Imani kuwa pombe ni ya kustarehesha ilitoka wapi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya siku ndefu na yenye changamoto, mara nyingi mimi hujikuta nimeketi na bia au glasi ya divai.
Taratibu kama hizi ni ishara kwamba siku ya kufanya kazi imekwisha na kwamba wakati wa kujifurahisha na kupumzika umefika.
Tatizo ni kwamba baada ya muda tabia hii ya unywaji pombe haifanyi kazi tena.
Matumizi ya pombe ya mara kwa mara na kupita kiasi uhusishwa na mafadhaiko na usingizi mbaya.
Hata hivyo, wazo kwamba pombe hupumzisha bado ni imani yenye nguvu.
Kuna ushahidi kwamba watu wengi walianza kunywa zaidi wakati wa janga la covid-19 ili kujaribu kupumzika.
Kwa kuangazia historia ya pombe kunaweza kutoa uelewa fulani kwa nini imani hii imeenea.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sababu za kimatibabu?
Katika historia, pombe mara nyingi imekuwa ikitumiwa kwa matibabu na inachukuliwa kuwa yenye manufaa muhimu.
Nimesoma jinsi watafiti wa karne ya 19 na mapema karne ya 20 walivyotumia kinywaji hicho.
Kuchunguza tabia za wasafiri kunaweza kutoa uelewa kimatibabu wa pombe.
Kwa sababu, katika enzi kabla ya majaribio ya kimatibabu, waandishi wa matibabu waligeukia simulizi za watafiti kukusanya ushahidi kuhusu athari za kiafya za vyakula na vinywaji tofauti.
Kwa hiyo, maandishi hayo yanaweza kutusaidia kuelewa uhusiano kati ya pombe na afya.

Chanzo cha picha, GETTY/SCOTT POLAR RESEARCH INSTITUTE
Kwa kweli, wagunduzi wengi wa Aktiki ya VictArctic walikunywa glasi ya mvinyo "kupata joto" mwishoni mwa siku ndefu ya kuteleza.
Walisema iliwasaidia kulala, kupumzika na kupunguza usumbufu.
Pia wasafiri wa Uingereza katika Afrika Mashariki mara nyingi walikunywa kiasi kidogo cha pombe mwishoni wa safari ya siku.
Waliiona kuwa "dawa" yenye manufaa ambayo iliwasaidia kukabiliana na athari za homa na mikazo ya kihisia ya kusafiri.

Chanzo cha picha, Getty Images
Afya na usawa
Kwa kiwango ndogo, pombe inaonekana kama kichocheo, kwani hufanya moyo kupiga haraka, na kutoa nguvu zaidi.
Lakini baadaye huzuia mfumo mkuu wa neva, na hivyo kupunguza kasi ya mtu kufikiria na kuchukua hatua
Athari hizi za kiafya zilikuwa muhimu sana katika matibabu mwanzoni mwa karne ya 19, kwani baadhi ya wataalamu wa kimatibabu waliuona mwili kama mfumo ambao ulipaswa kuwekwa katika usawa.
Na vichocheo au dawa za kupunguza mafadhaiko zilionekana kuwa njia muhimu za kurejesha nafuu ikiwa mtu alikuwa akijisikia vibaya.
Baada ya muda, maoni haya yalipoteza umaarufu miongoni mwa wanasayansi na madaktari, na kubadilishwa na nadharia ambazo zilitaka kujua sababu za maambukizi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukosoaji kwa unywaji pombe
Kubadilisha mitazamo ya kimatibabu kuhusu magonjwa haikuwa sababu pekee ya kupunguza unywaji wakati wa safari za utafiti.
Ukosoaji unaokua wa unywaji wa wasafiri hao pia ulitokana na mabadiliko ya mitazamo ya kimatibabu na kijamii kuhusu pombe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii ilitokana na kampeni iliyojikita katika Ukristo wa kiinjilisti ambayo ilitaka kukatisha tamaa na wakati mwingine kupiga marufuku moja kwa moja uuzaji wa pombe.
Hata wale ambao walipata unywaji wa pombe wa wastani unakubalika walianza kuwa na wasiwasi kwamba inaweza kuwa hatari zaidi katika hali ya hewa.
Kwa mfano, msafara wa Arctic (1875-1876) ulikosolewa kwa kusambaza mgao wa pombe, kwa madai kwamba ulikuwa umechangia kuzuka kwa ugonjwa, ambao unadaiwa kusambaa miongoni mwa wanywaji pombe wa kupindukia wa msafara huo.
Ukosoaji kama huu ulimaanisha kwamba watafiti walizidi kusisitiza kwamba unywaji wao ulikuwa wa wastani na wa kimatibabu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vichocheo: pombe au kafeini
Kama utafiti wa hivi majuzi wa unaonyesha, vichocheo vikiwemo pombe vilibakia kuwa dawa maarufu kwa wasafiri wa Ulaya barani Afrika hadi mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii ilikuwa kwa sababu zilikuwa za bei nafuu, rahisi kutumiwa, na zilikuwa na athari zinazoonekana kwenye akili na mwili wa mnywaji.
Pia waliaminika kueneza imani kwamba hali ya hewa ya joto ilikuwa na madhara ya kimwili na ya kisaikolojia.
Wasafiri wengine waliviona vileo kama vichocheo muhimu ili kusaidia kukabiliana na athari hizi.
Hata wale waliopinga unywaji bado waliona vinywaji vya kusisimua kuwa muhimu, lakini badala yake walishauri kikombe cha kahawa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uelewa wa kimatibabu wa kinywaji hicho umebadilika sana katika miaka 150 iliyopita.
Kwa sasa, mazoea ya kunywa huamuliwa sio tu na sababu za matibabu, lakini pia na mitazamo ya kitamaduni kwa vinywaji tofauti na sehemu ambazo tunavitumia.












