Unawezaje kumfukuza kazi mtu kwa njia ambayo ni ya ukarimu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Miaka miwili baada ya kupata mrejesho chanya kutoka kwa mameneja wake katika kampuni ya masuala ya fedha , André Santos alishangaa baada ya kupokea simu kutoka katika ofisi siku moja.
Afisa wa masuala ya wafanyakazi alikuwa na ujumbe mfupi kwa ajili yake: kampuni ilikuwa inapitia mabadiliko na André alifutwa kazi mara moja.
"Nilikanganikiwa. Nikasema, unamaanisha nini?" André anakumbuka. Lakini kulikuwa hakuna maelezo zaidi. Hapakuwa na simu kutoka kwa meneja wake wa zamani.
Wakati ule, André alikuwa ameoa na alikuwa na mtoto wakiume mwenye umri wa miaka mitano, na mke wake hakuwa anafanya kazi. Wawili hao walikuwa wakiishi Rio de Janeiro, Brazil.
Alielekea ofisini kurejesha kitambulisho cha kazi, kuchukua vitu vyake na kuondoka kwenye jengo la ofisi, akilia.
"Nilitikiswa," aliiambia BBC. "Wakati simu yangu ilipolia, unafikiria kitu kingine chochote lakini sio kufutwa kazi. Ni wakati ule ambapo niligundfua kuwa hakuna kitu kama 'tuko familia moja. Ni kila mtu peke yake."
Bahati ya André' ilichukua mkondo mpya. Alikuwa mshawishi katika sekta yake-lakini wakati ule, kufutwa kazi kwa ukatili kulimfanya awe mwenye huzuni.
Inaeleweka kabisa kuwa katika hali hiyo kwa mtu yeyote kufutwa kazi bila , wataalam wanasema. Lakini sio lazima iwe hivyo.
'Kiwango fulani cha ubinadamu'

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kufutwa kazi kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtu binafsi na hatuwezi kusema kujua kuzema ukweli hii itakuwa na maana gani kwao binafsi," anasema Gemma Dale, mhadhiri wa kitivo cha biashara na sheria, katiak chuo kikuu cha Liverpool John Moores cha Uingereza.
Kufutwa kazi kwa ukarimu
Wataalamu wanasema inawezekana kumfuta kazi mtu kwa njia ya ukarimu. Ingawa hakuna sheria ngumu na za haraka, huwa kunakuwa na mambo makuu matatu : uwazi, huruma na usaidizi.
"Kama kiongozi unahitaji kuweka matarajio na uwe wazi kuhusu jinsi watu wanavyoweza kufikia matarajio na kuyavuka ," Glickman aliiambia BBC.
Kama sababu ya kufuta kazi inahusiana na matokeo ya kamouni, basi viongozi wanapaswa kuwa wazi kuhusu matatizo ya kifedha yanayoikumba na kuwafahamisha waajiriwa kuhusu habari mbaya inayotarajiwa kuja.
Glickman anasema viongozi wazuri lazima wafahamu kuwa kufutwa kazi ni vigumu, na ''kuwapatia muda wa mpito'' wafanyakazi wanaotaka kuwafuta kazi.
Dale anasema kuwasaidia waajiriwa kuandaa CV zao, , pamoja na kuwapatia fursa ya idhini yako kama muajiri ambaye waajiri wengine wanaweza kukuuliza kuhusu utendaji wao inaweza kusaidia kupunguza mengi ya matatizo yao.
'Utamaduni mbaya'

Chanzo cha picha, Getty Images
Suala la Dale liliibua mjadala kuelekea mwishoni mwa mwaka, baada ya mkuu wa kapuni ya utaoaji wa mikopo ya Marekani Better.com, Vishal Garg, kuwashitukiza wafanyakazi wake 900 kwa kuwafuta kazi kupitia mawasiliano ya mara moja ya mtandao ya Zoom.
"Kama uko katika mawasiliano haya ya simu ya mtandao, wewe ni sehemu ya kikundu kisicho na bahati kinachofutwa kazi", Mkurugenzi mkuu aliwashanga waajiriwa ambao walishtkizwa na taarifa hii bila kujua.
Glickman anasema kumfuta kazi mtu "sio mazungumzo yanayopaswa kusikika mbele ya watu wengine "
"Wakati unapowafuta umati wa watu 900 kupitia Zoom...inaonyesha kutojali na hata ukatili, ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni muda mfupi kabla ya mapumziko ya Krsimasi. Unawaacha watu katika hali ya mbaya na ladha ya ubaya kwa muajiri wao wa awali ," anasema.

Chanzo cha picha, Great on the Job
Baada ya kupata lawama kutoka maeneo mbali mbali ya dunia, ilitangazwa mara moja kwamba Garg alichukua likizo kutokana na makosa mengi ya kiuongozi.
Dale anasema tukio hilo linaonyesha jinsi kushugulikia vibaya kwa suala la kufuta kazi kunavyoweza kuwa na athari mbaya kwa mahusiano ya umma(PR)
Kampuni yenye sifa chafu inaweza kuwa na changamoto ya kuajiri wachache wenye vipaji.
Kuhisi kutothaminiwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kupata lawama kutoka maeneo mbali mbali ya dunia, ilitangazwa mara moja kwamba Garg alichukua likizo kutokana na makosa mengi ya kiuongozi.
Dale anasema tukio hilo linaonyesha jinsi kushugulikia vibaya kwa suala la kufuta kazi kunavyoweza kuwa na athari mbaya kwa mahusiano ya umma(PR)
Kampuni yenye sifa chafu inaweza kuwa na changamoto ya kuajiri wachache wenye vipaji
'Walinifuta kazi, halafu wakataka nirejee'
Hivi sio jinsi André alivyojihisi baada ya kufutwa kazi, ingawa anasema hahisi hisia zozote kumuhusu muajiri wake.
Lakini anasema alikanganyikiwa sana wakati kampuni ilipompigia simu wiki kadhaa baadaye na kumuomba arejee kwenye kazi yake ya zamani tena.
Anaomba radhi kwa kushindwa " kuonyesha heshima inayofaa na shukran kwa watu binafsi ambao waliathriwa na kwa mchango wao katika kampuni ya Better" na kuongeza kuwa : " Nachukua jukumu la kufuta kazi , lakini katika mawasiliano nilikosea utekelezaji ."
Lakini Glickman hajaridhishwa sana na hatua zilizochukuliwa. Anasema kufuta kazi kunaeleza mengi kuhusu utamaduni wa kazi wa kampuni, jambo ambalo lililojitokeza katika kampuni ya Better.com lilielezewa kama "sumu".
"Kuwafuta kazi watu 900 kwa pamoja kwa njia ya Zoom inaonyesha utamaduni ambao hauwajali waajiriwa ," anasema.

Chanzo cha picha, Andre Santos
"Walisema kulikuwa na makosa na wakaniomba nirudi kazini. Na bila shaka , Nilisema hapana. Nilikuwa bado nafanya mtihani wa kazi na sikuwa na kazi, lakini niliona bora nisikubali kurejea kazini ," anasema André.
"Kusema ukweli, nilisema ningekuwa sijafutwa kazi, ningeishia kuacha kazi mapema, kwasababu hayakuwa mazingira mazuri na yanayotia moyo kikazi."
Leo,André anafundisha kozi kuhsuu jinsi ya kuuza. Juhusdi zake za kuwasiliana na watu katika miaka iliyopita hususan kupitia mtandao wa LinkedIn - zimemsaidia baada ya janga la covid kuikumba dunia, kwani aliweza kupeleka biashara yake kwenye mtandao.
Analipwa kutokana na kauli yake kwenye jukwaa, lenye mawasiliano ya mtandao ya watu 30,000 na ufuasi wa watu zaidi ya 300,000. Jumbe zake zimetazamwa na zaidi ya mara milioni 100.
Unaweza piakusoma:
André anasema kujigeuza mwenyewe kuwa chapa kulimpatia uhuru.
"Wakati tunapoajiriwa, ni kama tuna thamani zaidi.
Watu hutaka kuwa marafiki zetu. Lakini tunapofutwa kazi, baadhi ya marafiki zetu hutoweka.
Jambo hili sio zuri kwa afya yako," anasema.
"Niligundua kuwa nilipaswa kuwekeza katika mtandao wa mawasiliano yangu na chapa yangu ili kuhakikisha kila mara nina thamani -iwe nimeajiriwa au sijaajiriwa, ndani au nje ya ajira ."













