutekeleza majukumu yanayotarajiwa'' ya takriban wanajeshi 800 yakisaidiwa na vifaru, makombora na silaha nyingine.
Pili , makamanda wa Urusi na wapangaji wametumia miaka saba iliyopita kupata uzoefu wa vita katika mataifa ya Syria na mashariki mwa Ukraine. Ufanisi wa silaha zao zimepimwa katika maeneo ya vita na makamanda wa Urusi .wamejifunza kutokana na makosa yao.
Yote hayo yakizingatiwa pamoja, wachanganuzi wa magharibi wanaamini kuwa Moscow, ilichagua kuendelea kuwa na idadi kubwa ya wanajeshi wake na uwepo wa tisho la jeshi lake karibu na mipaka ya Ukraine kwa wiki kadhaa, kama sio miezi kadhaa inayokuja.













