Manamke wa Kinigeria ambaye maisha yake yalibadilika baada ya kukutana na wagonjwa wa ukoma

Chanzo cha picha, Iby Ikotidem
Katika mfululizo wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa Kiafrika, mwandishi wa riwaya kutoka Nigeria Adaobi Tricia Nwaubani anaandika kuhusu mwanamke ambaye maisha yake yalibadilika baada ya kupata ugonjwa wa ngozi na baadaye kutembelea watu wenye ukoma.

Iby Ikotidem alizoae sana maesha ya anasa. Alipendelea mitindo ya mavazi na vito vya thamani, alikuwa na marafiki wengi na kalenda yake ya shughuli ilikuwa imejaa, mara nyingi akiandaa matamasha katika Jimbo la Marekani la New Jersey, ambako ameishi na mume wake na watoto wao wawili kwa kipindi cha miaka 28 iliyopita.
"Nilikuwa na haiba ya juu katika ulingo wa burdani," alisema.
Lakini yote hayo yalikoma muda mfupi baada ya ngozi kavu kuonekana kwenye goti lake miaka 12 iliyopita, wakati biashara yake ya mali isiyohamishika ilipoanza.
Haikuchukuwa muda mrefu kabla ya hali hiyo kusambaa mwili mzima isipokuwa uso wake.
Kufuatua msururu wa uchunguzi wa kimatibabu, alipatikana na psoriasis, ugonjwa ambao husababisha seli za ngozi kujiunda na kuunda magamba yenye mwasho ambayo humuachia mwathiriwa mabaka baada ya kujikuna.
'Kioo kilikuwa adui yangu'
Hata alipovaa blauzi za mikono mirefu na sketi ndefu na kujifunika ili watu wasitazame, hali yake bado ilivuta hisia kila alikoenda.
Wakati fulani alipoinuka kutoka kwenye kiti, watu walishangaa kwa mshtuko "vumbi" kwenye sakafu ghafla limetokea wapi.
"Nilichukia kujiangalia. Kioo kilikuwa adui wangu," alisema.
Mara, unyanyapaa ukaanza.
Bi Ikotidiem anakumbukakisa kimoja ambapo alikuwa miongoni mwa wageni katika hafla ya wikendi katika nyumba ya rafiki yake - aliwekewa godoro katika chumba cha chini ya ardhi wakati watu wote walipelekwa kulala katika vyomba vya juu vya wageni.
"Nilikaachini sakafuni , nikalia sana," alisema.

Chanzo cha picha, Iby Ikotidem
Bi Ikotidiem alijitenga, kunyoa nywele zake- na maisha yake yalibadilika kabisa hadi mtoto wake wa kike wa miaka 12- alipomwambia: "Mama, wewe ni shujaa wangu. Tafadhali naomba usikubali huu ugonjwa ukumalize.'"
Bi Ikotidem alisema: "Tamko hilo liliyeyusha mawazo yote niliyokuwa nayo ya kujitoa uhai."
Mwaka ambao alipatikana na ugonjwa huo, watoto wake walialikwa kujiunga na kikundi cha vijana nchini Marekani kutoka jimbo la nyumbani la Akwa Ibom, ambako wangejitolea kufanya kazi ya hisani.
Mwanawe wa kiume, Anthony, wakati huo akiwa na miaka 15, alisistiza mama yake aandamane naye. akakubali shingo upande.
Walitembelea nyumba kadhaa za mayatima - ziara ambayo iliangaziwa na vyombo vya habari vya nyumbani.
Wakati anapata kiamsha kinywa hotelini asubuhi moja,Bi Ikotidem alifikiwa na mwanafunzi mwenza wa zamani ambaye alimsifu yeye na vijana kwa kazi yao na kupendekeza waeneze kampeni yao kwa makazi yawagonjwa wa ukoma katika jimbo hilo.
"Nilishangaa: 'nikauliza yaani! bado kuna ukoma nchini Nigeria?'" Ikotidem alisema. "Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuua kwamba bado kuna kuna ukoma duniani."
Licha ya kutokomezwa kama tatizo la afya duniani, ukoma bado umeenea nchini Nigeria, huku zaidi ya wagonjwa 3,500 wakigunduliwa kila mwaka, kulingana na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha nchi hiyo.
Ugonjwa huo wa bakteria unaweza kutibika iwapo utagunduliwa na kutibiwa mapema lakini usipotibiwa unaweza kusababisha madhara makubwa kwenye mikono na miguu na hata kupooza na upofu.
With limited funding from a government that has many other public health priorities, leprosy colonies in Nigeria tend to depend mostly on international charities"

Baadhi ya wazazi walisitasita wakati Bi Ikotidem alipotaja kwenda katika Hospitali ya Ukoma ya Ekpene Obom lakini hatimaye wote waliandamana naye - ziara iliyobadilisha maisha yake.
Sawa na hospitali zingine za ukoma nchini Nigeria, Ekpene Obom pia inatoa malazi kwa wagonjwa ambao hawawezi tena katika jamii zao asili kutokana na unyanyapaa.
Hata baada ya kuponywa ugonjwa huo ambao unaweza kutibika ndani ya miezi sita hadi 12 kwa kutumia dawa za antibaiotiki, wanasalia hapo na familia zao, watoto wao pia wakisoma shule ndani ya majengo hayo.
Bi Ikotidem aliwaambia wakazi na wagonjwa kwamba anaelewa masaibu yao.
"Nilijua nini maana ya kutelekezwa na kutazwa kwa mshanago," alisema.
Kuuza vito vyake
Katika muongo mmoja uliopita, Bi Ikotidem amefanya kuwahudumia wagonjwa wa ukoma kuwa dhamira yake ya maisha.
Kupitia Hope's Door (Mlango wa Matumaini), wakfu aliyoanzisha, ameelekeza kazi yake hadi sasa kwenye makoloni matatu kusini na kaskazini mwa Nigeria.

Chanzo cha picha, Getty Images
Miongoni mwa usaidizi mwingine anawapatia viatu maalum, magongo ya kutembelea na viti vya magurudumu. Anawapa watoto wao vifaa vya kuandikia shuleni. Anakarabati maeneo yao ya makazi.
"Ungeliona godoro ambazo walizokuwa wanalalia ungesikitika kwani hata mbwa wako hawezi kulia," alisema.
Kwa ufadhili mdogo kutoka kwa serikali ambayo ina vipaumbele vingine vingi vya afya ya umma, makoloni ya ukoma nchini Nigeria hutegemea zaidi misaada ya kutoka kwamashirika ya kimataifa, kama vile The Leprosy Mission.
"Wanapokuwa na matatizo , wananipigia simu, sio serikali," alisema Bi Ikotidem, ambaye mradi wake wa awali ulikuwa kuuza vito vya dhamani na kuandaa shughuli za kuchangisha fedha na kuwaleta marafiki pamoja.
Mradi wake mkubwa unaofuata ni kuwasaidia wakazi wa makoloni kutokuwa tegemezi, kwa kuwapa miche na zana za kilimo kwenye ardhi yao.
"Naenda kulala nikifikiria hii jamii na kuamka nikiwaza kuwahusu," Bi Ikotidem alisema.
"Kutokana na psoriasis, Nilipata wito wangu, na katika wito wangu, nilipata uponyaji wangu."
Barua zaidi kutoka Afrika:













